Akisimulia tukio hilo, kaka wa mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mbwana, alisema tukio hilo lilitokea asubuhi ya Julai 6, mwaka huu, wakati akienda msalani aliposikia sauti ya kichanga ikilia kutoka chumbani kwa dada yake, hali aliyoiona siyo ya kawaida kwani hakuwa na mtoto.
Kuona hivyo, alisema alikwenda na kugonga mlangoni kwa dada yake huyo, lakini hakufungua mpaka alipoamua kuvunja mlango. Cha kushangaza, alisema alimkuta akiwa kama aliyechanganyikiwa, akijifanya kufagia huku damu zikiwa zimetapakaa ndani.
Fadhila mwenye umri wa miaka 30, anadaiwa kumvunja mguu mtoto wake mwenye umri wa siku moja, akiwa katika jaribio la kumuua..soma zaidi >>>>>>>>