WASICHANA saba wamepoteza maisha wilayani Nachingwea mkoani Lindi baada ya kubakwa na kunyongwa kisha kuwekewa vijiti na chupa kwenye sehemu zao za siri.
Wasichana hao wamepoteza maisha kwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi minne iliyopita na wamekuwa wakipigiwa simu nyakati za usiku na kukutana na waliwapigia simu ambapo hubakwa na kunyongwa na kisha katika sehemu za siri kuwekewa vijiti au chupa.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila amebainisha aina hiyo ya mauaji jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine.
Mwananzila alikuwa amekwenda hospitalini hapo kuwatazama majeruhi ambapo alifafanua kuwa mauaji hayo yanaendelea na juzi mtu mwingine aliuawa katika mazingira hayo.
Mwananzila alisema kuwa binti mmoja aliweza kupigiwa simu na kundi hilo, aliamua kupiga simu kituo cha polisi na kuweka mtego baada yeye kutoka nje, polisi walikuwa wameshazingira maeneo hayo na wauaji wale walimfuata ndipo huyo binti alianza kuvutana nao na hatimaye Polisi waliwatia mbaroni watu hao. Mkuu huyo wa mkoa aliwaonya mabinti hao na kusema: “ni makosa kwa wasichana kutoka nje baada ya kupigiwa …
Alisema mauaji hayo yana ishara ya imani ya kishirikina. Hata hivyo uchunguzi unaendelea kufanyika. Alisema suala hilo liko ndani ya uchunguzi hivyo ni vizuri kufanyia kazi kwanza na kuwataka wananchi wawe na subira.