Mama mzazi wa star anayeipeperusha vizuri bendera ya Tanzania kimataifa kwa sasa kupitia muziki, Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz jana (July 11) alipata nafasi ya kuzungumza na paparazi, mambo mbalimbali yanayomhusu mwanaye.
Haya ni baadhi ya maswali ambayo aliulizwa na paparazi, pamoja na majibu aliyoyatoa:Kuhusu tuhuma za Diamond kujihusisha na ushirikina katika muziki wake:
“Hiyo si kweli na wala hana ushirikina, si unajua tena mtu ukiwa juu kila mtu atakusingizia anachowaza yeye ili apate sifa ajulikane…Havijatokea watu uzushi tu wanapenda sasa ushirikina wa nini , kama mtu upo juu upo juu kama upo chini upo chini, nay eye sasa hivi ni nafasi yake kama sio nafasai yake atashuka walikuwepo wangapi, alikuwepo Mr Nice alikuwepo juu, lakini zamu yake imefika imeshuka imekuja zamu ya Nasib wacha awe juu itakapofika yake kushuka atashuka”.
“ Siipokei vizuri laikini sasa nitafanya nini nay eye star, wengine wanajitongozesha bila kutongozwa..mi mwenyewe hapa kutwa napigiwa simu mpaka nazima, wananipigia simu wanafikiria Nasib wanajitongozesha mpaka nawatumia meseji mbona mnajitongozesha, hii sio namba ya Nasib hii namba katoa ya biashara ya Tshirt 0716186318 sio namba ya Diamond, namba yake mama yake.sitaki usumbufu..wananitumia mapicha ya uchi , mapicha ya nini sasa ni ustarabu gani huo”>>>