Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

AIBU:WABONGO WAFUMANIANA CHINA....WAZICHAPA KAVUKAVU,WAVUANA NGUO BARABARANI NI NDANI YA SWAUM KALI

$
0
0
 Warembo wawili, raia wa Tanzania (Wabongo), mmoja akifahamika kwa jina moja la Glory na mwingine ambaye jina halikupatikana wakikwidana.

Ni aibu kubwa kwa taifa! Huku Waislamu wakiendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, warembo wawili, raia wa Tanzania (Wabongo), mmoja mkazi wa Sinza, Dar aliyetajwa kwa jina moja la Glory na mwingine ambaye jina halikupatikana, wanadaiwa kufumaniana laivu nchini China na kugeuka kituko cha aina yake, Ijumaa Wikienda ndilo lenye uthubutu wa kuripoti tukio hilo.Habari za awali zilidai kuwa Glory ndiye aliyemfuma mwenzake na bwana’ke, raia wa Nigeria kisha kumshushia kipigo kabla ya kutoana nje na kwenda kuchaniana nguo barabarani, mchana kweupe.


OFM KUTOKA GUANGZHOU, CHINA
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu, mwakilishi wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers nchini China (jina kapuni), alisema kuwa akiwa katika pitapita zake za kukusanya matukio ili kuyatuma Bongo kuonesha jinsi gani Wabongo wanavyoidhalilisha nchi yao ughaibuni, wikiendi iliyopita alitembelea eneo la Guangzhou Rujing Lu Sky Coffee nchini humo ambalo Watanzania wengi hufanyia ‘biashara’ zao.

Raia hao wakizichapa kwa ghadhabu.

Mwakilishi huyo wa OFM alisema akiwa eneo hilo linalosifika kwa matukio na starehe za kichumbani ndipo alipokumbana na timbwili hilo ambalo linaichafua taswira ya Wabongo ambao wanakwenda China kuchukua biashara mbalimbali.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>