Staa wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka akiwa na familia yake.
Cherekochereko! Baada ya maswali ya muda mrefu na kwamba ndoa hakuna, hatimaye mipango kabambe ya ndoa ya staa wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka na mchumba’ke, Malick Bandawe imekamilika ambapo sasa siku zinahesabika.Kwa mujibu wa Malick ambaye pia ni msanii, kulikuwa na maandalizi ambayo yalikuwa yakiendelea hivyo kwa sasa kila kitu kipo sawa na kinachosubiriwa ni kugawa kadi ambazo zitakuwa zinaonesha tarehe ya ndoa.
“Sasa hivi dogo amekua, anaweza kufanya fujo mbili-tatu hivyo kinachofuata ni ndoa, kadi zitaanza kugawanywa soon,” alisema Malick ambaye ni baba wa mtoto mmoja aliyezaa na Rose Ndauka.