Nimekunwa mnoooooo na hii post ya Mange huko www.u-turn.co.tz hii post nimecopy ukitaka orijino ya Mange nenda www.uturn.co.tz

MANGE ''Hivi siku hizi ndo imekuwa fashion ndoa zikiharibia mnaenda elezea kwenye media? sijaelewa……''

JOY 'Marioo wanaomba uruma ya watu badala ya kuangalia tatizo la msingi...
Dida nakuaminia mwakani ndoa ya nne, chezea Dida wewe mbona wao wanaoa na kuacha kutwa napenda kuona wanawake nao wakivaa suruali lol…..''

JOY 'Mie nilisema hata 100 ntafunga nini nne'

MANGE ''PS. Wanaume wengine wanachekesha, mtu hela huna alafu unataka kumchunga chunga mkeo, hivi mmenotice kuwa matajiri hawanaga hizo za kuchunga mke?

Maana anajiamini anajua anakulisha anakuvisha huwezi kwenda popote, wasio na pesa sasa? uwiiii ni headache atataka akugande ka luba maana anajua dizaini akitokea mwenye nazo waweza sepa lol……''

JOY ' Fact

MANGE ''Bongo ni noma mwanaume anasema kabisa kwenye video nilimchampa vibao na nikamchapa na mikanda kwenye makalio and nobody does nothing, (Joy ' Halafu tunajiita watetezi wa Haki za Wanawake TZ!) ..

MANGE 'Kukaa ukae kwangu mikanda unitandike, hapana aisee….Joy 'huyo mwenyewe alochapwa hajaenda polisi wala hajasema kitu, hapo utamsaidiaje?

Na kama mtu kama Dida ananyamaza bila kupaza sauti wale weenzangu na mie waoga wataweza kuvunja ukimya kwa Ukatili wanaotendewa? uliona yule mwanamke aliyefumuliwa rasta bila chanuo? nilifuatilia nikaambiwa yule ni mahaba ninyonge!

MANGE ''Nimeona kuna wale wanaosema huyu kaka anaonekana mtu fresh kutokana na maelezo yake kwenye video ila Dida ndo hana heshima, naona nyie hamuwajui wanaume.

Hata siku moja usim judge mwanaume akiwa kapupu, mjudge mwanaume akiwa na pesa. Wakiwa hawana kitu wana jua maadili yote, Quraan nzima wanaijua, dini wanaiheshimu, wake wanawaheshimu yani wewe mwanamke ndo utaonekana chizi.

Sasa subiri apate pesa ndo utamjua yeye ni nani hiyo dini ataiwekea na remix zake mwenyewe na hivi mwuislamu basi akuletee na bi mdogo……'' hapa sitii neno dada Umesomekaaaa ILA UMESAHAU MAHABA YOTE UTAPATA...

MANGE HAPA UKAZIDI KUNIPA GAGA SUKO LA MOYO ''Embu ulizeni wanawake waliotoka mbali na waume zao walioanza nao tangu wanapanda mabasi wengine wanakwambia mume wake alikuwa kashika dini hata pombe hanywi baada ya kuzipata weeeeeeeh ni balaa.

Kwa hiyo hata huyu mume wa Dida lazma awe mpole hivyo na mkarimu na kutaja mambo ya Quran sijui nini, ikitokea siku akapata pesa ndo true colors zake zitatokea.

Lazma awe na busara hivyo mtu unaishi kwa mwanamke alafu ujitie mjanja si ndo maana inabidi awe mpole…..'' NOTED au MSG DELIVAD

HAYA SASAAA MANGE HAPA NDO UMEUA ''Ila na huyu kaka nae iwe fundisho kwake next time aende akachukue mke kijijini amlete mjini, yani mwanamke atamweshimu vile anavyotaka yeye.

Maana akifikiria mume wake kamtoa kijijini kamleta Daslam, kamnunulia weaving hata zile za wachina za sh. elfu 8, uwiii mwanamke mbona atamwamkia na yeye kweli hapo atakuwa baba mwenye nyumba na heshima zote anazotaka atapewa.

Ila akienda tena kuoa mwanamke aliemzidi akaishi kwenye nyumba ya huyo mwanamke alafu afikirie atakuwa anatengewa chakula mezani na kuwekewa maji bafuni akaoge atakuwa hayuko serious.

Amake sure next time yeye ndo provider la sivyo itakuwa kila mwaka anaenda magazetini kulia lia mke hamweshimu……..'' VERY TRUE! kama unataka kumfunga kamba kuku wako kamchukue bushi...

NYONGEZA...
Mwanaume suruali inahusu wakina mama wenzanguuuu? jamani tuache unafiki Mapenzi mwenzake Pesa! wanaojua hivyo tunajituma hata usipopata nyingi lakini unaonekana mtu unavyobangaiza!

Mtu unatakiwa usiwe keroro kwa mwenzako jamani! hakuna mwanamke anaependa mwanaume ambae ni tegemezi jamani eh! Kama ambavyo sasaivi hakuna mwanaume anaetaka mwanamke Goli kipa.

Maisha ya sasa ni magumu sana sana. kwa hiyo pambana ili uweze kulipa japo some bills kwa mahitaji yako na ya familia yako!

Heshima ndo inakuja hapo bandugu! heshima si kucheza ngololo! eti umeolewa badala msaidiane maisha inakuwa ndo umejitwika ZIGO! ni shiiiidraaaa jamani mwe! Bill za maisha ugaramie wewe, za watoto na za mwanaume tena kijana mwenye nguvu zote ugaramie wewe kweeeli! kiruuu haihusu kweliiii...

Mwanamke unajitahidi kufanya kazi usiku na mchana, mwenzako kazi ni kuingia sheli na kwenye mabutiki kwa pesa ya mkewe, kutwa yupo Insta na FB halafu anasubiri na usiku acheze ngololo! halafu anataka akupande kichwani MBUTAAAAAA..Hiyo haipo ivyo...

TANGAZO TANGAZO

TUMESHAWACHOKA NA TUMEANZA OPERESHENI TOKOMEZA MARIOOO NA KINABUSHOKE, TUNATAKA KUWAONA MKIJITUMA KUHUDUMIA FAMILIA ZENU NA WAKE ZENU, Ngololo tumezichoka na zinatuzeesha! Mwanamke tangu ujiozeshe hujui hata mafuta ya AYU toka kwa mpenzi! yaani wewe tuu ndo unamnunulia kila kitu jamani ote mae!

Hii ishu imekuwa ngumu sana kwa sisi wanawake kuiongelea, kazi tumebakia kuongelea masalon, mabotiki na sehemu zingine ambazo tunakutana lakini si kwenye majukwaa na wao wayasikie.

Nimewahi kuwashawishi kwamba njooni kwenye kipindi tuliweke wazi hawa kina Marioo wajijue na wajitambue huenda wakajirekebisha maana tumewachoka, waliruka kimanga! kwa kifupi Wanawake wengi si wote bali walio wengi haya ndo maisha yetu siku hizi.

hadi tunatamani kurudi zamani, ambapo mama zetu kazi yao kubwa ilikuwa ni kuzaa.. siku hizi tunatafuta pesa mpaka dakika za mwisha kabisa yaani mtu unatoka kazini unaenda LEBA kuzaa!

Wanaume kuweni na Huruma! kama haitoshi mahari tunajilipiaga, gauni la harusi twajinunulia hadi suti ya mumeo wanunua Harusi tunafanya Yeleuuuuwiiii!!! kuna Mwanamke mmoja aliniambia kwamba asipoimba yaani asipopata dili ya kwenda kuimba nyumbani hawali..mumewe anategemea sauti ya mkewe tuu.

Mwanaume ana nguvu zake, ana akili zake, tatizo ni USHARO UHARO hawataki kujituma....SWALI TUNALOJIULIZA NI KWANINI HAMPENDI KUJITUMA KUTAFUTA PESA??? MNAPENDA SANA MATUMIZI KULIKO KUTAFUTA PESA NA MNAJIDANGANYA NA NGOLOLO MWE!

Tumeshawachoka kuwabeba sasa tunawatua chini tunawabwaga mazima, na sisi tunadandia wenye kujituma na kutambua wajibu wao kwetu na familia bila kusukumana! yaani kuna watu wanajua kujali jamani, anajali mke hadi watoto.

Kwani sisi hatutaki kula Raha kama MANGE? na sisi tumeshtuka tunataka tuonje Raha babue, mtu unashindwa kwenda hata MIKUMI mbugani! kisa mzigo wa familia umekuelemea hadi unatembea upande na mume unae lakini kazi ni USHARO UHARO!

HITIMISHO
Kwa sasa tunawatazama tuu mnavyogombania Media mkijitetea tuu huku HOJA ya msingi hamuigusi kabisa! bora Shem E hapo kideoni kagusia kidunchu kwamba wife ndo anaprovide na kwamba alihamia kwa wife..

Sasa hapo anajua mlipa pango? na magari je anajua nani kanunua? maana kuna wengine mnapenda kuendesha tuuu lakini hampendi kujua yametoka wapi!.

Yule mwingine nae anajitetea 'oh nilikubali kuwa BUSHOKE kwa sababu nakupena sana!' IVI UNAFIKIRI WATU NI WAJINGA KIASI HICHO? WEWE SEMA KWAMBA ULIKUBALI KUWA BUSHOKE KWA SABABU YA PESA PESA PESA PESAAAAAAAA . kina Marioo Mgombaniege Media salama SISI HATUNA HABAREEEEEEEE.......

NOTE
Sifurahii Ndoa ya mtu yeyote kuparanganyika! napitisha HOJA tuu ujumbe ufike... Maisha yakiwa ni magumu sana Ndani ya Ndoa hata furaha ya Ndoa hutaiona.

Pia tukibaki kutegemea mtu mmoja tuu nayo inachosha sana.. ndo maana tunafika huku kwa kutafuta press kwa ajili ya Ndoa yako.... so tuchukue tahadhari hiyo... Poleni mliopo kwenye tafrani kwa sasa. tujifunze pale tulipojikwaa na si tulipoangukia... AMEEEEN