Katibu wa mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Martine Simangwa kushoto akikabidhi msaada wa bati 100 kwa uongozi wa kijiji cha Usengerendeti kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya wauguzi wa Zanahati ya kijiji . |
Wananchi wakishiriki kushusha bati hizo |
Katibu wa mbunge Mgimwa Bw Martine Simangwa akieleza kazi mbali mbali zilizofanywa na mbunge Godfrey Mgimwa toka alipochaguliwa |
Katibu wa mbunge Mgimwa Bw Martine Simangwa kushoto akikabidhi bati 80 kwa uongozi wa serikali ya kijiji cha Mahanzi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika kijiji hicho kipya |
.............................................................................................
Na Francis Godwin Blog.
Na Francis Godwin Blog.
MBUNGE wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa ametoa msaada wa bati 180 zenye tahamani ya zaidi ya Tsh milioni 1 kwa kata ya Wasa kwa kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake katika kata hiyo.
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya mbunge Mgimwa katibu wake Martine Simangwa alisema kuwa bati hizo ni sehemu ya jitihada za mbunge huyo kuunga mkono harakati za wananchi katika kuibua miradi ya kimaendeleo katika maeneo yao.
Hata hivyo alisema kuwa bati hizo 100 ni kwa ajili ya kijiji cha Usengerendeti ambao wapo katika ujenzi wa nyumba ya waganga katika Zahanati ya kijiji na bati 80 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule katika kijiji kipya cha Mahanzi .
Alisema kuwa moja kati ya mambo ambayo mbunge Mgimwa ameyawekea kipaumbele zaidi ni pamoja na elimu pamoja na afya na kuwa jitihada za kuhakikisha mambo hayo yanashughulikiwa zinafanyika .
Pia alisema katika kuhakikisha maendeleo ya jimbo hilo la Kalenga yanaendelea kusonga mbele zaidi ni vema wananchi wa jimbo hilo kuelekeza nguvu zao katika maendeleo na kuachana na baadhi ya watu wanaopita katika jimbo hilo kwa ajili ya kuutaka ubunge mwaka 2015.
Kwani kufanya hivyo ni kuendelea kurudisha nyuma maendeleo ya jimbo hilo na kuwataka wanaofanya hivyo kwa sasa kusubiri muda ukifika ndipo wananze kujipitisha na kuwa kimsingi katika nafasi ya ubunge hakuna mbunge kivuli hivyo kitendo cha watu hao wanaojipitisha kufanya hivyo kwa sasa ni kuvuruga kasi ya maendeleo ya jimbo hilo.
Akizungumzia kuhusu suala la afya katika jimbo hilo alisema kuwa hali ya huduma ya afya bado si mbaya sana japo kuna changamoto mbali mbali ambazo zinapaswa kushughulikiwa ikiwemo ya dawa pamoja ,ukosefu wa nyumba za watumishi wa afya na baadhi ya maeneo zahanati na vituo hivyo vya afya kukosa umeme.
Awali wananchi wa kata hiyo ya Wasa walimpongeza mbunge huyo kwa kuonyesha uaminifu kwao na hata kuanza kutimiza ahadi zake kwa wakati mfupi zaidi ukilinganisha na wabunge wengine waliopata kuongoza jimbo hilo ambao hadi wameondoka madarakani baadhi ya ahadi hawajatekeleza kwa wananchi.
Alisema Yohana Sanga kuwa jimbo la Kalenga kwa muda mrefu limekuwa ni jimbo linaloongoza kwa kubadili wabunge kwa kila kipindi kimoja na ndi sababu ya jimbo hilo kuendelea kuwa nyuma katika maendeleo ukilinganisha na majimbo ambayo wabunge wake wameongoza kwa zaidi ya kipindi kimoja na kuwa kwa sasa wao hawana haja ya kubadili mbunge mwingine zaidi ya Mgimwa .