Mke wa ndoa wa marehemu Tyson, Yvonne Sheryl ‘Monalisa’ akiwa katika picha ya pamoja na mwanaye Sonia.
ZIKIWA zimekatika siku 40 tangu kifo cha muongozaji maarufu Bongo, George Otieno ‘Tyson’, mke wa ndoa wa marehemu, Yvonne Sheryl ‘Monalisa’, mama yake mzazi , Suzan Lewis ‘Natasha’ pamoja na mwanaye Sonia wamefanyiwa sherehe.
Kwa mujibu wa Monalisa, sherehe hiyo ni ya kimila kwa upande wa kabila lao la Kizaramo ambapo wenyewe huita shughuli ya kuoshwa.Shughuli hiyo iliyokusanya mastaa kibao ikiongozwa na Team Monalisa na Team Natasha ilifanyika wikiendi iliyopita nyumbani kwa Monalisa, Yombo – Buza jijini Dar es Salaam.soma zaidi hapa>>>>