MUIGIZAJI mwenye jina katika filamu za Bongo, Kajala Masanja juzi kati alipatwa na mchecheto ghafla wakati wa shughuli iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere maarufu kama Steve Nyerere huko Masaki, jijini Dar es Salaam.Katika tukio hilo ambalo Steve Nyerere alikuwa ameandaa chakula cha usiku kwenye ukumbi wa Great Wall, MC wa shughuli, Chiki Mchoma alimtaka Kajala kusimama na kutoa neno kwa niaba ya wasanii wa kike wa Bongo Movie, lakini cha ajabu, mwanadada huyo alipatwa na aibu ya ghafla kiasi cha kushindwa kuzungumza.
“Ni ajabu kweli yaani, maana Kajala tunayemjua siyo wa kushindwa kusema kitu sehemu kama hii, halafu sasa alishindwa hata kutoa sababu kwa nini hakuongea,” alisema msanii mmoja aliyekataa jina lake kuandikwa