Stori: Musa Mateja
Mchecheto! Staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, hivi karibuni alijikuta akiendelea kuwehukia penzi la mwanamuziki Mkanada anayefanya shughuli zake nchini Marekani, Justin Drew Bieber (20), Amani lina cha kushika mkononi.
Ishu hiyo ilitokea Julai 14, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa BoT uliopo maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam ambapo wasanii wa Marekani waliotinga Bongo kwa mwiliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ walikuwa wakitoa semina kwa wasanii wa Bongo.
Lulu ambaye kwa miaka mingi amekuwa akiweka wazi mapenzi yake kwa Bieber alifika ndani ya ukumbi huo na kumwambia staa mwenzake wa sinema, Zuweza Mohamed ‘Shilole’ kwamba lengo la kufika kwake ni kuwaomba wasanii hao namba za simu za Bieber.
ILIKUWAJE?
Semina hiyo ilikuwa na lengo la kutoa mbinu za namna ya kukuza na kupanua soko la muziki na sanaa zote Tanzania.
Semina ilianza saa 3:00 asubuhi na wasanii wa Bongo waliitikia wito kwa kufika mapema, lakini Lulu alizama ukumbini hapo saa 8:12 mchana.
Justin Bieber
AINGIA KWA MBWEMBWE
Lulu alishuhudiwa akiwasili ndani ya ukumbi huo kwa mbwembwe nyingi huku akimwambia Shilole kwamba ametia timu kwa lengo la kuchukua namba za simu za mpenzi wake wa moyoni, Bieber kwa vile alijua miongoni mwa Wamarekani hao lazima mmoja atakuwa na mawasiliano ya msanii huyo.
HATUA KWA HATUA NA AMANI
Mwanahabari wetu, baada ya kuyanasa mazungumzo ya Lulu kwa Shilole, alianza kumfuatilia staa huyo hatua kwa hatua kama kweli atamvaa mmoja wa wasanii hao na kumuomba namba za simu za Bieber!
Lulu alikwenda kukaa kwenye kiti mbele kidogo huku wasanii wengine wa Bongo wakiwa kwa nyuma yake na akaanza kufuatilia semina hiyo ilivyokuwa ikiendeshwa kwa usahihi.
Muigizaji na Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha E! cha nchini Marekani, Terrence J akiongea mbele ya wasanii wa Bongo leo.
JINA LA BIEBER LATAJWA, LULU ASHTUKA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mtoa semina mmoja alilitaja jina la Bieber katika mfano wa maelezo ya kuzingatia, ndipo Lulu akashtuka na kujishika sehemu ya kushoto kifuani kisha akamwelekea meneja wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ’Diamond’, Babu Tale ambaye alikuwa karibu yake na kumwambia maneno haya: “Naona sasa hawa Wamarekani wanaanza kugusa ninapopataka mimi.”
BAADA YA SEMINA
Baada ya semina kumalizika, baadhi ya wasanii wa Bongo walipiga picha za pozi na Wamarekani hao huku Lulu akienda chemba kuzungumza na Diamond, jambo lililotafsirika kuwa huenda alitaka msanii huyo amfanyie wepesi wa kukutana na Wamarekani hao kwa vile yeye alikuwa huko hivi karibuni akiwania Tuzo za BET.
Terrence J na Shaka Zulu (kulia).
LULU AONDOKA KIMYAKIMYA
Mpaka mwisho, Lulu aliondoka kimyakimya tofauti na alivyowasili huku paparazi wetu akiendelea kumfuatilia.
AMANI LAMVUTIA WAYA
Baadaye mwandishi wetu alimpigia simu ya mkononi staa huyo na kumuulizia kama alikipata alichokuwa amekikamia ndani ya ukumbi huo.Paparazi: “Lulu nilikusikia pale ukumbini ukimwambia Shilole kuwa lengo lako kubwa la kwenda ni kuipata namba ya simu ya Justin Bieber, vipi uliipata?”
Lulu: “Of course ni kweli nimekuwa nikimpenda Bieber tangu alipoibuka na Wabongo wanajua hilo, maana nimekuwa nikimsifia na kumzungumzia, ila pale ukumbini nilipongia Shilole ndiye alianza kwa kuniambia nimekwenda kuchukua namba ya Bieber.
Prodyuza David Banner akizungumza jambo na wasanii kwenye semina iliyofanyika leo.
“Hata mimi nilimkubalia kuwa ninavizia watakapomaliza kutoa semina niipate namba ya Bieber lakini sikumaanisha sana jamani!”
Paparazi: “Je, ulipokwenda kuongea na Diamond nini ilikuwa hoja yako kwake, akuunganishe nao?”
Lulu: “Mambo mengine bwana. Kuna wakati Shaka Zulu (mmoja wa wagane hao) naye alimzungumzia Justin Bieber na baada ya kutaja jina tu nilishtuka sana, nilitaka nione akina Diamond watasemaje?”
KUMBUKUMBU ZA LULU
Mwaka 2011 baadhi ya magazeti pendwa ya Bongo sanjari na mitandao ya kijamii yaliripoti jinsi Lulu alivyopagawa na mwanamuziki huyo kiasi cha kushindwa kuvumilia na kujianika kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Lulu alikwenda mbele zaidi kwa kudai kuwa, kwa jinsi anavyompenda staa huyo alikuwa tayari kumpa chochote kile (hakufafanua). Alikuwa ‘akitwiti’ kwa Kiswahili wakati mwingine akitumia ‘yai’ (Kingereza).
Katika maelezo yake Lulu alikaririwa akisema kuwa endapo staa huyo atatua Bongo, atatembea utupu kutoka nyumbani hadi sehemu ambayo Bieber atakuwa anapafomu.
Bieber mwenyewe anadaiwa kuwa na mashabiki zaidi ya 47,180,630 wanaomfuatilia kwenye Twitter hivyo huenda ilikuwa vigumu kumsoma Lulu.
KAMA VILE HAITOSHI
Hivi karibuni ambapo hata mwezi mmoja haujapita wakati Diamond akiwa nchini Marekani kwenye Tuzo za BET, Lulu alimtupia kwenye Instagram maneno haya: “Hongera kwa levo uliyofikia. Huko ulinionea Justin Bieber wangu?”
NADRA SANA, KWA LULU VIPI?
Ni nadra katika jamii ya Kiafrika mwanamke kuanika hisia za mapenzi yake kwa mwanaume asiyekuwa na habari naye huku jamii ikijua au kutambua hilo lakini Lulu amethubutu. Je, inakuwaje hapo?.
CREDIT:GPL