Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

HATIMAYE OKWI LIVE AT YANGA LEO MAZOEZINI!!

$
0
0

Hatimaye Emanuel Okwi leo amefanikiwa kuweka  rekodi yake ya pili ya kuzichezea timu mbili kubwa hapa nchini za Simba na Yanga.

Pia amenza  polepole kumziba mdomo mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage ambaye amekuwa akidai kuwa mchezaji huyo hatoitumikia Yanga.

Katika mazoezi ya Yanga leo kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar, Okwi alikuwa kivutioo kikubwa na watu wengi walijitokeza kumshuhudia.

Rage amekuwa akisisitiza Okwi hatocheza Yanga, huenda kesho kauli yake hiyo ikafutika kabisa atakapoichezea Yanga katika mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba.

Baada ya mechi hiyo, kitakachosubiriwa ni Okwi kucheza mechi ya mashindano, suala ambalo Rage atakuwa amepoteza cha kusema.

Rage ameendelea kusisitiza kwamba Okwi hatakiwi kucheza Simba, lakini Yanga wanaendelea na mambo yao kama kawaida



Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>