Jana ilikuwa ni mara yangu ya 4 toka nirudi Tanzania toka nje Miaka 2 iliyopita kwenda Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi baina ya timu hizo. Mimi ni mshabiki wa Yanga ninaijua timu hii kwa muda mrefu sana toka enzi za Mangara Tabu akiwa MWenyekiti wa timu hiyo. Enzi za Watoto wa Yanga, mpaka kocha Mrumania Victor na Tambwe Leya, mpaka Yanga inameguka vipande na kuwa Pan African, baadaye nikaenda nje na kuishi huko takriban miaka 30 lakini niliporudi miaka 2 iliyopita bado nimeendelea kuishabikia timu hiyo kongwe sana bongo. Baada ya mchezo wa jana nime-conclude kwamba Yanga sasa haina uwezo tena wa kuifunga Simba ni kwa sababu mbili kubwa nazo ni Uongozi mbovu na Saikolojia. Uongozi mbovu un ajonyesha wazi kwenye habari za kila siku za timu hii ya Yanga, kwani Mwenyekiti wa timu hiyo wa sasa analalamikiwa sana na Viongozi wengi wa sasa na wa zamani kwa pembeni kwamba anaiendesha timu hiyo bila kuwashirikisha na pia kujali sana masilahi yake zaidi ya kibiashara, pamoja na kwamba sijaikubali sana hoja hiyo lakini hoja mpya ndani ya package hiyo kwamba amesajili wachezaji wengi wa Simba kwa gharama kubwa sana na bila sababu ya msingi ni hoja nzito sana siwezi kuipinga. Simba wanawezaje kuwafunga Yanga hata na pamoja baada ya timu hiyo kuwachukua wachezaji maarufu waliokuwa Simba? Maana yake ni kwamba Simba walikuwa sawa kuwakataa wachezaji hao ambao Yanga imewakumbatia na kuwanunua kwa hela nyingi sana as opposed na uwezo wao kimpira. Ngassa, Okwi na Kaseja kama makaratasi yanasema kweli wanatakiwa kuwa hawana mshindani hapa Bongo, sasa iweje uwe nao na ushindwe kushinda? Hii ni hoja kubwa sana na ya msingi ya Viongozi wengi wa sasa na wa zamani wa timu hiyo. Halafu inakuja hoja ya Saikolojia, hili ni tatizo la muda mrefu sana kwa Yanga dhidi ya Simba, ni kwa muda mrefu sana sasa Simba imekuwa iikifunga Yanga tena kwa magoli mengi sana, ninakumbuka nikiwa mdogo Simba iikifunga Yanga magoli 6 kwa bila na ninakumbuka majuzi Simba ikiifunga tena Yanga magoli 5 kwa bila, kwenye mechi ya mwisho kabl;a ya mechi ya jana Yanga ilikuwa inaongoza kwa magoli 3 kwa bila mpaka nusu ya mchezo, lakini yote matatu yakarudi kipindi cha pili na jana ikawa ni aibu tena kwa Yanga, hawakuwa na uwezo wa kuwazuia Simba wala kushindana nao kiwanjani hasa kati kati ya uwanja. Yanga walionekana kucheza kwa wasi wasi sana dakika zote 90 za mchezo wa jana huku Simba wakicheza kwa uhakika na kujiamini sana hasa mchezaji wao aliyekuwa akishambulia upande wa kulia namba 7 alikuwa na uwezo wa kuifungua ngome yote ya Yanga kila alipoamua kufanya hivyo na kuwatesa sana wakati wa mchezo wa jana. Jana usiku nilikuwa Club moja ya starehe hapa mjini nikawakuta Viongozi karibu wote wa Simba hata wale tunaoambiwa kwamba hawaelewani wakiwa pamoja na washabiki wao, wakifurahia ushindi. Yanga inahitaji kufanya maamuzi magumu sana sasa hivi kama ya bunge juzi ili iweze kwenda kwenye mstari unaotakiwa, Viongozi wa juu wa Yanga wa sasa jipimeni wenyewe kama kweli mnafaaa kuiongoza timu hiyo kuelekea kunakotakiwa na hasa kuifunga Simba. Moja ya shauku ya wapenzi wa Yanga siku zote ni kuweza kuifunga Simba kwanza, ama sivyo ni kazi ya bure kwa viongozi wa timu hiyo na sasa ni muda mrefu sana Yanga mmeshindwa kuifunga Simba kwa ushindi wa kishindo kama ambavyo Simba imekuwa ikifanya na kwa muda mrefu sana. Yanga inatakiwa kuwa imara na daima mbele ni muhimu sana Viongozi wa sasa wa juu wa timu hiyo mkajipima wenyewe kama mnafaaa!! - Le Mutuz | |