MAMA wa aliyekuwa msanii wa muziki na filamu, Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’, Zainabu Mkiety, bado yuko kwenye maumivu ya kudhulumiwa haki za mwanaye jambo linaloongeza simanzi moyoni mwake.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, mama huyo alidai kushangaa kuona wahusika waliokuwa wakifanya kazi na Sharo Milionea wanakaa kimya juu ya malipo ya kazi hizo ambazo marehemu aliacha akidai.
Alisema, alichoambulia ni zile pesa za gari alilokuwa akitumia marehemu pamoja na vitu vya ndani lakini kila akifuatilia malipo ya kazi, hakuna anayemjali huku akidai kuwa huenda ni kwa sababu ya kukaa kijijini pamoja na uzee wake.
“Nawaomba wasinidhulumu jamani, nahangaika na uzee huu, mwanangu alikuwa ndiye nguzo maishani mwangu, mfano niliona hadi kalenda lakini sikuona chochote juu ya kalenda hizo, nawaomba sana,” alisema mama huyo kwa sauti iliyojaa maumivu.