Mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji leo amejikuta katika wakati mgumu kutokana na foleni kali ya magari.
Hata hivyo akili yake ilichemka haraka na kuamua kusahau kuwa alitajwa kwenye orodha ya Forbes 2013 ya watu matajiri zaidi Afrika, kukodi piki piki aka boda boda.
“The traffic in Dar is crazy,I was so fed up sitting in the car, I had to rent a(Boda Boda) 2 make it 4 a meeting, I guess I need a chopper,” alitweet.
Huenda wazo la kununua chopper akalifikiria kwa nafasi kubwa zaidi ili kuepukana na foleni kali wakati mwingine na hivyo kushindwa kuhudhuria mikutano ya maana.