Serikali imesema haitavumilia mtu au kundi la watu wa aina yoyote ambao watabainika kuendeleza vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na kutaka jamii kutumia madawati ya jinsia katika vituo vya polisi kuripoti matukio yote ya aina hiyo ili yadhibitiwe kabla ya kuleta madhara makubwa ikiwemo watu kupoteza maisha.
Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya ndani Mh Dk Emanueli Nchimbi wakati wa uzinduzi wa dawati la jinsia pamoja na mpango kazi wa miaka mitatu unaaonyesha majukumu ya jeshi la polisi katika kuimaraisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Naye mkuu wa jeshi la polosi nchini IGP Saidi Mwema amesema tangu kuanza kufanyiwa majaribio mpango huo umeonyesha mafanikio makubwa na hivyo ameitaka jamii kujitokeza na kutumia dawati hilo.
Akizungumza katika hadhara hiyo mratibu mkazi wa umoja wa mataifa Bw Aliberic Kacou amewataka viongozi kuhakikisha kuwa wanatumia nafasi zao pamoja na sheria zilizopo kuhakisha kuwa wanawadhibiti wale wote ambao kila mara wamekuwa wakifanya vitendo vya kikatili kwa makusudi.
-ITV