Jana mitandao ya kijamii ilijazwa taarifa kwamba jana jioni, John Mnyika (Mb) alimwandikia barua ya kujiuzulu Katibu Mkuu wa CHADEMA.
Ofisa Habari Mwandamizi wa CHADEMA, Tumaini Makene (0752 691569) alijibu kwa kukanusha kuhusu taarifa hizo na kuongeza kuwa kwa muda uliotajwa, Mhe. Mnyika alikuwa katika shughuli za chama akitimiza majukumu yake.
Akasema taarifa hizo ni mradi wa kutengeneza uongo unaofadhiliwa na watu kwa sababu ya, “kuwasumbua wanachama na Watanzania, lakini pia kutaka kuonesha kuwa kundi la wasaliti na wanafiki ndani ya chama linaungwa mkono na watu makini ndani ya chama ambao kama wangekuwa upande wao, wangesaidia kundi hilo kuondoa taswira hasi linalopata mbele ya jamii. Wanatafuta uhalali walioupoteza kwa kufanya harakati za kusaliti mapambano.
Mioyoni mwao wanaumia kweli kweli kuonekana wanaungwa mkono na watu wasio wanachama wa CHADEMA, ambao wengine wanalazimika kwenda kuwanunua pale feri Posta na Kariakoo ili waje kuwashangilia Mahakamani na kukimbia barabarani.