RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kutangaza majina ya mawaziri watano mapema wiki hii,taarifa za ndani kutoka Ikulu ya Rais Kikwete iliyonaswa na Habarimpya.com zinaeleza kwamba, zoezi hilo limepangwa kufanyika mapema wiki hii kabla ya Rais kuanza zoezi la kuteuwa wabuge wa bunge la Katiba.
"Rais anamajukumu mengi sana ya kitaifa kipindi hiki na moja ya majukumu yake ni kufanya uteuzi wa mawaziri watano watakaojaza nafasi zilizo achwa wazi kabla ya Bunge la Katiba kuanza"kilisema chanzo cha Habarimpya.com kutoka Ikulu ya Rais Kikwete Magogoni jijini Dar es Salaam.
Chanzo hicho pia kilifafanua kwamba baadhi ya majina yanayotajwa kuingia katika wizara hizo ni pamoja na Mbunge wa kuteuliwa Dk Asha-Rose Migiro (Wizara ya Fedha na Uchumi),James Lembeli (Wizara Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa).
Wengine ni Lazaro Nyalandu na Naibu wake kuwa Dk Mary Mwanjelwa (Wizara ya Maliasili na Utali),January Makamba (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) huku nafasi yake ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, ikichukuliwa na Vita Kawawa (Mbunge wa Namtumbo),Jenista Muhagama (Wizara ya Mifugo na Uvuvi).
Kuhusu nafasi za Manaibu Waziri katika Wizara hizo, Chanzo chetu kilidokeza kwamba kuna uwezekano wa manaibu waliokuwepo katika Wizara hizo kuendelea katika nafasi zao, ingawa orodha hiyo inaweza kubadilika wakati wowote.
"Mpaka hivi sasa hayo ndiyo najina ninayofahamu kwamba yako mezani kwa mzee,kutokana na jinsi ambavyo yanatajwa mara kwa mara,ingawa lolote linaweza kubadilika, kwani kazi ya kuteuwa mawaziri inahitaji umakini wa hali ya juu, hivyo usije ukashangaa kuona mabadiliko katika orodha hiyo"chanzo hicho kilifafanua.