1. Kwanza elewa neno WEB ni nini:
WEB ni kifupisho cha neno zima WORLD WIDE WEB - si umeona websites nyingine zinaanza na www, basi www ni kifupisho cha World Wide Web. Kwa lugha rahisi WEB ni namna maalum ya ku share taarifa kupitia internet kwa kuunganisha mawasiliano toka kompyuta tofauti tofauti ulimwenguni. Kama vile mie nipo nchini Colombia naandika maneno haya kwa laptop yangu wewe hapo ulipo unasoma hii post kwa- sababu ya hii teknolojia ya world wide web (web).
2.WEBSITE ni muunganisho wa maneno mawili WEB na SITE.
Wajua neno web nini , basi unganisha na neno SITE kama unavyojua neno SITE ni eneo maalum kwa ajili ya shughuli maalum, au sio ? Basi WEBSITE inamaanisha ni sehemu maalum ambapo habari au taarifa fulani zinapatikana. Mfano kama wataka kusoma status za rafiki zako wa FB basi wajua ni lazima uende FACEBOOK. Hivyo FACEBOOK ni SITE kwako maalum kwa kucheki mambo maalum kama hayo ya status ! Kwakuwa FB ni site iliyopo ndani ya muunganiko tuuitao WEB, hivyo FB tunaiita WEBSITE.
3. Kwa mujibu wa Wikipedia, neno blog ni kifupisho cha neno Web LOG, yaani rekodi au usajili wa taarifa za mara kwa mara ndani ya WEB. Ili kufupisha neno zima WEB BLOG wakaita kwa kifupi BLOG-yaani kutoka neno WEB, tumechukua herufi B, halafu tukaunganisha na neno LOG, hivyo kuwa na BLOG.
--Kuelewa utafauti kati ya BLOG na WEBSITE kunategemea sana kuelewa hayo maneno matatu hapo juu yaani WEB, WEBSITE na BLOG.
Zifuatazo ni tofauti kati ya blog na website:-
Uandishi : Kwenye blogs tuna kitu tunaita POSTS ambapo hayo ni maelezo yanayowekwa na mwandishi wa blog mara kwa mara. Hata hivyo websites kwa asili huwa hazibadilishwi taarifa mara kwa mara kama ilivyo blog.
Uhifadhi wa taarifa: Blogs zina mtindo maalum wa kuhifadhi posts toka ya kwanza mpaka ya mwisho kuiandika. Na mara nyingi waweza kuona hifadhi (ARCHIVE) ya posts hizo katika blogs nyingi, hata hivyo websites nyingi huwa hazina hifadhi ya taarifa zao za siku za nyuma ndani ya websites husika.
Teknolojia: Mtu yoyote yupo huru kuandaa website kwa mtindo anaotaka yeye, tofauti na blogs ambapo tayari teknolojia yake inategemeana na matakwa ya kampuni husika inayotoa huduma ya blogging. Mfano kuna wordpress inao mtindo wake maalum, na blogger nao wana mtindo wao maalum wa jinsi blogs zao zitakavyotokea au jinsi utakavyoziandaa.
Ushirikishwaji wa wasomaji: Mara nyingi kwenye blogs huwa tuna sehemu ya comments kwa kila post, wakati taarifa za websites nyingi hazina kipengele cha ku comment.
ANGALIZO: Asasi nyingi siku hizi zimekuwa zikiambatanisha teknolojia ya blog katika websites zao ili kuendelea kuwa karibu na wateja wao watarajiwa.
Swali kwako: Je, nimesahau utofauti mwingine kati ya blog na website ? Comment hapo chini kwa kutaja tofauti nyingine.
MAREJEO: Waweza pata habari zaidi kuhusu blogs na websites toka:-