The Dataz ni kwamba Mheshimiwa sana Waziri Mkuu Mstaafu siku ya Jumanne iliyopita aliitwa Rasmi na Kamati ya Maadili ya CCM Taifa Lummumba, kwenda kutoa ufafanuzi wa kwa nini amejitangaza mapema kwamba anagombea Urais kinyume na Kanuni za CCM.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, na ndiye Mwenyekiti wa Wenyeviti wote wa CCM Mikoa ya Tanzania, majuzi alitangaza kwamba Wenyeviti wote wa CCM wa Tanzania wanamuunga mkono Mh. Lowassa kugombea Urais 2015, jana aliitwa Kamati Kuu Zanzibar na kupewa mkwara mzito na leo ametoa statement ya kuyakana maneno yake mwenyewe ya majuzi kwamba anawakilisha Wenyeviti wote wa Mikoa nyuma ya Lowassa.