Wajumbe wa chama cha NCCR-Mageuzi waanza kuwasili kwa ajili ya uchaguzi mkuu ndani ya chama cha NCCR-Mageuzi, huku kukiwa na minong'ono ya chini kwa chini juu ya kuwa ni bora Mwenyekiti ashinde(wakiwa na maana ya Mh.Mbatia) na wengine wakivutana juu ya nani awe Katibu mkuu kati ya Katibu mkuu aliyepo Samwel Ruhuza na mpinzani wake katika nafasi hiyo Mosena Nyambabe.
Blogu ya Mwafrika ilipotaka kujua majiana ya wajumbe hao hawakuwa tayari kutaja majina yao. Jumamosi ya wiki hii ndio mzizi wa fitina utakatika kwa nafasi za juu za ungozi wa chama hicho.