Ripoti ya uchunguzi binafsi juu ya mgogoro CHADEMA
Mimi ni Raia wa Tanzania, sina uanachama wa chama chochote cha siasa na sina ushabiki na kiongozi yeyote wa kisiasa. Nitawasilisha uchunguzi wangu binafsi juu ya mgogoro unaoendelea hivi sasa ndani ya chadema
Nitaanza kwa kuzungumzia kile ambacho nimekuwa nikikiona hasa kwenye mitandao na hata stori za vijiweni.
- Tuhuma namba moja ni tuhuma dhidi ya Zitto kwamba amenunuliwa na CCM ili kukiharibu chama
- Tuhuma namba mbili ni tuhuma kwamba Zito anaonewa na viongozi wa juu, Slaa na Mbowe (hapa pia ukabila umeingizwa na udini pia)
Hizo mbili ndio tuhuma kubwa na ndizo zinazojadiliwa sana na ndicho chanzo cha mvutano baina ya pande mbili hizi.
Katika mgogoro huu uchunguzi wangu unaonyesha kuna pande 3 (tatu) ambazo ziko katika mgogoro
- Wanachama wa CHADEMA (wanakitetea chama)
- Zitto na watu wake (Wanamtetea zito na kuushutumu Uongozi wa juu)
- Uongozi wa juu wa chadema na watu wao (Wanamshutumu zito na kuutetea Uongozi)
Mgogoro ulipo
Mpaka sasa vita kuu iliyopo ni vita kati ya Mbowe + Slaa dhidi ya Zitto, Zito amesimama Upande ambao anapingana na Maamuzi ya Uongozi wa juu Tofauti na tuhuma anazopewa kwamba anakisaliti chama. Na pia sababu yake kubwa ni kwamba anaonewa na Uongozi huo kutokana na msimamo wake wa kuhoji juu ya matumizi mbalimbali ambayo yanafanywa na Uongozi wake. (Tuhuma ambazo sijapata majibu yake toka kwa watuhumiwa hao kuhusu matumizi ya fedha za chama nk)
Tuhuma anayopewa zitto ni kubwa pia lakini sijamsikia akizikanusha na kuzitamka wazi na kuweka Ukweli halisi uliopo, wahusika wote ni kina nani, na Lengo hasa lilikuwa ni lipi kwa kile anachodaiwa kukifanya.
HARAKATI ZA MTAANI
Nilibahatika kuhudhuria hii kesi ambayo inaendelea, na hata leo pia nilikuwepo eneo la mahakamani na nilianzia nje na nikaona kuna pande mbili ambazo zote zilikuwa na mashabiki wa kutosha lakini unapomtazama mtu jinsi muonekano wake ulivyo unaweza ukajua hadhi ya ofisi anayofanyia kazi ni ipi.
Ukweli ni kwamba wengi wa watu waliokuwa wanashangilia na kupiga kelele ni watu ambao kimwonekano sio wale ambao tunaweza sema wameacha shughuli zao na kwenda kuhakikisha haki inatendeka. HII NI WAZI KUWA KULIKUWA NA WATU WA KUTENGENEZWA (hii ni kutoka pande zote)
Nikisimama kuutazama mgogoro huu kati ya Mbowe na Slaa dhidi ya Zitto ninaona kabisa kuwa Mbowe na slaa wameegemea upande wa Chama, hivyo mgogoro unaonekana ni wa Chama na Zitto. Ukiangalia hadithi za Pande zote utagundua kuna mgogoro wa kimaslahi, kicheo na Kimajukumu hili halipingiki. Nikirudi kwenye Chama na wafuasi wa CHADEMA naona kabisa kuna watu wapo neutral kwa kutojua nani yuko sahihi
- Wengi hawaamini kama Zito ambae alikuwa mtoa hoja nzito maarufu bungeni anaweza akafanya kitendo hicho cha usaliti
- Wapo pia wengi wanaoamini Zitto ametumwa na wapinzani wa CHADEMA kwenda kuwavuruga kwa Hisani ya haohao wapinzani
- Wapo pia wanaoamini kuwa Mbowe na Slaa wanamfanyia Fitina Zitto kwa sababu ya Uongozi
HITIMISHO
Wana chadema nawashauri, jaribuni kuangalia tuhuma za pande zote kwani ukiziangalia kiundani bado kila tuhuma ni nzito na ikitatuliwa itakijenga chama. Kama Zitto ameweza kuzizungumza tuhuma ambazo hata Chacha wangwe alizisema ni wazi pia atajitokeza Mwingine mbeleni ambae atayasema hayo hata kama Zitto hatakuwepo ndani ya Chadema. Migogoro haitaisha iwapo mtakaa kimya kwa kusikiliza upande mmoja.
Kwa kuwa Mgogoro huu una Sura mbili tofauti basi ni wazi kuwa mnapaswa muweke sura zote zifanane ili muweze kutatua huu mgogoro ambao unakitafuna chama.
Nitaendelea...