Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

THE MAJANGAZ & BONGO:- NA HUYU NDIYE MZEE ANAYEDAI YANGA NI TIMU YAKE NA HATI HIZI HAPA ANAZO LIVE!!

$
0
0


ALIYEJITANGAZA kuwa mmiliki wa klabu ya Yanga, Juma Mwambelo, amesema yu tayari kukabidhi nyaraka zinazotafutwa na uongozi wa klabu hiyo kwa Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

 
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alitangaza kwenye mkutano wa Yanga kwamba Mwambelo anashikilia hati za umiliki wa klabu ya Yanga kimakosa na anatakiwa kuzikabidhisha haraka iwezekanavyo kabla ya kuchukuliwa hatua.
 
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwombelo alisema yupo tayari kumpa Rais Kikwete naye aukabidhi uongozi wa Yanga chini ya Yusuf Manji.“Kweli hati hizo ninazo kwa kuwa mimi ni mmiliki wa Klabu ya Yanga, ila Rais Kikwete pekee ndiye naweza kumkabidhi, hata mwanaye Ridhwani nimewahi kumueleza kuhusiana na hili,” alisema.“Mimi ndiye mmiliki wa Klabu ya Yanga, nina hati miliki halali ya klabu, hii hapa (anaonyesha), nina hati miliki ya jengo la Jangwani, pia ninayo ya jengo la Mafia, lakini hiyo waliiba na tayari nilisharipoti polisi.
 
“Kuhusu hati ya jengo la Jangwani ipo benki na yenyewe sijailipia kwa kuwa kuna deni, deni hilo ni zile fedha ziliyotumika kujenga Uwanja wa Kaunda. Hivyo, deni likilipwa benki itakubali kutoa hati kisha kuirudisha wizarani na kutolewa rasmi.“Nashangaa Yanga wanapodai wanatumia katiba mpya, hii siyo halali, katiba halali ya Yanga ni ile ya mwaka 1967 ambayo nakala yake hii hapa (anaonyesha),” alisema.Alipoulizwa juu ya uhalali wa wanachama wa sasa wa klabu hiyo, alisema: “Wanachama wengine wote ni feki, mpaka unatokea mgawanyiko mwaka 1975, wanachama halali wa Yanga walikuwa 400, kuanzia hapo hakuna wanachama halali tena, hata akaunti zinazotumika siyo za klabu.“Hapa nilipo nimekuja polisi (Magomeni) ili kutoa taarifa ya kujihami, nahofia kupigwa kutokana na walichokisema kwenye mkutano,” alisema. 
 
Katika mkutano mkuu wa Jumapili, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karume, PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, uongozi wa Yanga ulimtaja mzee Juma kuwa ndiye aliyeiiba hati ya jengo la klabu hiyo tangu Juni 24, 2009.“Mimi nilipigwa na watu mwaka 1987 nikapoteza fahamu kwa siku tano, tangu pale sijawahi kwenda klabuni wala uwanjani kuitazama Yanga, hata huyo Mrisho Ngassa simjui, namuona tu kwenye magazeti, kikubwa ninachotaka ni utaratibu ufuatwe ndani ya Klabu ya Yanga,” alisisitiza huku akitabasamu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>