Mh:Mwigulu Nchemba akihamaki Kuona Wajumbe wa Mkutano Wanafungua Mikoba yao na Kutoa Fedha za Kumkatia tiketi iliarejee Dsm Kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha.
Katibu Wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Akwilombe akihesabu fedha zilizokuwa zikichangishwa kwaajili ya Mh:Mwigulu Nchemba,Nyuma Mh:mwigulu haamini Macho yake.
Mapenzi tele ya WanaCCM kwa Mh:mwigulu Nchemba wakiendelea Kumwaga fedha kwa Kiongozi huyo iliaendee akawatumikie kwenye Wizara ya Fedha.
Mh:Mwigulu Nchemba akishukuru kwa Katibu Mkoa wa Mtwara baada Ya Kukabidhiwa tiketi arejee Dsm kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha.
Ni Mkono wa Kwaheri Kutoka Kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwa Wajumbe waliokuwepo kwenye Kikao cha Halmashauri ya Mkoa wa Mtwara CCM.
Wajumbe waliokuwepo kwenye Kikao
Ni tukio La Kihistoria kwa Kizazi hiki na yawezekana baada ya Mwl.Nyerere Kuchangishiwa fedha na Mali aende kudai Uhuru kwa Kuzunguka Nchi Nzima,Basi Mwigulu Nchemba alikutwa na jambo hilo hilo la Kutumwa na Wananchi akaitumikie Wizara ya Fedha.
Ni Jumapili ya 19.01.2014 Mh.Mwigulu Nchemba akiwa kwenye Majukumu yake ya Ujenzi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mtwara,Sikuhiyo alikuwa na Kikao cha ndani cha Halimashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mtwara kujadili mwenendo wa chama na na Uchaguzi mdogo wa Udiwani unaoendelea Nchini.
Mh>Mwigulu Nchemba anapokea wito wa Kurejea Jijini Dsm haraka iwezekanavyo,Wito huo ulikuwa moja kwa moja unahusisha Uteuzi wa Baraza la Mawaziri kwani Siku ile ndani na Nje ya Mitandao ya Kijamii kuligubikwa na Wimbi la Ikulu Kuitisha Vyombo vya Habari kwaajili ya Kutangaza Baraza la Mawaziri.
Wajumbe waliokuwa ndani ya Kikao walitaarifiwa na Katibu Mkoa wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara(Ndugu Akwilombe aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA kabla ya ZItto kupokea Kijiti) Kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Mh.Mwigulu Nchemba anawito wa kurejea jijini Dsm.Taarifa hizi zinaamsha hisia za Wajumbe na Kuanza kuimba Nyimbo za Chama kwa Furaha na Kibwagizo cha Tunaimani na Mwigulu Nchembaa..oyaaaaaaa oyaaaaaaa oyaaaaaaa.
Wakati hayo yakiendelea Ghafla Mmoja wa Wajumbe akajitokeza Mbele ya Ukumbi na Kusema Kwa namna Mh.Mwigulu Nchemba anavyofanya kazi zake kwa Umahili wa hali ya Juu na Kuifikisha CCM hapa kila mmoja akajivunia kuitwa MwanaCCM nalazimika Kuchangia Fedha kwaajili ya tiketi ya Ndege ili Mh>Mwigulu aweze kufika Dsm leo leo.
Ukumbi Mzima ukalipuka kwa kuanza kuimba na kuchangia fedha kwaajili ya tiketi ya Ndege Mh:Mwigulu Nchemba aende Dsm akapewe Majukumu Mapya,Imani kubwa kwa Wanamtwara ni Kwamba popote alipo Mh:Mwigulu Nchemba kazi inafanyika kwa Ukamilifu tena wao wanasisitiza Mwigulu ni mtu wa Watu.
Ni Zaidi ya Sh.Laki tano za Kitanzania za papo kwa papo zilipatikana na tiketi ikapatikana ilikuhakikisha Mwigulu Nchemba anaondoka Mtwara kwa Ndege na afike Dsm kukabidhiwa Majukumu mapya ya Kulijenga Taifa letu.
Ni nadra sana kuona Kiongozi unakubalika kiasi hiki kwa Wananchi na wakalazimika kuwiwa kukupa Madaraka ya Juu zaidi iliuendelee kuwapigania,Lakini Kwa Mwigulu NChemba hili ni Wazi kabisa kuwa Watanzania na WanaCCM wanakubali Mchango wa Mh;huyu kwenye kuitetea CCM na Tanzania Kwa Ujumla wake.
UJUMBE:Inawezekana kabisa Kwa Kila mmoja wetu kufikia hatua hii ya Mh:Mwigulu Nchemba kupewa heshima kubwa kama hii ya Kutumwa kuwatumikia wananchi,Kupiganiwa na Wananchi uendee ukawatee.Yaliyofanyika enzi za Nyerere akipigania Uhuru leo hii yanakuja Kutokea Kwa Mh:Mwigulu Nchemba na Kwako Pia INAWEZEKANA KUWA MZALENDO NA MWADILIFU TU.