↧
WAKUU WA MAJESHI TANGU TANZANIA ILIPOPATA UHURU.
↧
WIMBO MPYA WA DIAMOND PLATINUMS WAZIMWA NA WEMA SEPETU KUHUSU SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA
↧
↧
KAULI YA AFANDE SELE KWA PAUL MAKONDA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA

Afande ameandika
‘Katika hili sakata la MAPAPA na MAPUNDA ya Unga kama kweli braza Paul yupo serious na sio ‘Matango Pori’kama tulivyoona ktk masakata mengine,huenda hata wale WASAFI wakaonekana wachafu…kila la kheri Mr Paul….RiP Da Amina…wacha parry ianzeee…..’
↧
THE MAGAZETI YA BONGO LEO SATUDAY/JUMAMOSI 04/02/2017 LIVE
↧
WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WASIFIWA KWA UBABE KATIKA MAENEO YAO YA KAZI
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene amesema kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Simbachawene ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Chemba Juma Nkamia kuhusu Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuwa wababe katika maeneo yao ya kazi.
“Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanasimamia maeneo yao kwa mujibu wa sheria na wana haki ya kuwachukulia hatua watumishi ambao hawatekelezi majukumu waliyopewa,” alifafanua Simbachawene.
Aliendelea kwa kusema kuwa, hata kama kuna Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni wababe katika maeneo yao ya kazi hauwezi kusema kila Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyechukua hatua dhidi ya mtumishi ambaye hawajibiki katika kazi yake ni mbabe au muonevu.
Aidha, Simbachawene amesema kuwa ni wakati sasa wa watumishi wa Umma kutekeleza wajibu wao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Kwani hakuna kiongozi ambaye ataweza kumchulia hatua mtumishi ambaye anawajibika na kazi zake kama alivyopangiwa.
Vile vile amesema kuwa, wakuu hao wa Mikoa na Wilaya wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika maeneo wanayoyasimamia, kutokana na watumishi wengi wa Serikali walikuwa wamejisahau kutekeleza wajibu wao na kufanya kazi kimazoea.
↧
↧
MAZITO MENGINE KUHUSU HAMRORAPPA,MENGI YAFICHUKA KUHUSU MAISHA YAKE

MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu wa kijiwe hiki Mpaka Home, kama ilivyo ada ni kuwatembelea mastaa wa fani mbalimbali hapa Bongo na kuweza kuyajua maisha yao halisi ya kila siku nje ya kazi zao, wiki hii tulikuwa maeneo ya Mikocheni B nyumbani anapoishi kijana Athuman Omary wengi wakimfahamu kwa jina la Harmorapa.

…akiandaa kitoweo na mpenzi wake
Msanii huyo awali alikuwa akiishi Vingunguti jijini Dar, lakini sasa maisha yamebadilika kidogo, ameweza kupata nyumba kubwa maeneo ya Mikocheni na hiyo yote ni kutokana na sapoti kubwa anayopewa na bosi wake aitwaye Irene Sebuka.Nyumbani hapo msanii huyo ambaye anafanana na mkali wa kutoka Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Harmonize,anaishi na mwanamke wake aitwaye Nancy au anavyopenda kumuita mwenyewe Wolper, wake.Ungana nami hapa chini ili uweze kujua anaishije nyumbani hapo.

Kwanza ilikuwaje mpaka akajiita Harmorapa?
“Unajua hata wewe mwenyewe ukiniona hakuna ubishi kwamba mimi sifanani na Harmonize sasa kwa vile naimba na nikaona wazi niko kama yeye ndio maana nilijipa jina hilo na nilikuwa natamani sana nimuone na yeye anione mimi pacha wake.

…akimnywesha soda
Nini kimebadilika kwenye muziki wake kati ya zamani na sasa?
“Maisha yapo tofauti sana kwa kweli sasa hivi, nyuma nilikuwa sina muelekeo na chochote lakini sasa hivi maisha yangu nayaona kabisa katika mwanga ulio bora kabisa na ninajivunia kuwa mimi siku zote na hata hivyo zamani nilikuwa naishi Vingunguti lakini sasa Mikocheni tofauti kubwa sana.

…wakifanya usafi chumbani.
Zamani alikuwa akifanya kzi gani zaidi ya muziki?
“Zamani nilikuwa nauza mabegi ya kike na ya kusafirisha hadi Mwenge kuuza, ndio ilikuwa ni biashara kubwa japokuwa nilikuwa na ndoto ya kuwa mwanamuziki lakini nilijua wazi ipo siku Mungu angesikia kilio change.
Wolper wake ameshamuoa? Anaishi naye?
“Huyu bado sijamuoa lakini ninaishi naye na si unajua Kibongobongo ukikaa na msichana ndio mke kabisa, basi tuombe Mungu mambo yatakuwa mazuri kabisa huko mbeleni.

Alimpataje mpenzi wake? Haogopi kuibiwa?
“Huyu alikuwa ni mteja wangu wa mapochi Mwenge, kwa hiyo nikamzoea tukazoeana mpaka ikatokea hivyo na tuna mwaka sasa na kuhusu kuibiwa hiyo ni akili yake kwa maana akiamua kufanya hivyo atakuwa ni yeye mwenyewe lakini mimi sina wasiwasi naye.

wakiwa kitandani.
Ni kitu gani anapenda kufanya akiwa nyumbani?
“Mara nyingi mimi nikiwa na mapumziko nyumbani napenda sana kufanya usafi na muda mwingi kufua nguo na hata kumfulia mpenzi wangu. Baada ya hapo ni kuangalia TV hususan wanamuziki mbalimbali wa nje.

Harmorapa akiwa na meneja wake.
Mafanikio aliyonayo yanatokana na muziki au kitu kingine?
“Japokuwa ninaimba muziki lakini nashukuru Mungu, bosi wangu Irene Sabuka, ameniajiri katika kampuni yake ya kuuza vifaa vya magari Kariakoo na ndipo huko maisha yangu yalipobadilika hivyo sitegemei muziki tu.

…akimwagilia maua.
Ni chakula gani anapenda? Vipi kuhusu mavazi?
“Sifa moja kubwa ya mpenzi wangu ni kujua kunipikia mchele wa Pisholi na nyama. Kuhusu mavazi, mimi napenda sana kupendeza yaani nikitinga tisheti na jinzi naona niko freshi na nguo ambazo wanapenda kuvaa mabraza meni.

Maisha gani alipitia huko nyuma?
“Nyuma sitaki kukumbuka kabisa, nilipitia maisha mabaya sana na ya dhiki mno. Sitaki kurudi huko nyuma nilikotoka na ninaomba Mungu anisaidie kwa hilo.”
↧
HUU NDIO MKWANJA ANAOINGIZA STAA WEMA SEPETU KWA MWEZI

Wema Sepetu amezindua rasmi app yake, WS, kwenye jukwaa la app la simu za Android, Google Playstore.
App yake inapatikana bure kabisa. Ukishainstall, itakuomba usign-up kwa kutumia akaunti yako ya Gmail. Basically, app yake ipo kwaajili ya yeye kuwasiliana na mashabiki wake, kila siku. Anachofanya, ni kuandika mambo mbalimbali kuhusu yeye binafsi kama fashion, muziki, filamu, na hata mahusiano.Kwa mfano ametumia app hiyo kuwafahamisha mashabiki wake kuhusu kuwepo kwenye orodha ya mastaa walioitwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanaohusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya.Kwenye app hiyo hadi sasa pia, ameweka pia video/audio akizungumzia tattoo zake, timu za mitandaoni, filamu tatu anazozipenda, gharama za nywele zake, nyimbo 3 za Diamond (ex wake) anazozipenda na vingine.
Haya ni mambo ambayo mashabiki wake wanavutia sana kumsikia akiyasema.
Awali, aliweza kuwapa taarifa hizi kupitia akaunti yake ya Instagram au kupitia interview anazofanyiwa, lakini sasa wayatapata kupitia app yake. Tofauti sasa ni kwamba, taarifa hizi mashabiki hawatazipata bure, watalazimika kuzilipitia.
Gharama yake hata hivyo, ni pesa ya madafu kabisa. Mfumo wa malipo ni wa subscription, kama ambavyo huduma za kustream muziki kama Tidal au Spotify hufanya. Shabiki ana option kadhaa rahisi tu, kulipia kwa mwezi, ambayo gharama ni shilingi 1,000 tu (mimi nimejiunga na hiyo), miezi mitatu 2,500 na pia kuna option ya miezi sita hadi mwaka mzima ambayo inaenda ikipungua kwa kadri unavyonunua kifurushi cha muda mrefu.
Wale ambao wamesubscribe, watakuwa na access ya kupata habari na matukio exclusive ya Wema, ambayo huwezi kuyapata kokote, hata kwenye akaunti za mitandao ya kijamii. Kila kitu ambacho atapenda kukisema sasa, atakuwa akikiweka kwenye app yake, na ni subscribers wake pekee watakuwa na access nazo. Kuna option kibao za kulipia kuanzia M-Pesa, Tigo Pesa hadi visa, na hivyo kuwa app inayoweza kuingiza fedha dunia nzima. Kwa kutengeneza hamu zaidi ya watu kudownload app yake, huenda Wema akaanza kuadimika sasa kwenye interview za redio, TV au blog. Ubuyu wote atauweka kwenye app yake.
Sasa hebu tupige hesabu ya kiasi anachoweza kuingiza ndani ya mwezi mmoja. Well, app bado ni mpya na watu ndio wanazidi kuifahamu sasa, na idadi ya watu wanaoidownload muda huu ni kubwa. Rate yake ya ukuaji ni kubwa sana hivyo kuna uwezekano kuwa ndani ya mwezi mmoja, akapata zaidi ya watu 5,000. Kama watu hawa wote watachagua kujiunga kwa kifurushi cha mwezi cha shilingi 1,000, atakuwa ameingiza, shilingi milioni 5.
Pindi app ikichanganya ikawa na watumiaji laki moja, ataingiza shilingi milioni 100 kwa mwezi. Na pale ambapo app itafikisha subscribers milioni moja, kwa kila mwezi atakuwa na uwezo wa kuingiza 1,000,000,000 (shilingi bilioni 1). Ni namba kubwa kuifikia, lakini kwa umaarufu wake, ndani ya miaka kadhaa, ataweza kufikisha.
Bila kusahau kuwa, watu milioni 1 ni nusu ya followers wake zaidi ya milioni 2.5 kwenye Instagram, kwahiyo inawezekana. Na hapo yapasa kuzingatiwa kuwa takwimu za TCRA kuwa hadi mwishoni mwa mwaka 2015, watumiaji wa internet nchini walikuwa ni zaidi ya milioni 17 na wengi wakiipata kupitia smartphone. Kuna uwezekano kwa sasa wamefikia zaidi ya milioni 20, hivyo unaongelea idadi kubwa ya subscribers ambao Wema ataweza kuwavutia kwenye app yake.
Pesa ya subscription, sio pekee atakayokuwa akiingiza. Pindi app yake itakapopata umaarufu, ataweza kuvutia matangazo kutoka google wenyewe ama kutoka kwenye makampuni moja kwa moja na kumlipa fedha nyingi kutangaza bidhaa zao.
Kwa sababu Wema ni mtu maarufu na fan base yake ni kubwa, ana uwezo wa kuwa na content nyingi za kuvutia kwa miaka mingi ambazo mashabiki wake watafurahia kuziona kwenye app. Ana mengi anayoweza kufanya, ikiwemo kuweza kutoa hata series fupi fupi ambazo zitapatikana exclusively kwenye app yake, simulizi za uhusiano wake na mastaa kama Diamond, marehemu Kanumba, Idris Sultan, TID, Mr Blue, Chaz Baba na maisha yake mengine.
Haya yote, ni mambo ambayo mashabiki wake huwa na hamu kubwa ya kuyajua na wako tayari kulipa kiasi chochote ili kupata. Na kwa kutoa app, Wema Sepetu amegundua njia rahisi zaidi ya kufikisha content yake na yeye mwenyewe kutengeneza fedha za kutosha
↧
RC MAKONDA ATOA AMRI KUWAKAMATA WALE WOTE AMBAO HAWAKURIPOTI KITUO CHA POLISI KATI KUFUATIA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

NA Anthony John Glob jamii
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amelitaka jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kuwakamata wale wote ambao hawajafika kuripoti kituoni hapo kwa tuhuma za uuzaji na uvutaji wa madawa ya kulevya.Akizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo Mhe. Makonda amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao walitakiwa kuripoti katika kituo cha kati cha polisi na hawajafika ambao ni Rashidi makwilo (chidi benzi, Sameer Kheri (mr blue) pamoja na wamiliki wa klabu za kuuza pombe.“Kuna watu waliowaita lakini mpaka sasa hawajafika. Naliagiza jeshi la polisi kuwakamata na kuwaweka ndani wote ambao hawajafika mpaka juma tatu”, amesema.
Sambamba na hayo Mkuu huyo wa mkoa ameongeza majina matatu ya askari polisi na wasanii ambao wanatakiwa wakamatwe kwa tuhuma za kushirikiana na wauza madawa ya kulevya pamoja na Vanesa Mdee na mwana dada Tunda kufika katika kituo cha kati.Makonda ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kutokomeza hali ya uuzaji na uvutaji wa madawa ya kulevya hapa nchini.
Mwanadada maarufu hapa jijini Dar,Wema Sepetu akiongozwa na Mmoja wa Makachero wa kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam wakiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya
Mmoja wa wasanii anaetambulika kwa jina la kisanii Babuu wa Kitaa akiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya
Baadhi ya watu waliofika kituo cha polisi kati kujionea watuhumiwa mbalimbali wa Madawa ya kulevya walioitikia wito wa kuitwa kutoka kwa RC Paul Makonda
Mmoja wa wasanii mahiri wa bongofleva,maarufu kwa jina la kisani T.I.D akiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya
↧
SERENGETI BOYS YAFUZU FAINALI ZA AFRICA

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys, imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), imethibitisha hilo pasi shaka kwamba Tanzania ndiyo yenye nafasi ya kucheza fainali hizo zitakazofanyika kuanzia Aprili 2, mwaka huu huko Gabon baada ya Madagascar kuenguliwa kutokana na kutoandaa vema fainali hizo.
Taarifa hizo za CAF kutoka Libreville, nchini Gabon zinathibitisha kwamba Kamati ya Utendaji ya CAF imeipa ushindi Tanzania dhidi ya timu ya Jamhuri ya Congo ambayo katika michuano ya kufuzu, ilimchezesha mchezaji Langa Lesse Bercy aliyezidi umri kinyume cha kanuni za kanuni za michuano hiyo.
Serengeti Boys ilikusanywa na kuandaliwa kwa michezo mingi ya kimataifa ambako kwa mwaka moja tu 2016, ilicheza mechi zisizopungua 16 ya kimataifa.
Katika michezo hiyo ya kirafiki na ushindani, Serengeti Boys ilipoteza mchezo wa 16 tu dhidi ya Congo ilihali kulikuwa na rufaa kuhusu mmoja wa wachezaji wa Congo ambaye alionekana kuwa na umri mkubwa. Mchezaji huyo ni Langa Lesse Bercy.
CAF, kwa nyakati tofauti ikiwamo Novemba 10, 2016 na Desemba 15, mwaka jana walitoa agizo kwa Congo Brazzaville kumpeleka kijana huyo Cairo, Misri kwa ajili ya vipimo vya MRI ili kuthibitisha au kupangua madai ya Tanzania. Congo Brazzaville hawakupeleka.
Langa Lesse
Januari 12, mwaka huu 2017 iliamriwa kwa mara nyingine kijana huyo kupelekwa jijini Libreville, Gabon ili kufanyiwa vipimo vya MRI, lakini hakupelekwa na katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF, kimeamua kumaliza suala hilo na kuipa ushindi Tanzania.
Siku 10 ziliisha Januari 23, mwaka huu lakini tangu hapo kumekuwa na maswali ya kutosha kuhoji nafasi ya Tanzania yakitoka kwa Watanzania kupitia wanahabari, lakini TFF ilisimama kidete kutangaza kuwa tunasubiri uthibitisho wa CAF ambayo leo Februari 3, mwaka huu imetangaza rasmi kuwa Tanzania itacheza fainali hizo.

↧
↧
MSANII BEN POL AMEFUNGUKA MENGI KUHUSU TUNDA

Msanii Ben Pol amefunguka na kuweka sawa juu ya tetesi ambazo zipo mtaani kuwa anatoka na video queen Tunda ambaye sasa inasemakana anatoka na rapa Young Dar es Salaam.
Ben Pol alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) alisema yeye alikuwa na urafiki wa mbali sana na Tunda na kusema hizo tetesi hazina ukweli kwani Tunda alikuwa rafiki wa karibu wa mdogo wake na si yeye.
"Siyo kweli sijawahi kuwa na mahusiano na Tunda nachojua mimi Tunda alikuwa karibu na mdogo wangu mimi yaani rafiki yangu wa karibu anaitwa Tonny Dagi, ndiyo alikuwa naye karibu sana, sijawahi kujua kama Tunda anajihusisha na mambo ya madawa ya kulevya sababu sijawahi kuwa karibu naye kivile, kusema nimekaa naye hata masaa sita au manne sijawahi kukaa naye karibu" alisema Ben Pol
Mbali na hilo Ben Pol alizungumzia suala la video Queen huyo kuhusishwa na madawa ya kulevya, anadai kama ni kweli anajihusisha na mambo hayo si jambo zuri sababu tayari yule amekuwa kioo cha jamii kuna mabinti wengi wanamuangalia na wengine wanatamani kuwa kama yeye hivyo si jambo jema yeye kuwa huko.
"Kama ametajwa kweli na anafanya hivyo vitu, kiukweli siyo kitu kizuri haileti picha nzuri yeye ameshakuwa na impact kubwa, mabinti wengi wanamuangalia, wengine wapo mashuleni huko wanatamani kuwa kama yeye, kuwa ma models, wanajulikana kwa hiyo haiwezi kuleta picha nzuri kama ni kweli inabidi aache" alisema Ben Pol
↧
JPCC KATI YA TANZANIA NA MALAWI NI CHACHU YA KUIMARISHA MAHUSIANO
JPCC kati ya Tanzania na Malawi ni chachu ya kuimarisha mahusiano
Wajumbe wanaoshiriki katika Kikao cha 4 cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi kilichofunguliwa leo jijini Lilongwe, Malawi wamehimizwa katika majadiliano yao ya siku tatu kubuni mkakati utakaowezesha kutatua changamoto zinazojitokeza kutokana na muingiliano mkubwa wa ngazi mbalimbali za ushirikiano baina ya wananchi wa mataifa hayo mawili.
Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Wataalam, Balozi Ramadhan Mwinyi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokuwa anasoma hotuba ya ufunguzi.
"Kama mnavyofahamu kunapokuwa na maingiliano makubwa ya wananchi wa nchi mbili kama zilivyo nchi zetu, changamoto haziwezi kukosa kujitokeza. Hivyo ni jukumu letu sisi wataalamu kubuni mkakati wa kuhakikisha kuwa changamoto hizo zinashughulikiwa haraka iwezekanavyo".
Balozi Mwinyi alieleza kuwa kikao hicho ni fursa nzuri kwa Serikali za Tanzania na Malawi kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi zao katika maeneo tofauti ikiwemo uchumi, uwekezaji, biashara, kutunza mazingira, elimu, Tehama, kilimo, uhamiaji, uchukuzi na masuala ya ulinzi na usalama, Hivyo alihimiza wajumbe wa pande zote mbili kuwa wabunifu katika majadiliano yao ili watoke na mipango inayotekelezeka kwa kuwa wananchi wanachohitaji ni maendeleo na sio mikakati inayoishia katika makabrasha.
Aidha, Balozi Mwinyi aliekeza kuwa watu wengi walistaajabu kusikia ujumbe wa Tanzania unakuja Malawi kushiriki kikao hiki kama walivyostaajabu kuona Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya mazungumzo hivi karibuni na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Peter Mutharika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Alisema hakuna cha kustaajabisha hapo, isipokuwa ifahamike lengo kuu la pande zote mbili ni kuona uhusiano kati ya Tanzania na Malawi unaimarishwa na kwamba mkutano huo ni ushahidi kuwa nchi hizi mbili zipo karibu zaidi kuliko hapo awali.
Naibu Katibu Mkuu aliihakikishia Serikali ya Malawi kuwa Serikali ya Tanzania imedhamiria kushirikiana na nchi hiyo katika kuboresha mahusiano ya kidiplomasia, uchumi na kijamii, hivyo alisisitiza umuhimu wa yale yote yatakayoafikiwa katika mkutano huo yanatekelezwa katika muda uliopangwa. Alishauri iundwe timu ya ngazi ya Makatibu Wakuu ambayo itakuwa inakutana kila baada ya miezi sita kutathmini utekelezaji wa maazimio ya kikao hicho.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Dkt. Dalitso Kabambe alisisitiza umuhimu wa nchi hizi mbili kuweka mikakati itakayorahisisha wananchi kufanya biashara bila vikwazo. "Bisahara ni jambo muhimu lazima tuhakikishe kuwa Serikali zetu zinaweka mazingira mazuri ili wananchi wafanye biashara kwa wepesi".
Kikao hicho kinatarajiwa kufungwa rasmi na Mawaziri wa Mambo ya Nje siku ya Jumapili tarehe 05 Februari 2017 ambapo Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anatarajiwa kuwasili Malawi tarehe 04 Februari 2017. Mawaziri hao pia wataweka saini Mikataba mitatu ya ushirikiano katika mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia, usafiri wa anga na utalii.
Wajumbe wa Tanzania katika kikao hicho wanatoka katika sekta mbalimbali wakiwemo wajumbe kutoka mikoa miwili ya Mbeya na Ruvuma inayopakana na Malawi ambao wanaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla.
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi na Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha JPCC kati ya Tanzania na Malawi, Dkt. Kalitso Kabambe akisoma hotuba ya iufunguzi na ukaribisho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akisoma houtuba ya ufunguzi wa kikao cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Dkt. Dalitso Kabambe. Kikao hicho kinafanyika Lilongwe, Malawi kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 03 Februari 2017.
Wajumbe wa Tanzania wakisikiliza hotuba za Makatibu Wakuu. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Suleiman Salehe na Kaimu Mkurugenzi kutoka Mamlka ya Viwanja vya Ndege.
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Ali Ubwa na mjumbe mwingine ambaye jina lake halikupatikana.
Bw. Kalitso Kabambe akiwa na Balozi wa Malawi nchini Tanzania.
Sehemu ya ujumbe wa Malawi ukifuatilia hotuba za ufunguzi
Wajumbe wa pande zote mbili wakiwa katika kikao cha JPCC
Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mwinyi akihojiwa na Mwandishi wa TBC, Bw. Hosea Cheo
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Victoria Mwakasege akihojiwa na Mwandishi wa TBC
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla akifanya mahojiano na Mwandishi wa TBC
↧
STAA DIAOMOND PLATNUMZ AAKWAMA KUREJEA KWA ZARI
Msanii wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaduwaza ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kumpokea baada ya kutua kutokea Sauzi akiwa peke yake, tofauti na ilivyotarajiwa kuwa angerejea na mzazi mwenzake, Zarina Hassan ‘Zari’.
Awali zilivuja taarifa kuwa, Diamond amekwenda Sauzi kumchukua Zari na mtoto wao aliyezaliwa hivi karibuni, Nillan ili waje kufanya sherehe kidogo.
Kufuatia taarifa hizo, Jumatatu iliyopita, nyakati za jioni, watu wa karibu na Diamond walifika ‘airport’ kuwapokea lakini kilichowashangaza wengi ni kumuona anatoka mwenyewe na mabegi yake, jambo lililowafanya wahisi kuna kitu.
“Hee, mbona yuko peke yake sasa? Zari na watoto wako wapi sasa? Au wamezinguana?” alisikika akisema mmoja wa akinadada waliokuwa uwanjani hapo.
Mbali na dada huyo, wengi walionekana kunong’ona kuonesha kutoamini wanachokiona na kwa kuwa Diamond alijua kuwa kawaangusha kwa kutokuja na Zari, hakuwa na mbwembwe zaidi ya kwenda kwenye gari lililokuwa limeletwa na kijana aitwaye Q Boy, wakaondoka zao.
↧
VITA YA MADAWA YA KULEVYA: ASKARI 12 WALIOTUHUMIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA WASIMAMISHWA KAZI
Kufuatia tuhuma zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda zikiwahusisha baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi Askari 12 waliotuhumiwa ili uchunguzi ufanyike dhidi yao.Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi uliopita, IGP Mangu alisema ni lazima Jeshi la polisi lichukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo, hata kama ni Askari."Jeshi la Polisi linachukua hatua madhubuti za kuwachunguza Askari na Wasanii waliotuhumiwa na baada ya uchunguzi kumamilika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayethibitika kwa uhalifu huo" alisema IGP Mangu.Pia IGP Mangu ameiomba jamii kuendelea kutoa taarifa za uhalifu wa aina yeyote ili nchi iendelee kuwa salama.hapo chini ni Majina ya Askari wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya, ambao wamesimamishwa kazi.
↧
↧
HAYA NDIO MANEMO YALIYOTOA DITTO BAADA YA JINA LAKE KUTAJWA KWENYE LISTI YA RC MAKONDA

Mwimbaji Ditto ambaye ni mmiliki wa hit single ‘moyo sukuma damu‘ amefafanua kuhusu kilichoendelea baada ya jina la Ditto kusikika kwenye orodha ya Watuhumiwa wa utumiaji/uuzaji dawa za kulevya iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Baada ya jina lake kutajwa baadhi ya watu walianza kumtukana na wengine kumpigia simu nyingi wakidhani ni yeye katajwa lakini ametoa ufafanuzi leo kwamba hakuwa yeye bali ni jina tu lilikosewa na kwamba yuko huru na anaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Amesema amepata usumbufu kiasi chake kwa kupigiwa simu mara kwa mara lakini pia kwa baadhi ya watu kutokujua kwamba jina lilikosewa hivyo wakaanza kumshutumu, kutoa matusi na kumlaumu moja kwa moja.
↧
NAPE AIPONGEZA SERENGETI BOYS KWA KUFUZU FAINALI ZA AFCON GABON 2017
↧
DC SHINYANGA AONGOZA KONGAMANO LA WAFANYA BIASHARA WA WILAYA YAKE
Ijumaa Februari 03,2017 kumefanyika Kongamano la wafanyabiashara kutoka wilaya ya Shinyanga lililoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo(TCCIA) kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.Kongamano hilo lililokutanisha wafanyabishara kutoka Shinyanga Mjini na Vijijini na nje ya mkoa wa Shinyanga lililenga la kuibua na kujadili fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga na kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo.Mgeni rasmi katika Kongamano hilo ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.
Kushoto ni mgeni rasmi katika kongamano la wafanyabiashara ,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga,(TCCIA) Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack wakiwa katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga leo Ijumaa Februari 3 2017
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Sekretariati wakiwa ukumbini
Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira aliyemwakilisha katibu tawala wa wilaya hiyo akitambulisha viongozi wa serikali waliohudhuria kongamano hilo
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia wafanyabiashara
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia wafanyabiashara,kulia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack akizungumza wa kufungua kongamano hilo ambapo alisema wameamua kukutana ili kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack alitumia fursa hiyo kumpongeza rais John Pombe Magufuli kwa kuhimiza uchumi wa viwanda na kuahidi kuwa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga wapo tayari kumuunga mkono
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack pia aliiomba serikali kupunguza rundo la kodi kwawafanyabiashara kwani kodi hioz zinawakatisha tamaa kuendelea kufanya biashara
Meneja wa Benki ya Maendeleo -TIB Kanda ya ziwa Zacharia Kicharo akitoa mada wakati wa kongamano hilo
Meneja Miradi kutoka Tanzania Local Enterprise Development (TLED) Stanley Magese akitoa mada wakati wa kongamano hilo
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Kongamano linaendelea
Mwalimu wa walipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga Anthony Faustine akitoa mada kuhusu ulipaji kodi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwahutubia wafanyabiashara wilaya ya Shinyanga waliohudhuria kongamano hilo ambapo aliwaasa kujitokeza kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda kwani serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli inataka watanzania kuwekeza katika viwanda
Mkuu huyo wa wilaya Josephine Matiro alisema serikali ya wilaya ya Shinyanga ipo tayari kushirikiana na wafanyabishara katika kukuza uchumi wa mkoa wa Shinyanga
Matiro aliwapongeza wafanyabiashara waliojitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwaomba kuendelea kuwekeza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akizungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kushoto) akiteta jambo na mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack na katibu wa Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo
Mc Mama Sabuni anayeongoza Kongamano hilo akiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
Wafanyabisahara wakiwa ukumbini.Kulia ni mkurugenzi wa Vigimark Hotel bi Victoria Majige
Tunafuatilia kinachoendelea
Kulia ni Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo,kushoto ni Afisa tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui akitoa mada wakati wa kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wafanyabiashara kujenga mazingira ya kukopesheka,kuwa waaminifu na kulipa madeni yao kwa wakati kama wanavyokubaliana na benki
Pamui alitumia fursa hiyo kuwapongeza wafanyabiashara wilaya ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwataka kujenga utamaduni wa kujitokeza katika vikao na mikutano mbalimbali ili kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu mpya za kufanya biashara.
Wafanyabiashara wakifuatilia yanaliyokuwa yanajiri ukumbini
Mkurugenzi wa Vigimark Hotel iliyopo mjini Shinyanga Victoria Majige akizungumzia changamoto ya ubovu wa barabara inayoelekea katika hoteli hiyo ambapo aliiomba serikali kutengeneza barabara hiyo walau kwa kiwango cha moramu
Mfanyabshara wa Uyoga wilayani Shinyanga Hamisa Nuhu akichangia hoja wakati wa kongamano hilo
Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akichangia hoja ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Katibu wa Wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Shinyanga Gregory Kigusi akichangia hoja ukumbini
Katibu wa TCCIA Marcelina Saulo akielezea kuhusu namna wafanyabishara wanavyokerwa na bei kubwa ya mabango ya matangazo na kuiomba serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za matangazo kwani inawakatisha tamaa wafanyabishara na kuamua kuondoa matangazo
Afisa Biashara wa manispaa ya Shinyanga Sunday akieleza namna serikali inavyofanya kuhakikisha kuwa gharama za matangazo inapungua
Mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga Dotto Mdoe akijitambulisha kwa wafanyabishara ambapo alisema serikali itaendelea kuwalinda wafanyabiashara katika kuuweka mji wa Shinyanga salama
MC Mama Sabuni akifanya yake ukumbini
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono akizungumza wakati kufunga kongamano hilo ambapo aliwaomba wafanyabiashara kujitokeza kutoa taarifa za watumishi ama idara yoyote inayowaomba rushwa katika biashara zao.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
↧
WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI WA IRAN NA OMAN
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Iran Nchini Tanzania Mhe.Mousa Ahmed Farhang aliwasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akizungumza mara baada ya nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Iran nchini Tanzania Mhe.Farhang. Kushoto ni Maafisa kutoka Ofisi za Ubalozi wa Iran nchini na Maafisa Kutoka Wizarani (kulia) wakifuatilia mazungumzo. Katika mazungumzo hayo Waziri alimkaribisha Balozi na kumhaidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika utekelezazi wa majukumu yake na kwa nchi ya Iran kwa ujumla, ili kuendeleza na kudumisha uhusiano wa Kidiplomasia uliodumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na Iran.
Waziri Mhe. Balozi Dk. Mahiga akizungumza na mgeni wake Mhe.Balozi Farhang
Balozi Mteule wa Iran Mhe. Farhang akizunguza mara baada ya kuwasilisha nakala za hati za utambulisho ![]()

Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Iran nchini Tanzania Mhe. Farhang
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Oman nchini Mhe. Ali A. Al Mahruqi alipowasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga na Balozi Mteule wa Oman nchini Tanzania Mhe. Mahruqi wakionesha nakala ya hati ya utambulisho
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akimsikiliza Balozi Mteule wa Oman nchini
Mazungumzo yakiendelea, Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Abasi Kilima akifuatila mazungumzo
Picha ya pamoja
↧
↧
STAA WEMA SEPETU AZIMA WIMBO MPYA WA DIAMOND PLATNUMZ NA NE-YO
Safari hii inaweza ikawa ni bad timing kwa mwanamuziki mashuhuli Africa, diamond platinum, baada ya hivi karibuni kuachia video ya wimbo wake mpya huitwao Marry me aliomshirikisha mwanamuziki Ne-yo kutoka marekani. Video hiyo inasemekana kufanyiwa fitina ya coincidence na mwana dada mwenye mvuto na umaarufu wa aina yake nchini,
Wema sepetu ambapo scandal inayomkabili kwa sasa kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya kuvuta hisia kwa mashabiki zake na maadui zake, hali ambayo imefanya kila mmoja kuvutiwa na story ya mrembo hyo asiyekaukiwa na drama kuliko habari za msanii yeyote nchini kwa sasa (akiwemo diamond na zari). Wema kwa sasa amekuwa dhahabu kwa waandishi wa habari,
Kila mtu anataka kuandika habari zake, nadhani ujio wake mpya pamoja na uzinduzi wake wa app yake bila kusahau scandal ya utumiaji madawa ya kulevya, vinatajwa kumuweka msanii huyo kwenye level za juu zaidi kuliko msanii yeyote kwa sasa.
By warumi
↧
MAKAMBA AWATAHADHARISHA WATAALAM WA ATHARI ZA MAZINGIRA KUHUSU UWEPO WA VISHOKA KATIKA TASNIA HIYO:

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Yusuph Makamba akiongea na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa Tathminiya Athari za Mazingira nchini Dar es Salaam jana (leo) Na: Frank Shija – MAELEZO
Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini wametahadharishwa kuwepo kwa matapeli wanaingilia taaluma hiyo kwa lengo la kufanya udanganyifu na kujipatia kipato.Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira Tanzania (TEEA) leo Jijini Dar es Saalam.Makamba amesema kuwa taaluma ya tathmini ya Athari za Mazingira ni ya shughuli ambayo inahitaji mkubwa sana na ni kwa mujibu wa sheria za nchi lakini kumekuwapo na makanjanja ambao wamekuwa wakifanya uraghai kwa wawekezaji na kutia doa tasnia nzima ya taaluma ya uthamini wa athari za mazingira.
“Serikali inakusudia kubadilisha kanuni na taratibu ili kuongeza udhibiti wa udanganyifu katika eneo la Tathmini ya Athari za Mazingira(IAE) kwa kuweka viwango stahiki kwa wataalamu wa tathmini ya athari za mazingira vitakavyozingatia elimu na uzoefu,” alisema Makamba.Aliongeza kuwa ni vyema sasa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Chama cha Wataalumu hao kushirikiana kuhakikisha taaluma hiyo haingiliwi na makanjanja ili kufanikisha utoaji wa huduma zenye viwango stahiki na vya kuridhisha.
Awali akiwasilisha salamu za Bodi ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Profesa Ruben Mwamakimbullah amesema amemshukuru Waziri Makamba kwa kukubali kujumuika na wataalamu hao katika mkutano huo muhimu na kuongeza kuwa wao kama Bodi watafanyia kazi ushauri wote alioutoa na kuahidi kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta heshi kwa tasnia ya tathmini ya athari za mazingira na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Bonaventure Baya amesema kuwa mkutano huo umekuwa ukiwakutanisha Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini ambapo utumia fursa hiyo kukumbushana mambo yanayohusu weledi na majukumu yao.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa mkutano huo ni wa tatu kufanyika ambapo umetanguliwa na mikutano iliyofanyika februari 2011 na Machi 2015 na kuongeza kuwa NEMC imekuwa ikiratibu mkutano huo kwa lengo la kuwakutanisha Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini ili kujadili changamoto zao na kupeana uzoefu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Yusuph Makamba akiongea na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa Tathminiya Athari za Mazingira jijini Dar es Salaam jana (leo) ).

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mwandisi Bonaventure Baya akiongea na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini Dar es Salaam jana (leo)

Mjumbe wa Bodi wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Ruben Mwamakimbullah akitoa salamu za Bodi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Mazingira Prof. Salome Misana katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam waTathmini ya Athari za Mazingira Dar es Salaam jana (leo))

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Yusuph Makamba akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini Dar es Salaam jana (leo).(Pichazotena Benjamin Sawe)
↧
CHID MAPENZI ATOA MANENO HAYA KWA WATU WANAOTAKA KUMCHAFUA MKE WAKE(+VIDEO)
↧