Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live

MSANII HARMORAPA AENDA KITUO CHA POLISI KUHAKIKI JINA LAKE KAMA LIPO

$
0
0
Harmorapa ameonesha yeye sio mtu wa mchezomchezo linapokuja suala la afya ya akili na hasa maisha ya vijana wenzake.

Majira ya saa nane maeneo ya centrral police, Harmorapa alionekana kaunta akijaribu kuangalia kama kuna uwezakano wowote ule jina lake likawepo hapo either kama mtumiaji au punda, lakini kwa bahati nzuri anadai halikuwepo.

Akiongea na wahandishi wa habari baada ya kuthibisha jina lake halikuwepo ,Harmorapa amedai alipata maelfu ya sms kutoka kwa mashabiki wake ambao walitaka afatualie suala hilo polisi maana hawako tayari kumuona akipotea kwenye game na hasa kipindi hiki ambacho ameonekana kuziba ombwe la msanii anayetuwakilisha kimataifa.

pia msanii huyo amewaomba wasanii watumie muda mwingi studio na location na wajiatahidi kukaa mbali na maeneo ya Kinondoni hasa wanapokuwa na stress.

By Msaga Sumu

VODACOM YAZINDUA SIMU MPYA ZA SMART BOMBA

$
0
0
Sasa ni wakati wa watanzania kufurahia ubunifu wa kiteknolojia wa mawasiliano unaoendana sambamba na mazingira yao halisi na kufurahia kupata taarifa na burudani kwa njia ya interneti ambapo kuanzia leo wateja wa Vodacom,
mtandao unaoongoza nchini wataweza kujipatia simu za kisasa zinazotumia interneti aina ya Smart Bomba.
Simu za Smart Bomba ambazo zimezinduliwa rasmi nchini leo zinapatikana kwa gharama nafuu ya shilingi 99,000/-muundo wa matumizi yake uko katika lugha ya taifa ya Kiswahili pia zinanunuliwa zikiwa tayari zimeunganishwa na kifurushi cha interneti chenye GB 10 za buree kwa mwezi na ofa hii inatolewa katika kipindi cha miezi 3 mfululizo kwa ajili ya kumuwezesha mteja kupata na kufurahia intanenti yenye kasi kubwa ya Vodacom mahali popote na wakati wowote.
Mbali na muundo wa matumizi ya simu hii kuwa katika lugha ya Kiswahili na kwendana na mazingira halisi ya maisha ya watanzania walio wengi,simu za Smart Bomba zina umbo la kuvutia,nyepesi na zina kioo cha mbele,cha ukubwa wa kutosha,zinafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya android inaongeza kasi ya kuperuzi internet,inayo kamera ya kurekodi na kupiga picha kwa kiwango chenye ubora wa hali ya juu vilevile inao mfumo wa utambuzi wa ramani ya maeneo mbalimbali ujulikanao kama GPS ambao unatoa maelekezo kuonyesha mahali mtu alipo na mahali aendapo kwa urahisi hususani madereva wa teksi ambao huwapeleka wateja wao sehemu mbalimbali wasiozijua,na zimeunganishwa na program za simu za kurahisisha Maisha za Vodacom kama vile M-Paper
Balozi wa Vodacom Tanzania,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond Platinumz” akiongea na wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya Dar es Salaam, Domician Mkama
Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu hii,Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya Dar es Salaam,Domician Mkama,alisema wakati ni huu wa kila mtanzania kuweza kufurahia matumizi ya simu za kisasa zinazotumia internet (Smart Phones) kwa ajili ya kupata taarifa na burudani kutoka mitandaoni kutokana na kupatikana kwa mara ya kwanza kwa gharama nafuu nchini.
“Kuingia sokoni kwa simu za Smart Bomba za gharama nafuu na zilizotengenezwa kwendana sambamba na mazingira na Maisha ya watanzania walio wengi zikiwa zimeunganishwa na GB 30 kwa matumizi ya miezi 3 ya mwanzoni ni ofa ya kipekee ambayo imebuniwa kubadilisha maisha ya wateja wetu walio wengi na kuendelea kuyafanya kuwa murua”.
Mkama aliongeza kusema “Hivi sasa tuko katika zama za kidigitali ambayo mawasiliano ya watu wengi yanafanyika kupitia mitandao ya kijamii ,hivyo wananchi wengi wakiwa na simu za kisasa zinazotumia internet wanaweza kufanya mambo mengi kwa urahisi na haraka kuanzua kwenye biashara,kupata taarifa mbalimbali,kutumiana salamu na kupata burudani za muziki na sinema kutoka mitandaoni”.Alisema.
Alisema wakati ni huu kwa makundi mbalimbali ya watanzania katika jamii kuchangamkia fursa hii pekee kwa kununua simu ya Smart Bomba kwa gharama nafuu na kuwa mtu wa kisasa anayeenda na wakati na simu hizi zinatukuwa zinapatikana kwenye maduka yote yanayouza simu nchini na zina waranti ya mwaka mmoja.
Balozi wa Vodacom Tanzania,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond Platinumz” akiwaburudisha wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3
Kwa kutambua kuwa kundi kubwa kwenye jamii linahitaji matumizi ya intanenti kupata burudani na kupakua muziki hususani muziki wa Bongo Flava,uzinduzi wa simu hii na matangazo yake yamemuhusisha mwanamuzi nguli wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo,Diamond Platnumz aliwapongeza Vodacom kwa kuingiza sokoni simu ya kisasa ya Smart Bomba ambayo imelenga kutumiwa na wananchi wengi kwa kuwa ina unafuu na inaendana na Maisha halisi ya watanzania. “Sasa ni wakati wa kila mtanzania kwenda kidigitali kwa ku chart,kupata nyimbo za wazipendazo live kupitia simu zao na kupakua filamu wazipendazo ,kutumiana salamu na picha kwa njia ya simu,kuperuzi internet na kupata taarifa na burudani kupitia ncha za vidole vyao na haya yote yanapatikana katika mtandao mkubwa nchini wa Vodacom pekee.

RAPA AY AFUNGUKIA URITHI WA MAMA YAKE

$
0
0
IKIWA ni miaka nane sasa tangu mama mzazi wa Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Ambwene Yessayah ‘AY’, Lydia Bizima afariki dunia, staa huyo ameibuka na kueleza urithi alioachiwa na mama yake.
Akibonga na Mikito Nusunusu , AY alisema enzi za uhai wa mama yake alikuwa akimuhusia sana kuhusu kujiamini, kujituma ambapo kila
anapoyakumbuka maneno hayo, anajikuta akipata nguvu na kufanya mambo makubwa na mazuri zaidi. “Mama yangu kipenzi aliniachia urithi mzuri kwani mara nyingi alikuwa akinisisitizia kuwa ni lazima nijiamini, nijitume na nifanye kazi nzuri kwa sababu yeye pia alikuwa anajiamini sana na mpiganaji hivyo nimeufanyia kazi ndiyo maana niko hivi nilivyo leo,” alisema AY

IGP ERNEST MANGU AWASIMAMISHA KAZI ASKARI POLISI WALIOTAJWA NA RC MAKONDA

$
0
0

Zikiwa zimepita siku mbili toka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kutaja majina ya baadhi ya askari polisi pamoja na wasanii mbalimbali wakituhumiwa kuhusika katika ufanyaji wa biashara za madawa ya kulevya na matumizi ya madawa hayo

IGP Ernest Mangu leo amewasimamisha kazi askari 12 

Kufuatia sakata hilo la madawa ya kulevya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi askari 12 kupisha uchunguzi baada ya askari hao kutajwa kushirikiana na wauza madawa ya kulevya.

Yafuatayo ni majina ya askari hao 12 ambao wamesimamishwa kazi le kupisha uchunguzi dhidi yao 

WAZIRI NAPE AIPONGEZA SERENGETI BOYS KWA KUFUZU FAINALI ZA AFCON GABON 2017

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye

LEMUTUZ AENDELEA KUINGIZA MKWANJA NA KULA BATA BUSHARA NA MASTAA HAWA.

$
0
0

Watu wengi tumekuwa na mitazamo ambayo imekuwa haitusaidii hata chembe, kwani tumekuwa tunaamini katika kufanya kazi peke yetu pasipo kuwashirikisha wengine, lakini kufanya hivi ni sawa na kuzima moto kwa chafya, lakini ukweli ambao haufichiki ni kwamba ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako ila ukitaka kwenda mbali nenda na wengine.



Hiyo ni falsafa nzuri sana husani katika suala zima la kuyasaka mafanikio. Pia katika suala zima la mafanikio tukumbuke ule usemi ambao husema ushirikiano ni nguvu na utengano ni dhaifu.

Ili kulielewa hili vizuri la kufanya kazi kwa shirikiano hebu angalia picha za mfalme wa mitandao ya kijamii hapa bongo Lemutuz Nation akiwa na mastaa hawa wakila bata.


















KAIMU MKURUGEZI MTENDAJI WA TANESCO, DKT.TITO MWINUKA AKAGUA VITUO VYA KUPOZA UMEME VYA WILAYA YA TEMEKE NA KARIAKOO

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt.Tito E. Mwinuka, (pichani kushoto), amefanya ziara ya kutembelea vituo vitatu vya kupoza na kusambaza umeme wa msongo wa Kilovoti 132, (132Kv), vya Mbagala, Kurasini Wilayani Temeke na Kariakoo Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari 4, 2016 na kuwaomba wateja wa Shirika hilo kuwa wavumilivu wakati juhudi za kukamilisha mradi wa uboreshaji umeme ukiwa unakaribia kukamilika.
Dkt. Mwinuka alisema,  ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi katika maeneo ya Mbagala, Kigamboni na Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, kumepelekea upatikanaji wa umeme kwenye maeneo hayo kuwa na matatizo kidogo kwani vituo vinavyosambaza umeme kwenye maeneo hayo vilikuwa na ukubwa wa kupoza umeme wa Kilovoti 33 tu, na ndio maana TANESCO kupitia Mradi wa uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam unakaribia kukamilisha ujenzi wa vituo vilivyotajwa hapo juu ili view na uwezo mkubwa wa Kilovoti 132 na hivyo kuondoa kabisa tatizo hilo.
“Barabra zinapozidiwa na magari ni rahisi sana kubaini kutokana na ongezeko la magari yanayotumia barabara hizo, lakini ongezeko la watumiaji umeme na shughuli za kiuchumi inakuwa vigumu kubaini kwa haraka, kwa hivyo niwaombe wateja wetu kuwa wavumilivu kwani tatizo hilo litakuwa limepatiwa ufumbuzi katika kipindi kifupi kijacho.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Dkt. Mwinuka pia aibainisha, kuwa kazi ya kuongeza ukubwa wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme inaendelea kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi ambako nako vituo vya sasa vya ukubwa wa Kilovoti 33, vinabadilishwa na kuwa na uwezo wa Kilovolti 132.
Dkt. Mwinuka amewapongeza wakandarasi kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa haraka ili kuwaondolea adha wateja wa Shirika hilo wa upatikanaji wa umeme ulio bora na wa uhakika.

 Dkt. Mwinuka (kulia), akipatiwa maelezo ya litaalamu na Mkuu wa miradi (anayeshughulikia usafirishaji) wa TANESCO, Mhandisi Frank Mashalo, alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Februari 4, 2017. Wakwanza kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.
 Mitambo ya kupoza na kusafirisha umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, kikiwa katika hatua za mwisho ukamilika
 Dkt. Mwinuka, (wapili kulia), akimsikiliza mkandarasi kutoka kampuni ya FICHTNER, ambaye ndiyo Menenja mradi, Mathias Alby, wakati alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula Maendeleo, (kushoto), akitoa maelezo ya kiutendaji kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Tito E.Mwinuka, wakati wa ziara yake ya kutembelea vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Mbagala na Kurasini vilivyoko Wilayani Temeka. Katikati ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya.
 Dkt. Mwinuka (mbele), baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Dkt. Mwinuka, (wapili kulia) akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia miradi ya usafirishaji na usambazaji umeme, Mhandisi Gregory Chegere, (kushoto), wakati alipotembelea kituo cha Kurasini. Kulia ni
Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya.
 Muhandisi mwandamizi wa miradi wa TANESCO, Mhandisi Rosmystice Luteganya, (kushoto), akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka, kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Dkt. Mwinuka, (kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Fundi akiwa kazini kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo
 Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya, (aliyesimama), akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara hiyo, kwenye chuo cha TANESCO jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Dkt. Mwinuka, Mhandisi Chegere na Mhandisi Mashalo.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumza wakati wa kikao hicho.
 Jengo la kituo cha bkupoza na kusambaza umeme wa msongo wa Kilovolti 132 cha Mbagala jijini Dar es Salaam, likiwa limekamilika
Meneja wa TANESCO Wilayani Temeke, Mhandisi, Jahulula Maendeleo, (kulia), akizungumza na maafisa wa TANESCO wakati wakimsibiri Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Rito E. Mwinuka kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala jijini Dar es Salaam.

STAA JUSTIN BIEBER AMEREJEA UPYA KWENYE INSTAGRAM

$
0
0

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, Justin Bieber amerudi upya na jina lake lilelile la @justinbieber.

Ila Good Newz inaonekana ujio huu wa kurudi kwenye kurasa yake ya Instagram inaonyesha kwamba Bieber amepewa donge nono kutoka mtandao wa T Mobile ambao ameshindwa kuzuia unono huo.

HUU HAPA WIMBO WA MWANA FA ULIOTIMIZA MIAKA 15 TANGU KUANZA KUCHEZWA REDIONI

$
0
0

Hit maker wa ‘Dume Suruali’, Mwana FA afunguka juu ya ngoma yake iliyotimiza miaka 15 tangu kuanza kuchezwa katika redio mbalimbali. Ni wazi kabisa Dume suruali ni wimbo wake unaofanya vyema ndani ya nchi na nje pia.

Mwana Fa ni moja kati ya marapa bora walioko chini ya kivuli cha hip hop, ambaye tangu aingie katika ramani ya muziki wa kizazi kipya hajawahi kupoteza ubora wake.
Mwana Fa amekuwa msanii tofauti zaidi na wengine katika upande wa kutunza rekodi za muziki wake. Ni wazi changamoto moja wapo ya wasanii wa kizazi kipya ni kutokujua kutunza rekodi ya mambo yote katika muziki wao.
Kupitia akaunti yake ya ‘Instagram’ Mwana Fa ameweka wazi rekodi zake katika maisha yake ya muziki, ambapo ameeleza
Mwana Fa
“2/2/2017 Ni miaka 15 ‘cash’ toka mara ya kwanza wimbo wangu umepigwa redioni..Ingekuwa Vipi feat Jay Mo produced by Bon Luv nashukuru! Lakini pia hakuacha kuweka wazi wake ambao anaupenda zaidi ambao ni ‘Mfalme’ akiwa amemshirikisha G Nako.

PICHA ZA VIJIJI 15 VYENYE MVUTO ZAIDI DUNIANI

$
0
0
Tumezoea kuona miji mikubwa ikiwa na muonekano mzuri na ya kuvutia, lakini unaambiwa kuna vijiji pia duniani ni vizuri kwa muonekano,  leo nimekutana na hii list ya vijiji 15 ambavyo vinavutia zaidi duniani.

15. Alberobello- Italy
14. Pariangan-Indonesia
13. Savoca-Italy
12. Göreme-Uturuki
11. Madison-Marekani
10. Júzcar-Spain
9. Reine-Norway

8. Sidi Bou Said-Tunisia

7. Wengen-Switzerland
6. Shirakawa-go-Japan
5. Burano-Italy
4. Bibury-Uingereza
3. Hallstatt-Austria
2. Oia-Ugiriki

1. Eze-Ufaransa

YOUNG KILLER AKIRI JAMBO HILI KUMUHUSU DOGO JANJA

$
0
0
Rapa Young Killer amefunguka na kuweka wazi kuwa ni kweli alikuwa ‘Inspired’ kuingia kwenye muziki na msanii Dogo Janja kwani yeye alikuwa anaamini ili msanii aweze kufanikiwa na kutoba kwenye muziki ni lazima awe na umri fulani.

Young Killer alisema hayo jana baada ya kukutanishwa live yeye pamoja na Dogo Janja kwenye kipindi cha FNL ndipo alipokiri kuwa baada ya kuona Dogo Janja ametoboa na kuwa mkubwa ndiyo yeye akaongeza nguvu za mitikasi mpka na yeye akatoka kimuziki.
Dogo-Janja-681x851 (1)-horz
Dogo Janja & Young KIller
“Mimi napendaga kusema ukweli kipindi nahangaika na mishe zangu nilikuwa naamini ili utoboe kwenye muziki ni lazima uwe na umri fulani, sawa Young D alikuwepo na alipata nafasi tukawa tunamuona kwenye matangazo ya show na nini lakini nilikuwa sijaamini kama katoboa.
“Au anaweza kufanya kama tunavyofanya sasa lakini Janjaro alipokuja kutoka ndiyo nikaamini kabisa kumbe unaweza kutoboa ukiwa na hali yoyote muda huo huo na mimi nikaanza kujipanga nikapata mashavu kwa hiyo alikuwa Inspiration kwangu” alisema Young Killer.

RAPA COUNTRY BOY AJA NA BIASHARA HII IFAHAMU HAPA

$
0
0
Katika ulimwengu wa sasa ambao ajira zimekuwa ngumu na shida kupatikana, ujasiriamali na biashara vimekuwa ndio kimbilio la wengi. Watu wengi wanaingia kwenye biashara kama njia kuu ya kujipatia kipato.

Hitmaker wa ngoma ya “Hakuna Matata” Country Boy ameamua kutazama upande wa pili wa biashara tofauti na muziki ikiwa ni katika suala zima la kujitafutia kipato
16229408_313969388998823_4438854391247667200_n

Country Boy
Ikiwa muziki ni biashara ambayo inakwenda na wakati, mkali huyo ameamua kuitazama kwa jicho hilo ili kujiwekea misingi mizuri katika kujipatia kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.
Yawezekana ndoto za baadhi ya wasanii wengi ni kumiliki migahawa ya Chakula lakini huenda kinachosumbua ikawa ni mitaji au namna ya kuanza biashara hiyo rasmi.
Country Boy ameingia kwenye list ya Wasanii wa Bongo walioamua kuwekeza muda wao katika kutoa huduma ya Chakula na huduma hiyo ameipa jina la Country fast food delivery ambayo kazi yake ni kusambaza chakula kwa yoyote anaehitaji.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Country Boy alipost ujumbe huu..
Country Boy
Ujumbe huo ulisomeka hivi.. “Inshaallah kesho Tunaanza Country Fast Food Delivery Msosi Heavy Kwaajili Yako Chenye Upishi Mzuri Na Smart Mapishi Ya Kinyumbani Kabisaa”.

KAMANDA SIRRO:WEMA SEPETU,TID,NA NYANDU TOZZI BADO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

$
0
0
Wakati macho na masikio ya Watanzania wakisubiri kusikia hatma ya wasanii wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya, wasanii wanne waliofika Kituo Kikuu cha Polisi bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa bado wasanii hao Wema Sepetu, Dogo Hamidu, Khalid Mohamed (TID), na mtangazaji maarufu wa Clouds TV Babuu wa Kitaa bado wanashikiliwa na jeshi hilo.
“Bado tunawashikilia kwa mahojiano zaidi,” amesema Sirro kwa kifupi.
Wasanii wengine waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambao wanatakiwa kufika kituoni Jumatatu ni Vanessa Mdee, Tunda na watu wengine Halidali Kavila, Amani, Kashozi na Omry Sanga.

HII NDIO SAFARI YA MUZIKI YA REYVANNY WA WCB

$
0
0
Msanii Raymond alimaarufu kama Ray Vanny amefunguka na kuweka wazi safari yake ya muziki toka ameanza mpaka kufikia hatua kuingia chini ya usimamizi wa label ya WCB Wasafi chini ya Diamond Platnumz.

Ray Vanny kupitia kipindi cha 'Ngaz kwa ngaz' kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana anasema mwanzo kabisaa alianza kuandika, akaja kurap kisha akaingia kwenye kuimba.
"Mimi nilianza kwanza kuandika, kurap kisha nikaja kuimba, kwa sababu kuimba kama kuimba, kujua vizuri kupanga sauti nimejifunza kanisani, baada ya hapo ndipo nilianza kuandika ngoma za kuimba, tulikuwa watu kama sita na wote tulienda kanisani na walituambia kuna masuala ya kwaya, kwa hiyo siku hiyo hiyo tumeingia kanisani tukaingia kwenye kwaya ya kanisa. Alisema Ray Vanny 
Ray Vanny anasema akiwa kanisani ndipo alipojengeka kimuziki na kudai baadaye alikuja kushiriki katika mashindano ya Free Style wakati bado yupo shule, pia anadai kipindi ana rap kwenye mashindano kuna mtu alimwambia yeye ni mzuri zaidi kwenye kuimba kuliko kuchana.
"Niliposhiriki mashindano ya Free style  kuna mtu alinisikia nikiimba, akasema wewe upo vizuri zaidi kwenye kuimba. Basi niliendelea kurap nikashinda ki mkoa, baadaye tukashindanishwa Tanzania nzima nikashinda nikawa namba moja, kiukweli sikujua kama muziki una pesa hivi ila baada ya kushinda mashindano ya free style Tanzania nzima nikapewa mtonyo hapo ndipo niliposema haiwezekani ngoja nibadilishe filamu" alisema Ray Vanny 
Hapo ndipo Ray Vanny anasema safari yake kwenye muziki ilipokolea kwani pesa zile zilimfanya kuanza kuandika ngoma zake mwenyewe, zikamfanya aanze kuimba imba hadi alipoingia chini ya usimamizi wa Tip top Connection na baadaye kuingia WCB Wasafi.  

TAZAMA PICHA ZA HARMO RAPA AKIJIACHIA NA MPENZI WAKE


THE MAGAZETI YA BONGO LEO SUNDAY/JUMAPILI 05/02/2017 LIVE

TUNDA MAN ANYOOSHA MAELEZO BAADA YA RC MAKONDA KUMTAJA KWENYE TUHUMA ZA MADAWA

$
0
0
Kwa hili la Madawa Mastaa wengi bongo watakosa usingizi!! Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuanika majina ya wasanii pamoja na askari polisi wanaotuhumiwa kujihusisha na mtandao wa biashara haramu ya dawa za kulevya.


Ukiachilia mbali akina Wema SepetuChid BenzTID na wengine aliowataja juzi, jana Ijumaa, Makonda alilitaja jina la Tunda pamoja na Vanesa Mdee kuwa wamo kwenye orodha ya wasanii wanatuhumiwa kujihusisha na biashara hiyo na wanatakiwa kuripoti kituoni.
16230519_237402506710458_3127596812739805184_n
Tunda
Kwa kuwa mkuu wa mkoa hakutumia majina halisi ya kuzaliwa ya wasanii hao, taarifa zilianza kusambaa mitandaoni wengine wakisema kuwa aliyetajwa ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tunda Man huku wengine wakimpigia simu kumuulizia kuhusu ukweli wa skendo hiyo.
Baada ya kuona simu zinazidi kumiminika, Tunda Man aliamua kufunguka kupitia Instagram kwamba sio yeye aliyetajwa bali aliyetajwa ndio huyo kwenye picha, akaambatanisha na picha ya Mrembo Tunda ambaye ameonekana kama video queen kwenye video nyingi za bongo fleva.
Ujumbe huo ulisomeka hivi.. “Jamani Tunda aliyetajwa na Muheshimiwa @PaulMakonda ni huyu na sio mie maana simu zimekua nyingi, @Sudibrown na wewe hujui au umeamua kunipigia tu….”

PEDESHEE JACK PEMBA AFANYA BIRTHDAY PARTY YA KUFURU HUKO KONGO

$
0
0

Mfanyabiashara maarufu nchini aliyehamishia makazi yake nchini Uganda, Pedeshee Jack Pemba, jana alifanya birthday ya kufuru nchini Uganda, huku mwanamuziki mahiri kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide akiwa ndiye mgeni rasmi.

Vipande vya video zilizosambaa mtandaoni, vinamuonesha Koffi akipafomu live wimbo wa Ekotite (Selfie) akiwa na bendi yake, ambapo Jack Pemba anamtunuku noti kibao za dola miamia, na kushangiliwa na ukumbi mzima.

Kabla ya kufanyika kwa birthday hiyo, awali video ya Koffi aliyojirekodi akiizungumzia birthday hiyo na kuahidi kwamba atakuwepo nchini Uganda, ilikuwa gumzo kubwa mitandaoni na tukio la jana limewaacha wengi midomo wazi kwani si rahisi kwa msanii kama Koffi, kukubali kwenda kupafomu kwenye birthday na hata akikubali, dau lake huwa si la mchezo.

DK.SHEIN AWAANDALIA CHAKULA MAASKARI WALIOSHIRIKI GWARIDE LA MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA MAPINDUZI.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwapungia mkono maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakati alipowasili katika hafla ya chakula maalum kwa Askari hao iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni (kulia) Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman ,Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali wakisimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mara baada ya kuwasili katika hafla hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta jambo na Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman wakati wa hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mara baada ya kuwasili katika hafla hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, (wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir,(kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid na Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman (wa pili kulia) wakiwa katika hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akichukua chakula wakati wa hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, (wa pili kushoto) na Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman (wa pili kulia) wakichukua chakula katika hafla maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni.
Maaskari wa vikozi vya ulinzi walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar
/Maaskari wa vikozi vya ulinzi walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman,Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar baada ya hafla ya Chakula maalum aliyoiandaa kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,Sherehe iliyofanyika leo katika kambi ya KVZ Mtoni Mkoa wa Magharibi Unguja.
PICHA NA IKULU

NDUGU WAGOMEA MAITI YA MTOTO HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Shangazi yake Julieth, Judith Christopher akielezea tukio hilo kwa mwanahabari.
Julieth Daud (kulia) akiwa na dada yake nje ya wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo.
Julieth (aliyekaa kushoto), akiwa na ndugu zake nje ya wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo.
Mama mzazi wa Julieth, Veronica Lucas akiwa ameshika shavu kwa masikitiko kufuatia tukio hilo.
Mzazi Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini, akiwa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, alipozungumza na mwanahabari akidai amebadilishiwa mtoto aliyejifungua.




Na Dotto Mwaibale


MZAZI Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake wamegoma kuchukua mwili wa mtoto kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake kutokana na kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kujifungua.


Akizungumza kwa masikitiko nje ya viwanja vya hospitali hiyo Dar es Salaam jana, Daudi alisema kitendo alichofanyiwa kimemuumiza sana pamoja na ndugu zake wengine.


Alisema alifika Hospitalini hapo Februari 2 jioni akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica Lucas na shangazi yake Judith Christopher.


"Nilipofika daktari aliponipima aliniambia kuwa hasikii mapigo ya mtoto isipokuwa ya kwangu hivyo alishauri siku iliyofuata nipate kipimo cha utrasaund lakini kabla ya kipimo hicho nilijisia uchungu na kujifungua" alisema Daudi.


Daudi alisema baada ya kupita muda kidogo muuguzi aliyemzalisha alimfuata na kumueleza kuwa mtoto wake alikuwa amefariki na alipomuuliza alikuwa wa jinsia gani muuguzi huyo alimweleza kuwa alikuwa hajui kama alikuwa wa kiume au wa kike.


Aliongeza kuwa wakati yupo wodini alimuona kijana mmoja aliyevalia koti la hospitali akiwa amembeba mtoto ambaye hakujua alikokuwa amempeleka.


Alisema baada ya kuambiwa mtoto wake amefariki aliomba aonyeshwe lakini hakuoneshwa ambapo alilazimika kwenda kuomba simu kwa mlinzi wa hospitali hiyo na kuwajulisha ndugu zake walipofika nao waliomba kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo bila mafanikio.


Shangazi wa Julieth Judith Christopher alisema baada ya kutokea tukio hilo walikwenda kumuona Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye aliitisha kikao baina ya ndugu pamoja na maofisa wengine wa hospitali hiyo ambacho hakikufikia muafaka baada ya ndugu hao kukataa kuuchukua mwili wa mtoto huyo wakidai si wa kwao.


Aliongeza kuwa mganga mkuu huyo aliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa amefia tumboni baada ya mama yake kuiharibu mimba hiyo kwa nia ya kuitoa na ndiyo sababu mtoto huyo alizaliwa akiwa mfu.


"Wanafamilia tumegoma kuuchukua mwili wa mtoto huyo na maamuzi yaliyofikiwa ni kufanyika kipimo cha DNN na ili mama wa mtoto aruhusiwe kutoka hospitali inatakiwa ipelekwe barua ya mwenyekiti wa mtaa wake anakoishi" alisema Christopher.


Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Beauty Mwambebule alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo hakuwa tayari kuzungumza kwa njia ya simu badala yake alimtaka mwandishi wetu kwenda hospitali kupata undani wa jambo hilo.
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>