Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live

KAIMU MKURUGEZI MTENDAJI WA TANESCO, DKT.TITO MWINUKA AKAGUA VITUO VYA KUPOZA UMEME VYA WILAYA YA TEMEKE NA KARIAKOO

$
0
0
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt.Tito E. Mwinuka, (pichani kushoto), amefanya ziara ya kutembelea vituo vitatu vya kupoza na kusambaza umeme wa msongo wa Kilovoti 132, (132Kv), vya Mbagala, Kurasini Wilayani Temeke na Kariakoo Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari 4, 2016 na kuwaomba wateja wa Shirika hilo kuwa wavumilivu wakati juhudi za kukamilisha mradi wa uboreshaji umeme ukiwa unakaribia kukamilika.
Dkt. Mwinuka alisema, ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi katika maeneo ya Mbagala, Kigamboni na Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, kumepelekea upatikanaji wa umeme kwenye maeneo hayo kuwa na matatizo kidogo kwani vituo vinavyosambaza umeme kwenye maeneo hayo vilikuwa na ukubwa wa kupoza umeme wa Kilovoti 33 tu, na ndio maana TANESCO kupitia Mradi wa uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam unakaribia kukamilisha ujenzi wa vituo vilivyotajwa hapo juu ili view na uwezo mkubwa wa Kilovoti 132 na hivyo kuondoa kabisa tatizo hilo.
“Barabra zinapozidiwa na magari ni rahisi sana kubaini kutokana na ongezeko la magari yanayotumia barabara hizo, lakini ongezeko la watumiaji umeme na shughuli za kiuchumi inakuwa vigumu kubaini kwa haraka, kwa hivyo niwaombe wateja wetu kuwa wavumilivu kwani tatizo hilo litakuwa limepatiwa ufumbuzi katika kipindi kifupi kijacho.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Dkt. Mwinuka pia aibainisha, kuwa kazi ya kuongeza ukubwa wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme inaendelea kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi ambako nako vituo vya sasa vya ukubwa wa Kilovoti 33, vinabadilishwa na kuwa na uwezo wa Kilovolti 132.
Dkt. Mwinuka amewapongeza wakandarasi kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa haraka ili kuwaondolea adha wateja wa Shirika hilo wa upatikanaji wa umeme ulio bora na wa uhakika.

Dkt. Mwinuka (kulia), akipatiwa maelezo ya litaalamu na Mkuu wa miradi (anayeshughulikia usafirishaji) wa TANESCO, Mhandisi Frank Mashalo, alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Februari 4, 2017. Wakwanza kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.
Mitambo ya kupoza na kusafirisha umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, kikiwa katika hatua za mwisho ukamilika
Dkt. Mwinuka, (wapili kulia), akimsikiliza mkandarasi kutoka kampuni ya FICHTNER, ambaye ndiyo Menenja mradi, Mathias Alby, wakati alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula Maendeleo, (kushoto), akitoa maelezo ya kiutendaji kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Tito E.Mwinuka, wakati wa ziara yake ya kutembelea vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Mbagala na Kurasini vilivyoko Wilayani Temeka. Katikati ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya.
Dkt. Mwinuka (mbele), baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Kurasini jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mwinuka, (wapili kulia) akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia miradi ya usafirishaji na usambazaji umeme, Mhandisi Gregory Chegere, (kushoto), wakati alipotembelea kituo cha Kurasini. Kulia ni 
Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya.
Muhandisi mwandamizi wa miradi wa TANESCO, Mhandisi Rosmystice Luteganya, (kushoto), akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka, kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mwinuka, (kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Fundi akiwa kazini kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo
Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya, (aliyesimama), akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara hiyo, kwenye chuo cha TANESCO jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Dkt. Mwinuka, Mhandisi Chegere na Mhandisi Mashalo.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumza wakati wa kikao hicho.
Jengo la kituo cha bkupoza na kusambaza umeme wa msongo wa Kilovolti 132 cha Mbagala jijini Dar es Salaam, likiwa limekamilika
Meneja wa TANESCO Wilayani Temeke, Mhandisi, Jahulula Maendeleo, (kulia), akizungumza na maafisa wa TANESCO wakati wakimsibiri Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Rito E. Mwinuka kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala jijini Dar es Salaam.

SUPER STAR WEMA SEPETU ATOA KAULI NZITO,AFUNGUKA MAZITO KWA MASHABIKI WAKE

$
0
0
 Mwigizaji wa Tanzania Wema Sepetu ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alifika kwenye kituo kikuu cha Polisi kati Dar es salaam baada ya kutajwa kwenye orodha ya wanaotuhumiwa kufanya biashara ya dawa za kulevya, amewatoa hofu Mashabiki zake.
 

KATIBU MKUU WA CCM KINANAAZIDI KUCHAPA KAZI

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Dodoma mjini na mkoa huo, katika Ofisi ya CCM mkoa wa Dodoma, leo alipowasili kwenye ofisi hiyo, tayari kushiriki na kukagua shughuli za maendeleo ikiwa ni sehemu ya Madhimisho ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni kesho. Akizungumza Kinana amesema, CCM imeamua kufanya Maadhimisho hayo mkoani Dodoma kwa kuwa imedhamiriwa kuisaidia Serikali katika kutekeleza ilani ya CCM, hivyo CCM imeamua kufanya hivyo ili kuunga mkono azma ya Serikali kuhamia Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana akitoa salamu za shukrani, baada ya Kinana kuzungumza katika mkutano huo wa ndani. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Adam Kimbisa.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwasalimia mafundi alipowasili kukagua na kupanda miti kwenye mradi wa Ujenzi wa Dampo la Kisasa katika eneo la Kata ya Matumbulu wilaya ya Dodoma Mjini, leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni kesho.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipanda miti kwenye mradi wa Ujenzi wa Dampo la Kisasa katika eneo la Kata ya Matumbulu wilaya ya Dodoma Mjini, leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni kesho.

Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Dodoma Mjini, akishiriki kupanda mji kwenye mradi huo

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christina Mndeme akishiriki kupanda mti kwenye eneo la mradi huo

Mbunge wa Dodoma Mjini, Waziri Anthony Mavunde akishiriki kupanda mti katika eneo hilo

Kinana akimpongeza kwa kupanda mti katika eneo hilo, Mzee Godfrey James

Kinana akimsaidia kupanda mti mjumbe wa shina katika kata hiyo Ester Paschal

Kinana na ujumbe wake wakiondoka katika upandaji mti na kwenda kukagua ujenzi wa dampo la kisasa katika eneo hilo. Kushoto ni Mavunde na kulia ni Kimbisa

Mhandisi wa Manispaa ya Dodoma, Injinia John Nchilla akimpa Kinana maelezo kuhusu ujenzi wa dampo hilo la Kisasa katika Kata ya Matumbulu wilaya ya Dodoma Mjini

Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Nkuhungu, Dodoma Mjini, Pius Afa akimkaribisha Kinana kushiriki ujnezi na kupanda mti kwenye ujenzi wa Ofisi ya CCM ya Kata hiyo

Wanachi wakimpokea Kinana kwa shamrashamra alipowasili katika Kata hiyo ya Nkuhungu

Kinana akisalimia wananchi wa Nkuhungu

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Nkuhungu Pius Afa akimuonyesha Kinana ramani ya ujenzi wa Ofisi hiyo ya CCM ya Kata hiyo

Kinana akipokea tofali alipokuwa akishiriki ujenzi wa Ofisi hiyo ya CCM Kata ya Nkuhungu

Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Nkuhungu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40ya CCM ambayo kilele chake ni kesho

Kinana akishuka baada ya kushiriki ujenzi wa Ofisi hiyo kikamilifu

Kinana akizungumza na wananchi baada ya kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Mkuhungu, Dodoma leo. Picha zaidi alipotembelea Kijiji cha 

MUME WA KAJALA MASANJA ATOKA JELA,MENGI MAZITO YAFICHUKA UJIO WAKE BAADA YA KUTOKA JELA

$
0
0
  
 HAKILA kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho wake, hatimaye mume wa ndoa wa nyota wa filamu Bongo, Kajala Masanja, Faraji Agustino yuko huru akidunda mtaani baada ya kutoka jela katika Magereza ya Keko jijini Dar na kusema ole wao waliokuwa wakichepuka na mkewe, Amani limenyetishwaKwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka karibu na familia ya Faraji, alitoka jela siku kumi zilizopita baada ya kushinda rufaa ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya kudaiwa kutakatisha fedha haramu na kuuza nyumba iliyokuwa kwenye zuio.


MAMA ALIYEJITOSA KWA JPM ATILIWA SHAKA

$
0
0
TAHARUKI iliyojitokeza juzi mbele ya Rais John Magufuli, kwa mkazi wa Tanga, Swabaha Shosi kudai kudhulumiwa mirathi ya mumewe, imeibua sintofahamu mpya baada ya waliojiita familia ya huyo mume, kujitokeza na kutangaza kutomtambua Swabaha.Akizungumza jana Tanga na mwandishi , mwanafamilia aliyejitambulisha kuwa mtoto katika familia hiyo, Saburia Mohamed (37), alidai mara ya kwanza kumwona Swabaha, ilikuwa siku ya kumaliza msiba wa baba yake.Juzi katika kilele cha Siku ya Sheria, Swabaha huku akilia mbele ya Rais Magufuli na uongozi wa juu wa Mahakama na Polisi, alidai kunyimwa haki ya mirathi ya mumewe na vyombo vya kutoa haki nchini.Swabaha ambaye alifanikiwa kugonga vichwa vya habari juzi na jana, alitaja vyombo vilivyomnyima haki kuwa ni Polisi, Mahakama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Lakini jana Saburia, aliyejitambulisha kwa mwandishi wa gazeti hili kama mwanafamilia, alidai kutomtambua na kueleza kuwa siku ya kwanza kumwona, ilikuwa ya kumaliza msiba wa baba yao.

Saburia alidai kuwa siku hiyo Swabaha alitambulishwa kama binamu yao kwa shangazi yao aliyeko Mombasa na alikuwa akitoka eda Dar es Salaam baada ya kufiwa na mumewe.  

"Yule mama sisi kwa mara ya kwanza tulitambulishwa siku ya kumaliza msiba wa baba yetu tukiwa kwenye kikao cha familia, alifika saa sita mchana, tukaambiwa kuwa ni mjomba wa marehemu baba na ametoka eda Dar es Salaam ya aliyekuwa mumewe naye alithibitisha hilo," alidai.

Hata hivyo, Saburia alidai kuwa wakili wa familia alipokuwa akisoma wosia wa marehemu, Swabaha alimnyang'anya wosia huo na kukimbia nao baada ya kuona jina lake halimo.

Mtoto huyo alidai kuwa mwaka 2012 ilifunguliwa kesi ambayo ilimalizika kwa kufutwa Desemba 15, mwaka juzi na mwaka huo huo familia ilipeleka maombi Mahakama ya Mwanzo, kumpendekeza Saburia awe msimamizi wa mirathi.

Alidai kabla ya kupewa usimamizi, Swabaha alijitokeza mahakamani na kupinga kwa madai kuwa anayependekezwa kusimamia mirathi hiyo si mtoto halali wa marehemu.

Saburia alidai kuwa mama huyo hakuwa sahihi kupeleka taarifa kwa Rais, kwani kesi yao bado inaendelea Mahakama Kuu, ambako inasikilizwa na Jaji Amour Said Khamis na bado hukumu haijatolewa.

Alidai kuwa yeye na familia yake hawana vitisho vyovyote kwa mama huyo na familia ilipatwa na butwaa aliposema anahitaji ulinzi kwa kuwa anatishwa.

Mtoto huyo alielezea masikitiko yake kuwa ameumia baada ya Swabaha kumtangaza mbele ya Rais kuwa anahusika na uuzaji wa dawa za kulevya, kitu ambacho si kweli na kwamba yuko tayari kufanyiwa uchunguzi wa jambo hilo.

"Mimi ni mfanyabiashara wa nguo na nina duka langu la nguo barabara ya 14, ameniumiza sana pamoja na familia yangu kwa kusema nauza dawa za kulevya. Naomba Serikali iliangalie hili, kwani niko tayari kufanyiwa uchunguzi wa tuhuma hizi," alidai.

Mbali na Saburia, mwandishi wa habari hii alizungumza na aliyetambulishwa kuwa mke mkubwa katika familia hiyo, Mariam Juma ambaye alidai kuwa hamfahamu Swabaha.

"Mimi ninamfahamu mama yake ambaye ni wifi yangu na anaishi Mombasa, yeye sijawahi kumwona. Sasa nilishangaa kubadilika na kusema kuwa ni mke wa marehemu na kudai ananyanyasika kwa kudhulumiwa mirathi," alisema Mariam.

Aliitaka Serikali iingilie kati suala hilo ili wapate haki zao yeye na familia yake, ambayo ina watoto tisa na wake wawili.

Juzi Rais Magufuli aliwaagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashitaka, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na Mahakama kupitia Jaji Kiongozi, kushughulikia jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuhamishia kesi hiyo Mahakama ya Juu ili uamuzi ufanyike.

KAULI YA MENEJA WA DIAMOND PLATINUMS BAADA YA TAARIFA YA DIAMOND KUUNGANISHWA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

$
0
0

Diamond Platnumz Mapema Jioni ya Jumamosi ya Tarehe 4, 2017. Ilisambaa taarifa inayoanisha Majina Kadhaa ya watu maarufu hapa Bongo ikisema kuwa ni miongoni mwa watu waliotakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi jijini dar siku ya Jumatatu kufanya mazungumzo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul makonda na Jeshi la Polisi kuhusiana na Sakata la uuzaji na Utumiaji wa Madawa ya Kulevya nchini.


Katika majina hayo yaliyotolewa na Taarifa hiyo ambayo haikuonesha nani mtoaji wa taarifa hiyo bali ikionyesha Anuani tu ya Jeshi la Polisi nakuleta walakini wa taarifa hiyo ni Jina la Msanii Maarufu na Mwenye ushawishi mkubwa kwa sasa nchini Tanzania Diamond Platnumz ambapo kwenye taarifa hiyo ameandikwa kwa jina la Nasibu Abdul.
Taarifa
Taarifa iliyo Sambaa Mtandaoni
Meneja wa Msanii huyo Babu Tale ameona sio sawa kukaa kimya na ameweza kujibu kwa ufipi sana na kusema kuwa "No Information, No right to speak!!! Marry you - link on my bio". Amepost kupitia mtandao wa Picha wa Instagram.


PROF.LIPUMBA ADAI HANA UKARIBU NA SERIKALI

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amekanusha tuhuma za kuwa na ukaribu unaotia shaka kati yake na serikali na kutolea ufafanuzi ishu mbalimbali zinazoashiria ukaribu huo ikiwemo ya kuchepusha ruzuku ya chama.

Mwenyekiti huyo anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa amesema kinachodaiwa kuwa ni ukaribu wake na serikali, siyo sahihi kwa kuwa yeye huwa anaalikwa tu kwenye matukio mbalimbali ya kitaifa ambayo hawezi kukataa mwaliko.
"Kwa mfano ukikaribishwa kwenye shughuli ya serikai, labda Rais anazindua kitu, au sherehe za kitaifa na Rais yupo utakataaje" Amesema Lipumba.

RUZUKU
Suala la ruzuku ya chama hicho kuchepushwa pia ni jambo linalodaiwa kuwa ushahdi wa Prof Lipumba kuwa karibu zaidi na serikali, ambapo amesema ilikuwa ni lazima iwe hivyo kutokana na uamuzi wake kama Mwenyekiti wa chama wa kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Fedha, ambaye ndiye aliyekuwa mtia sahihi katika masuala ya fedha.
Pia sababu nyingine ya kuchepusha fedha za ruzuku amesema ni mahitaji ya chama kwa kuwa kilikuwa kinaingia kwenye uchaguzi hivyo kilihitaji fedha kwa ajili ya shighuli mbalimbali.
" Kuhusu ruzuku, nilikuwa nimetengua uteuzi wa mkurugenzi wa fedha, bwana Bashange, kwahiyo hakuwa tena signatory wetu, kwa nafasi yangu kama mwenyekiti niliona hafai, tukajitahidi kufungua akaunti nyingine lakini haikuwezekana. Ikabidi Naibu Katibu Mkuu ambaye ndiye anayeshika nafasi ya Katibu Mkuu anapokuwa hayupo ofisini, aandike barua ya kuomba ruzuku kwa ajili ya mahitaji tuliyokuwa nayo" Ameeleza Lipumba 
Lipumba ameendelea kusema "Tukapeleka taarifa kuomba ruzuku. Kwahiyo Naibu Katibu Mkuu akaandika barua kwenda kwa Msajili kuwa tunaomba ruzuku na ipitie kwenye akaunti nyingine, na hilo likafanyika" 
Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa

MIKUTANO
Kuhusu yeye kuruhusiwa kufanya ikutano, huku Katibu Mkuu wake akizuiliwa, hususani tukio lililotokea mkoani Mtwara, Lipumba amesema hata yeye alipokwenda Mtwara hakuruhusiwa kufanya kilichokuwa kimempeleka, na badala yake aliishia kufanya mikutano ya ndani, huku akibainisha kuwa kilichomkwamisha Maalim Seif ni kwenda bila kutoa taarifa kwa kiongozi wa wilaya.
"Nimekwenda Mtwara, nilikaribishwa na viiongozi wa wilaya, kazi yangu ilikuwa ni kufungua matawi, lakini polisi wakanizuia kuwa sitakiwi kufanya mikutano ya nje, nikafanya mikutano ya ndani...Lakini Maalim Seif alikwenda bila kumtaarifu kiongozi wa wilaya". Amesema

ULINZI
Lipumba aliyekuwa katika mahojiano na kituo kimoja cha TV, amekanusha taarifa za kupewa ulinzi na serikali na kufafanua tukio la kupigiwa saluti na askari, akisema kuwa siku hiyo hakupigiwa yeye saluti bali diwani wa eneo ambalo yeye alishiriki kufanya usafi.
"Pale Buguruni, tulikuwa katika usafi, na tulikuwa na diwani wa eneo lile, askari walikuwa wakiangalia usalama, na alipotokea diwani wa eneo lile, askari walimpigia yeye kwa kuwa ndiye mkuu wa eneo lile, siyo mimi"
Kitendo kilichodaiwa kuwa ni askari kumpigia saluti Prof Lipumba
Katika hatua nyingine, amesema anaendelea kumtambua Maalim Seif kama Katibu Mkuu halali wa CUF,  huku akimtaka amfuate ili wamalize tofauti zao na kufanya kazi kwa pamoja

KAJALA ASHAMBULIWA KWA KUTOMPELEKEA CHAKULA WEMA RUMANDE


HUYU HAPA KOPI YA HEMEDYPHD ‘HEMEDYRAPA

$
0
0
Ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa Harmorapa ameteka vichwa vya habari kuliko hata Harmonize ambaye ndiye mtu ambaye wamekuwa wakifananishwa naye.

Tunaweza kusema Harmorapa katumia Advantage ya kufanana na Harmonize ili na yeye ajulikane na kufanya kazi zake za kimuziki kiurahisi.
Anyway!! Tuachane na ishu za Harmorapa leo tena nimepata bahati ya kukutana na Kopi ya Hemedy PHD  na ishu kubwa ni kwamba jamaa kafanana nae kinoma na huyo jamaa Hemedyrapa,  na ivyoonesha ni mtu ambae anafahamiana na Hemedy. Anajulikana kwa jina la DJ Mario.
16110755_1070662323056757_2860319185433526272_n
DJ Mario & Hemedy PHD
Nimekuwa nikijiuliza!! hivi kuna umuhimu wa kutumia Advantage ya kufanana na Star fulani ili kukuza jina lako (Branding) hususani kwa wale wanao jihusisha na Sanaa au Michezo?
16122585_665949163578652_4081260542373658624_n
16123816_587023208174369_1282426803079610368_n

16464821_161517694347512_2263731052444909568_n

16123888_1237972666297231_7801474850966470656_n


RAIS MAGUFULI AHIMIZA UMOJA NDANI YA CCM

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho chama tawala nchini Tanzania, leo Februari 5, mwaka 2017 kinaadhimisha miaka 40 ya kuzaliwa kwake, ambapo Mwenyekiti wake Dkt. John Magufuli amesisitiza umoja ndani ya chama hicho.

Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yamefanyika kwa mtindo tofauti, ambapo badala ya kufanyika kwa mkutano mkubwa wa chama na sherehe kama ilivyozoeleka, wanachama wa chama hicho wameshiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali waliyoko, pamoja na kutembelea wagonjwa hospitalini.
Taarifa iliyotolewa jana na chama hicho, ilieleza kuwa kwa mwaka huu chama hicho kinataka kuwathibitishia watanzania kuwa ni cha wachapakazi na pia kipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
"Hakutakuwa na mikutano ya hadhara wala sherehe za maadhimisho kama ilivyo desturi. Tutafanya shughuli za kijamii na mikutano ya ndani. Msingi wa mijadala hii ni kuandaa MWONGOZO wa CCM mwaka 2017 ambao utakuwa na tafakuri za wanachama juu ya aina ya Chama wanachokitaka. Kwa kuwa MSINGI wa kuundwa kwa CCM ni kuwasemea na kuwatumikia watu, tunatoa wito kwa wanachama kuadhimisha kwa kufanya shughuli za kijamii". Ilisema sehemu ya taarifa hiyo
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho taifa ambaye pia ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewapongeza wanachama wote wa CCM, ikiwa ni pamoja na kuwasisitiza kuwa na umoja kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.
"Nawapongeza wanachama wa CCM wote na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi katika kutimiza miaka 40 ya CCM. Tuendelee kushikamana, kukijenga chama kwa kuisimamia Serikali katika kuleta maendeleo kwa Watanzania" Amesema Rais Magufuli

AFANDE SELE AFUNGUKA MENGINE KUHUSU MADAWA YA KULEVYA NA WCB

$
0
0

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutaja majina ya kadhaa ya wasanii na polisi mbalimbali ambao wanajihusisha huku wengine wakituhumiwa na matumizi na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Afande Sele amefunguka na kusema kama jambo hili litafanywa kwa haki na umakini basi huenda hata wale wasafi wakaonekana  ni wachafu.

Afande Sele ameonyesha wasiwasi juu ya sakata hili la madawa ya kulevya ila amesisitiza kuwa kama kweli litafanyikwa kazi kwa umakini mkubwa basi kuna kundi kubwa la watu ambao wanaonekana ni wasafi kuchafuka kutokana na sakata hili.


"Katika hili sakata la MAPAPA na MAPUNDA ya unga kama kweli braza Paul yupo 'serious' na sio 'Matango Pori'kama tulivyoona katika masakata mengine, huenda hata wale WASAFI wakaonekana wachafu...kila la kheri Mr Paul....RiP dada Amina...wacha party ianzeee" aliandika Afande Sele 
Kauli hii ya Afande Sele imekuwa ni kauli tata na imeibuka mjadala kwa baadhi ya mashabiki katika kuitafsiri wengine wakisema Afande Sele amezungumzia wasanii ambao wapo chini ya label ya WCB Wasafi chini ya Diamond Platnumz huku wengine wakisema amezungumzia watu ambao wanaonekana ni wema katika jamiii kumbe si wema bali ni wachafu kwa matendo yao kwa kujihusisha na biashara za dawa za kulevya.

HII NDIO LIST YA ASKALI WALIOSIMAMISWA KAZI BAADA YA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi askari 12 waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya wakati uchunguzi ukiendelea.

IGP huyo amewaambia wanahabari, Jumamosi hii katika makao makuu ya Polisi huku akisema kuwa Polisi ndiyo chombo kinachoongoza mapambano juu ya madawa hayo, huku akisema kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya askari atakayetuhumiwa.

“Tumeamua kuwasimamisha kazi wote walioguswa moja kwa moja na sakata hili, pia Polisi itachukua hatua madhubuti ikiwemo kuwapeleka mahakamani wasanii waliotuhumiwa,” alisema.

Askari hao ni wale waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda siku mbili zilizopita wakati akiwaambia wanahabari juu ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara na matumizi ya madawa hayo.


STAA WEMA SEPETU AWATOA HOFU MASHABIKI WAKE

$
0
0

Mwigizaji wa Tanzania Wema Sepetu ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alifika kwenye kituo kikuu cha Polisi kati Dar es salaam baada ya kutajwa kwenye orodha ya wanaotuhumiwa kufanya  biashara ya dawa za kulevya, amewatoa hofu Mashabiki zake.

Wema amesikika kwenye sauti aliyoiweka kwenye mitandao akisema: 'Nadhani natakiwa kusema kitu sababu najua nina mashabiki, nina watu wananipenda na kunifatilia…. nina watu wanani-support, nina watu wana hofu kuhusu mimi.


"Nina watu ambao wananijali sana na nina uhakika yani wana wasiwasi sana lakini nataka tu niwaambia kwamba msiwe na wasiwasi"


Msikilize hapo chini 


RAIS DONALD TRUMP APATA PIGO HILI

$
0
0

Jaji mmoja wa Marekani amesimamisha kwa muda utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia kutoka mataifa saba, yaliyo na raia wengi wa imani ya Kiislamu kuingia nchini Marekani.

Jaji wa Seattle alipuuzilia mbali sababu zilizotolewa na mawakili wa Serikali na kusema kuwa amri hiyo inaweza kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa mahakamani.

Serikali inatarajiwa kukata rufaa ya dharura dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, ambao ni changa moto kubwa kwa utawala wa Trump.

Serikali ya Marekani inasema kuwa makumi ya maelfu ya visa zimefutiliwa mbali tangu rais Trump kutia sahihi amri ya kupunguza idadi ya watu wanaopaswa kuingia nchini Marekani juma lililopita.

Kutokana na hatua hiyo, Idara ya Forodha ya Marekani imeyaambia mashirika ya ndege kwamba waruhusu abiria kupanda ndege kuelekea Marekani abiria ambao walinyimwa ruhusa baada ya Rais Trump kutoa amri kwamba watu kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi, wakataliwe kuingia Marekani.

Wakati huohuo waziri Mkuu wa zamani wa Norway, Kjell Magne Bondovik, alisema kuwa alizuiwa katika uwanja mmoja wa ndege mapema juma hili, katika tukio alilosema ni la uchokozi, kwa sababu eti alikuwa na visa ya Iran katika paspoti yake.

HII NDIO KAULI YA VANESSA MDEE BAADA YA KUTAJWA NA RC PAUL MAKONDA

$
0
0
Iliwashangaza wengi baada ya Vanessa Mdee naye kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya mastaa wanaohusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.
Ni shutuma nzito, na hata kabla uthibitisho rasmi haujatoka, madhara ya kutajwa majina yao yameanza kuonekana katika maisha yao
Wito huo umemkutia Vee Money akiwa nchini Afrika Kusini anakoshoot tamthilia ya MTV Shuga, na bila shaka atalazimika kukatisha kwa muda na kurudi Tanzania kwenda kituo cha polisi central, anakotakiwa Jumatatu ya kesho.
Pamoja na hivyo, Vee ameonesha kuvuta pumzi ndefu na kuacha maisha yaendelee kama yalivyo. Kupitia Instagram, Vee amepost picha hizo juu na katika ile aliyokaa ameandika: The show must go on … bomb ass dress from @asos #FILA.
Kwenye hiyo black and white ameandika: The night is darkest before the dawn. #Breakthrough #Juu #CashMadame #SheKing.”
Kwenye picha hizo amezima comments ili kuepuka maneno ya kejeli kutoka kwa baadhi ya watu ambao tayari wamefanya hivyo kwenye picha zingine. Vee anaungana na mastaa wengine wakubwa wakiwemo Wema Sepetu, Mr Blue, TID na wengine kwenye orodha hiyo.

KAMPUNI YA MO DEWJI LAMADA HOTEL NI MDAIWA SUGU WA KODI

$
0
0

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza oparesheni maalumu ya kukusanya Kodi ya Pango la Ardhi kutoka kwa wadaiwa sugu wa Makampuni, mashirika ya kiserikali na watu binafsi kwa kuwafuata katika maeneo yao.

Katika hatua ya kwanza Wizara kwa kushirikiana na Manispaa za  mkoa wa Dar es salaam imetoa notisi kwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la Ardhi wakiwemo Mohammed Enterprises anaedaiwa Shilingi milioni 73, Lamada  Hotel anaedaiwa Shilingi milioni 54, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) anaedaiwa Shilingi milioni 144 na Tanganyika Motors anaedaiwa Shilingi milioni 22.

Makampuni hayo yamepewa notisi ya siku 14 ili kulipa kodi hizo wanazodaiwa na endapo hawatalipa watafutiwa umiliki au mali zao kwa kupigwa mnada ili kufidia gharama wanazo daiwa.

Serikali kwa kutumia kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment imeendesha oparesheni hiyo kwa kufika katika ofisi za wamiliki wa viwanja na mashamba makubwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Akiongea kwa kusisitiza, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila amesema katika mwaka wa fedha 2016/17 Wizara imepanga kukusanya Sh. bilioni 111.77 kutokana na Kodi ya Pango la Ardhi.

Wizara haitaweza kufanikisha malengo hayo endapo itaendelea kuwaachia wadaiwa sugu ambao hawataki kulipa kodi. Kwani kwa miaka mingi sasa mapato mengi ya serikali yamekuwa yakiachwa kutokana na kushindwa kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi Kayandabila alisisitiza.

TAZAMA SHOW YA STAA ALI KIBA ALIYIPIGA HUKO DODOMA

$
0
0
Mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba usiku wa February 4 2017 alikuwa makao makuu ya nchi Dodoma kwa ajili ya kutoa burudani kwa Watu wake huku akisindikizwa na mdogo wake AbduKiba pamoja na band yake ya live…. Hii video hapa chini ina tukio zima: 

WAZIRI NAPE AINGILIA KATI SAKATA LA UNGA

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameingilia kati na kutaka busara itumike katika zoezi la kutaja wasanii wanaohusika na dawa za kulevya linalofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Nape ametoa ushauri huo leo Mjini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari kuhusu sheria mpya wa huduma za habari, ikiwa ni siku nne tangu mkuu huyo wa mkoa aanze kutaja wahusika wa dawa za kulevya wakiwemo wasanii wa bongo fleva na filamu.
Baadhi ya waliotajwa na kutakiwa kuripoti polisi kwa mahojiano ni pamoja na Vanessa Mdee, Wema Sepetu, Nyandu Toz, Chidi Benz, TID, Tunda, Babuu wa Kitaa n.k
Wema Sepetu (Kushoto) alipokuwa akiwasili katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa agizo la Paul Makonda

Nape baada ya kuulizwa swali na wanahabari kuhusu suala hilo amesema kuwa wizara yake inakiri kuwa tatizo hilo ni kubwa, na ilifikia hatua ya kuwasaidia baadhi ya wasanii kwenda kupata matibabu akiwemo msanii Ray C na kwamba wanaunga mkono jitihada zozote za kupambana na tatizo hilo.
Amesema tatizo lipo kwenye namna ya kuwaadhibu wanaogundulika kutumia dawa za kulevya, kwa maana ya sheria ipi itumike kuwashitaki, lakini pia tatizo lingine ni busara inayotumika kuwataja na kuwakamata watu ambao tayari wamekwisha athirika na dawa kulevya badala ya kuwasaidia.
Waziri Nape Nnauye
Kwa mtazamo wake nape amesema hilo ni tatizo la jamii nzima, na kushauri jamii yote ya watanzania kushiriki katika kujenga maadili ya watoto.

SERIKALI YATANGAZA KIGEZO CHA UANDISHI WA HABARI

$
0
0
Serikali imetangaza kuwa kiwango cha chini cha taaluma anayopaswa kuwa nayo mwandishi wa habri kuwa ni 'Diploma ya Uandishi wa Habari' kwa mujibu wa kanuni za sheria mpya ya hunda za habari zilizokamilika utungaji wake hivi karibuni.

Akizungumza na wana habari leo mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo , Nape Nnauye amesema kuwa kanuni zimeshaundwa na zimechapishwa kwenye gazeti la serikali tangu Februari 3 mwaka huu baada ya kupokea maoni ya wadau mbalimbali.
"Tumesoma, tumechambua maoni ya wengi, wapo waliotaka iwe cheti, wengine diploma, wengine digrii, wapo waliotaka PhD na wapo waliotaka iwe mtu yeyote nayejua tu kusoma na kuandika. Serikali imesimama katikati ya maoni hayo. Sifa ya chini kabisa kwa kuanzia itakuwa ni diploma ya uandishi wa habari” Amesema Nape
Waziri Nape amesema pia kuwa sheria hiyo imeshaanza kutumika tangu Desemba 31 mwaka 2016, ambapo yeye kama Waziri mwenye dhamana alishatoa tangazo katika gazeti la serikali.
Aidha kuhusu wasio na sifa hiyo, Waziri Nape amesema kuwa serikali imetoa kipindi cha mpito cha miaka mitano ili waandishi wasiokuwa na sifa hiyo, waliopo sasa na watakaoingia kwenye taaluma hiyo, wakasome ili wawe wamepata sifa hiyo.
Amesema katika utekelezaji wa sheria hiyo, kuna taasisi ambazo tayari zipo, zitaongezewa majukumu au kazi zake kuhuishwa, pia kuna vyombo vipya vitaanzishwa na kuna taratibu mpya za kiutendaji zitaandaliwa.
Kuhusu manufaa ya sheria hiyo, Nape amesema kuanza kutumika kwa sheria hiyo ni jambo muhimu kwa tasnia hiyo kwa kuwa ni ruhusa ya kuanza kwa mchakato wa kuifanya taaluma ya habari kuwa taaluma kamili yenye sifa mahsusi na  maadili yaliyokamilika pamoja na kuwa na vyombo vya kusaidia utekelezaji wake.
Sheria hiyo ilisainiwa na Rais Magufuli Novemba 16 mwaka 2016, na siku mbili baadaye ilichapishwa kwenye gazeti la serikali baada ya muswada wake kupitishwa na Mkutano wa 5 wa bunge mwezi Novemba 2016.

MWANAMKE WA TANZANIA AKAMATWA NA COCAINE LEO HUKO CHINA

$
0
0

Thelma Mkandawire (38) raia wa Zambia and Pamela Devid Kiritta (41) raia wa Tanzania baada ya kukamatwa na kilo nne za cocaine leo nchini India.

Wanawake wawili wamekamatwa jana Jumamosi na kilo nne za cocaine nchini India. Wanawake hao wametajwa kama Pamela Devid Kiritta mwenye umri wa miaka 41 raia wa Tanzania na Thelma Mkandawire mwenye umri wa miaka 38 raia wa Zambia.

Wanawake hao wamekamatwa ndani ya hoteli moja iliyoko kusini mwa jiji la New Deilhi baada ya maafisa husika kutonywa kuwa walikuwa wanapeleka mzigo huo wa cocaine kwa mtu fulani. Mwanamke wa Zambia alisafiri na ndege ya kampuni moja ya Ulaya akitokea Addis Ababa. Maafisa hao walianza kumfuatilia mara tuu alipotua kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa IGI.

Baada ya kucheki out, Mzambia huyo alichukua teksi na kuondoka zake. Maafisa walimfuatilia mpaka kwenye hoteli moja iliyopo eneo la Mahipalpur ambapo partner wake Pamela alikuwa anasubiria mzigo. Wote wawili walikamatwa kabla ya kuondoka hotelini hapo. Ndani ya begi la Mzambia kulikuwa na mzigo wa kilo nne za cocaine ambazo zilikuwa zimefungwa kwa ustadi mkubwa sana kiasi kwamba machine za airport hazikuweza kugundua.

Alipohojiwa na maafisa hao, Pamela alisema alikuwa amepanga kwenye flat moja iliyoko Vasant Kunj tokea Januari 20 mwaka huu. Pamela amesema kuwa alikuwa anamfanyia kazi mwanaume mmoja wa Afrika ya Kusini. Pamela ameitembelea India mara tisa tokea mwaka 2006. Pia Pamela ameshatembelea nchini nyingine kama Ecuador, Afrika Ya Kusini na Kenya. Maafisa wa India wanahisi kuwa safari zake zinahusiana na biashara ya dawa za kulevya.

Kwa upande wa Mzambia (Thelma) alikamatwa Pakistani mwaka 2015 kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya. Pia ametemblea nchi za China na Hong Kong kwa biashara hiyo hiyo.
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>