↧
KING OF ALL BONGO SOCIAL MEDIAS ATUA DODOMA.
↧
RAIS DKT SHEIN AREJEA NCHINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) wakiagana na Mhe, Airlangga Hartarto ambae ni miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia katika uwanja wa Ndege wa Soekarno Hatta Mjini Jakarta Nchini Indonesia baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi IORA Nchini humo Dk.Shein alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na kuagana na Mhe, Airlangga Hartarto ambae ni miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia katika uwanja wa Ndege wa Soekarno Hatta Mjini Jakarta Nchini Indonesia baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi IORA Nchini humo akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) wakizungumza na kuagana na Mhe, Airlangga Hartarto ambae ni miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia katika uwanja wa Ndege wa Soekarno Hatta Mjini Jakarta Nchini Indonesia baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi IORA Nchini humo Dk.Shein alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,
↧
↧
UN SECRETARY GENERAL STOPS IN DAR ON HIS WAY TO NEW YORK
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guterres (kushoto) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam jana. Mhe. Guterres alisimama kwa muda katika uwanja huo akitokea nchini Kenya kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Balozi Mahiga. Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe Guterres aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa Mgogoro huo Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Benjamin Willium Mkapa. Aidha, Dkt. Mahiga aliwasilisha Salamu Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri Mahiga akizungumza jambo huku Mhe. Guterres akimsikiliza kwa makini.
Dkt. Mahiga akiendelea kuzungumza na Mhe. Guterres huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakiwasikiliza kwa makini.
Picha ya pamoja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Bi. Mindi Kasiga naye akiagana na Mhe. Guterres
Mhe. Guterres akiagana na Dkt. Mahiga mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo yao.
H.E. Dr. John Pombe Magufuli, the President of the United Republic of Tanzania has urged the United Nations to continue its support in bringing about political stability in Burundi and the Democratic Republic of Congo.
In his special message to the United Nations Secretary General Mr. Antonio Guterres President Magufuli explained that the recent instability in the two countries has created refugees’ influx in Tanzania and its neighbors, hence the region is committed to ensure political stability is restored.
Delivering President Magufuli’s message to the United Nations Secretary General Mr. Antonio Guterres, Tanzania’s Foreign Minister Augustine Mahiga said that as the chair of EAC, Tanzania is hopeful with the progress been made in the mediation process in Burundi under the leadership of President Yoweri Museveni of Uganda and facilitated by the former President of Tanzania, H.E. Benjamin William Mkapa. Hon. Mahiga also informed the UN Secretary General that the upcoming EAC Summit is expected to receive a progressive report about the process.
With regards to the Democratic Republic of Congo, Minister Mahiga revealed that the Southern African Development Community is intending to include the agenda of political transition in DRC, whereby SADC member states are expecting positive deliberations. Tanzania is the current chair of the SADC organ of political, defense and security with the mandate to support the achievement and maintenance of peace and security as well as the rule of law in the SADC region.
Upon receiving President Magufuli’s message, Mr. Guterres praised Tanzania for its ability to uphold principles of good governance in the country as well as maintaining peace and creating a peaceful environment in the EAC and SADC regions.
Mr. Guterres commended President Magufuli’s efforts in Burundi peace process, and his readiness to host refugees from Burundi, emphasizing the role played by regional communities in Africa in resolving leadership crisis in African countries.
“The United Nations appreciates the work done by President Mkapa in Burundi under the EAC and its leadership. If the region come together the way EAC has done in the case of Burundi, I am sure together they will be able to establish lasting solutions” he remarked.
Minister Mahiga told the reporters that President Magufuli met Mr. Guterres during the AU Summit in Addis Ababa earlier this year, where the two leaders exchanged cordial discussions about various issues concerning the region.
“President Magufuli instructed me to deliver his message to Mr. Guterres, and has also extended an invitation to the Secretary General at an appropriate time to have a working visit in the country” concluded Hon. Mahiga.
Mr. Guterres was met and held talks with Foreign Minister Mahiga at the Julius Nyerere International Airport yesterday night where he was on transit from Somalia and Kenya for a working visit. Also present at the airport was the United Nations Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez and officials from the Ministry of Foreign Affairs including the Director of Multilateral Cooperation Ambassador Celestine Mushy and Ministry’s Spokesperson Ms. Mindi Kasiga.
Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dar es salaam, Tanzania
March 9, 2017.
↧
MENEJA PETIT MAN AFUNGUKA YALIYOMKUTA LUPANGO NA KIPIGO
MENEJA wa msanii wa Bongo Fleva, Bill Nass na County Boy anayefahamika kama Ahmed Salum ‘Petit Man’, ameongelea fedheha na hasara iliyomkuta alipokumbwa na kashfa ya kuhusishwa na dawa za kulevya na kujikuta akiswekwa lupango.
Katika mazungumzo juzi, Petit Man, alisema kitendo cha kukaa mahabusu kwa wiki moja kimempotezea fedha nyingi ambazo alikuwa amepanga kuingiza kwa wiki ile ili kuwafikisha hatua nyingine wasanii wake wanaomtegemea yeye kwa asilimia kubwa.
“Naumia sana nikizungumzia suala hili kwa sababu naona ni moja ya vitu ambavyo vilitaka kunitia umasikini, pesa (fedha) niliyoipoteza wiki ile ilikuwa ya kunitoa sehemu moja kwenda nyingine, ilikuwa nyingi na nilitarajia kufanya mengi sana,” alisema Petit Man.
Aliongeza kuwa mahabusu si sehemu nzuri kwani amejifunza mengi sana na amekumbana na watu tofauti ambao wengine ameweza kuwasaidia na wengine imeshindikana.
Akizungumzia kipigo alichodaiwa kupigwa, Petit Man, alisema kutangaziwa kupigwa ilikuwa kama fedheha kwake akikiri kwamba alipata misukosuko ya kawaida na si kipigo kama ilivyovumishwa.
“Nadhani Kamanda Sirro (Simon) ni askari mkubwa na msomi, sidhani kama anaweza kutoa adhabu isiyostahili na inayokiuka haki za binaadamu na mimi nilipata adhabu yangu kama mtuhumiwa na yote hiyo ilikuwa ni kupata ukweli na si mimi pekee, nadhani wengi walipata adhabu ili waseme, sasa huo uvumi mwingine mimi siutambui na huwa sipendi kuongelea naona kama umeniletea fedheha kwenye jamii, kila mtu anatafsiri yake,” alisema Petit Man.
Aliongeza: “Mimi sina rekodi mbaya, nina imani hii adhabu kabla ya kuisha nitapewa ruhusa ya kufanya mambo yangu kwa uhuru, hakuna asiyenijua mimi ni mtu wa aina gani, napenda sana kushirikiana na watu wa aina zote na kumsaidia mtu pale ninapoweza.”
Akizungumzia sakata la aliyekuwa swahiba wake wa muda mrefu, Wema Sepetu, kuhama chama, alisema kila mtu ana mawazo yake na utashi wake hivyo kama ameamua kufanya hivyo, basi inabidi wao wawe wasikilizaji kwani Miss Tanzania 2016 huyo ana wazazi wake na kwamba hayo ni mapendekezo ya mtu.
Hata hivyo, aliweka wazi akisema: “Mimi na Wema bado ni familia moja japokuwa kila mtu ana kampuni yake, niliamua kutoka kwenda kwenye kampuni ili kujitafutia kipato na nitaendelea kushirikiana naye kwa kazi ambazo tulikuwa tukifanya.”
Pia alizungumzia ndoa yake na mkewe, Esma Kandili ‘Esma Platinumz’ ambaye ni dada wa msanii nguli wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, akisema anaamini ndiye mwanamke aliyechaguliwa na Mungu na katu hatafikiria kwenda kwingine.
“Nina amini Esma ndiye mwanamke niliyechaguliwa na Mungu, tulijaribu kutengena ila ilishindikana na kujikuta kila mmoja akimhitaji mwenziye na sasa ndoa yetu imerudi, ifahamike ndiye aliyenipa heshima ya kuitwa baba baada ya kufanikiwa kupata mtoto aitwaye Taraj,” alisema Petiti Man.
↧
WAZIRI NAPE NHAUYE KUMLINDA MMILIKI WA REDIO EFM NA TV E
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, ameahidi kulinda uwekezaji wa mmiliki wa kituo cha Redio EFM na Tv E, Francis Ciza, maarufu Dj Majizo.
Nape alitoa kauli hiyo jana wakati alipotembelea makao makuu ya kituo hicho cha redio katika eneo la Kawe, Dar es Salaam.
Katika hotuba yake fupi aliyoitoa mbele ya watumishi wa redio hiyo jana, Nape alisema yeye ndiye waziri mwenye dhamana ya habari, hivyo ana wajibu wa kulinda habari na wawekezaji katika tasnia hiyo.
“Nataka nikuhakikishie mimi ndie waziri mwenye dhamana ya habari, kuilinda habari na tasnia yenyewe, lakini kuwalinda wanaowekeza kwenye tasnia hii, kwa sababu uwekezaji kama huu ulioufanya katika tasnia hii, ndio unanifanya mimi kama waziri niendelee kuwapo.
“Lakini ndio unaoifanya Serikali na Tanzania kuendelea kuwa nchi njema ya watu waendelee kuishi, kazi yako ni nzuri na nyinyi kwa kuwa mnasikika sana Dar es Salaam, mchango wenu wa kuifanya Dar es Salaam kuwa njema ni mkubwa na hauwezi kupuuzwa hata kidogo.
“Kwa mtu yeyote mwenye mapenzi mema na Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla atawalindeni, atawalinda na kuhakikisha mnapata ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yenu,” alisema.
Nape pia alimpongeza Majizo kwa uwekezaji mkubwa alioufanya na kuahidi kwamba serikali itampatia ushirikiano na msaada anaouhitaji ili kuhakikisha uwekezaji wake unasonga mbele.
“Kama Serikali na kama waziri mwenye dhamana ya habari, nimeshuhudia kwa macho yangu uwekezaji uliouweka hapa, tutalinda uwekezaji uliouweka usiharibiwe ovyo.
“Si Watanzania wengi wenye maono haya, najua umeanza mbali mpaka kufika hapa, si kazi rahisi, ndiyo maana nasema ukiona mtu kasimama si vizuri kwenda kumparamia ovyo.
“Ni vizuri kuheshimu kazi ambayo amehangaika nayo, jasho si la bure, uwekezaji huu ni mkubwa sana, labda iwe hujui alichowekeza, hujui kapambana kiasi gani kufika hapo ndiyo unaweza kufanya unachotaka,” alisema Nape.
Nape alisema katika dunia yenye ushindani vita ni kubwa, hivyo akamtaka mwekezaji huyo asikatishwe tamaa na kelele za barabarani kwa sababu Serikali iko pamoja naye.
Aliwaeleza pia watumishi wa redio hiyo kwamba wasiwe na hofu kwa sababu kazi wanayoifanya ina baraka za Mungu, hivyo hawapaswi kuvunjika moyo.
“Mkiona mti unaotupiwa mawe ni ule wenye matunda, kwa miaka mitatu mafanikio mliyoyapata ni makubwa sana, lazima yatamtisha yule aliepo sokoni, kwahiyo mkiona kuna vita basi mjue ni kwa sababu kasi yenu ni kubwa mno kiasi kwamba inawatia joto wengine.
“Mtu mmoja aliwahi kuniambia wakati naanza siasa kwamba ukiona watu hawakuzungumzii jiulize kama bado unaishi au umeishakufa, ukiona watu wanakuzungumza ujue umewazidi,” alisema Nape.
Majizo ni mmoja wa watu waliohusishwa na dawa za kulevya katika kampeni iliyokuwa ikiendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro.
↧
↧
STAA SHILOLE WATU HAWAWEZI KUISHI BILA KUMTAJA NUH MZIWANDA.

Bad girl Bongo mwenye tittle kubwa nchini Shishibaby amesema kwamba alifanya Tour na Nuh Mziwanda kama msanii mwenzake katika na si vinginevyo ila kama watu wanavyokuwa wakimtaja Nuh Mziwanda wanatoka pamoja.
Awali Shishi na Nuh walikuwa wapenzi ambao waliweka historia kubwa katika Story za mahusiano Bongo zilizobeba headlines za Entertainment news Bongo ila baadaye walimwagana baada ya Nuh kulalamika anaonewa zaidi kuliko kupata utamu wa Penzi.
Akipiga Story katika kipindi cha Leo Tena Shishi amesema anawashanga watanzania kuongea vibaya ukaribu wake na Nuh sababu walikwisha achana kitambo na Nuh ameoa.
“Tunachotakiwa kufahamu MUZIKI ni biashara niliangalia nani anaweza kufit in nikamchukua Nuh tukapige kazi” alimaliza Msanii huyu ambaye leo ametambulisha goma jipya linaitwa Hatutoi Kiki.
↧
LEBO YA WCB KUIPELEKA BONGO FLEVA KABURINI

Mavoko, Queen Darleen na Rayvanny
Hayo yote nayasema kuhusu nyota wa Bongo fleva, Nasibu Adul Juma au maarufu zaidi kwa jina la Diamond. Siku za hivi karibuni, Diamond ameanzisha zoezi la kuwachukua wanamuziki na kuwaingiza kwenye kundi lake maarufu sana la Wasafi Classic Baby ‘WCB’ ambalo limetokea kupata jina kubwa katika Muziki wa Kizazi Kipya Bongo.
Lebo hii ya Wasafi kwa sasa inaundwa na watu wanne, Queen Darleen, Rayvanny, Rich Mavoko na Harmonize. Awali, alianza na akina Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko na mwisho ni Queen Darleen. Harmonize na Rayvanny walikuwa hawakutamba sana kabla ya kwenda Wasafi. Mimi kwa hao, naona ni sawa kabisa na wala sina tatizo nao.

Queen Darleen kushoto na rafiki yake
ANAINUA VIPAJI
Katika mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya habari hapa Bongo, Diamond amekuwa akisema kwamba, anafanya hivyo ili kukuza muziki na kuinua vipaji vya wanamuziki wachanga wa Tanzania. Mimi kwa hilo pia sina tatizo naye. Pia, watu au wadau mbalimbali wa muziki huo wakawa wanampongeza Diamond kwa kuwa, zoezi lake la kuwabeba akina Harmonize linaongeza ushindani mkubwa katika Muziki wa Kizazi Kipya, kwamba kama yeye anawainua hawa, wengine wakainuliwa kule, muziki utapaa. Na kwa hili pia mimi sina tatizo nalo hata kidogo.

Daimond
NI HOJA ZA MSINGI SANA
Kuna hoja za msingi kwamba, kama si Diamond, hawa akina Rayvanny wasingekuwa hivi walivyo leo. Wasingejulikana kama wanavyojulikana wakiwa kwa Diamond. Hiyo ni hoja ya msingi sana, tena sana. Na kwa hilo mimi sina tatizo na hoja husika.
KUHUSU RICH MAVOKO
Katika zoezi lake la kuendelea kuchukua wasanii, Diamond akamchukua Mbongo Fleva, Rich Mavoko ndani ya kundi lake la Wasafi. Hapa kidogo baadhi ya watu wakahoji uhalali wa usahihi wake. Wengi waliamini kuwa, Diamond kumchukua msanii huyo ambaye alishajenga jina kubwa katika muziki huo ni sawa na kumpoteza njia kwani Rich Mavoko kuwa chini ya Wasafi kunaweza kumfanya afifie kama siyo kufa kabisa kisanii.

Mkubwa (kushoto) na Rich Mavoko
NINACHOKIONA
Sasa ninachokiona mimi ni kwamba, nia ya Diamond inaweza kuwa nzuri sana lakini kukatokea makosa madogomadogo kwenye kuchukua aina ya wasanii. Yapo madai ya chini kwa chini kwamba, pia ana mpango wa kumchukua msanii anayevuma sana kwa sasa, Darassa ambaye kibao chake cha Muziki kimeishika nchi kwa kupigwa maeneo mbalimbali. Kama kuna ukweli wa madai haya, naamini kuna siku tutakuja kusikia, hata Ali Kiba, Ommy Dimpoz nani sijui, wote wana mpango wa kujiunga Wasafi. Katika hili, ninatia shaka kwamba, lengo la Diamond kuwakusanya wasanii niliowataja na kumchukua pia Rich Mavoko ni njia moja kwake ya kuelekea kwenye kuudidimiza muziki wa Bongo Fleva.
Harmonise
Wasafi linajiimarisha kuwa kundi kubwa la muziki huo nchini. Sasa je, ikitokea hivyo, upinzani utatoka wapi? Ninavyojua mimi siku zote, palipo na ushindani ndipo panapokuza kitu. Ni sawa na timu za mpira wa miguu wa Tanzani, piga mahesabu kwamba, kuna siku Simba itashuka daraja. Je, Yanga atabaki na mshidani gani? Na kilele cha raha ya mpira wa Tanzania ni kucheza kwa Simba na Yanga.
Ndiyo maana, makocha wa timu hizo bora wafungwe na timu nyingine zote, lakini siyo Simba au Yanga. Hata shule wanazosoma watoto wetu siku hizi, ubora wake inatokana na kuwepo kwa shule bora nyingine. Kama ingekuwa shule moja tu ndiyo bora sifa yake isingekuwa na maana. Sifa ya mtu mrefu duniani kote inatokana na kuwepo kwa mtu mfupi. Kama watu wote wangekuwa na kimo sawa isingejulikana kama urefu ni bora.
Kuwepo kwa Wasafi kusiwe sababu ya kuwakusanya wanamuziki wengine hawa wenye majina makubwa kwani na wao uwepo wao ndiyo changamoto ya kuwepo kwa Wasafi. Inawezekana nia ya Diamond ikawa nzuri sana lakini mimi naamini anakokwenda, kunaweza kuwa ndiyo kaburi la muziki wenyewe.
↧
HATIMAYE PLATFORM YA DIAMOND PLATNUMZ YA KUUZA NYIMBO ONLINE IMEKAMILIKA

Miezi kadhaa nyuma mkali wa Bongo Fleva Diamond Platnumz alitusanua kwamba muda sio mrefu atakuja na mtandao wa kuuza kazi za wasanii. Na kudai kwamba hiyo ni kutokana na wasanii kudhulumiwa sana haki zao na vitu kama hizo.
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, mtandao huo umekamilika na tayari kabisa kwa ufanyaji kazi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond Platnumz ametusanua kila kitu kuanzia malengo na jinsi ya ufanyaji kazi wa mtandao huo.
Kikubwa na kilichowashangaza zaidi wengi ni baada ya kufunguka kuwa mtandao huo utadeal na kazi za wasanii wengi tofauti tofauti wa hapa nchini, tofauti na matarajio ya wengi kwamba mtandao huo unge-deal na kazi za wasanii wa WCB pekee.
Kupitia post hiyo, Diamond aliandika hivi “Habari Mashabiki zetu pendwa…tunayo furaha kukupa habari njema ya kwamba kuanzia sasa @wasafidotcom ndio sehemu rasmi na pekee ya kuweza kujipatia Nyimbo za wasani wako wote pendwa toka hapa nchini Tanzania na nje ya tanzania…lengo kuu la kuanzisha mtandao huu ni kuweza kuwarahisishia Mashabiki na wadau wa mziki wetu muweze kujipatia kazi za wasani wenu zikiwa zina Quality ama ubora sahihi, kirahisi na haraka…lakini pia kutusapot vijana ama watoto wenu nasi tuweze kuendelea kuwatengenezea kazi zenye ubora zaidi….Lakini pia sababu nyingine ya kuamua kuanzisha mtandao huu ni jinsi mlivyokuwa mnatusapoti vijana wenu kwa kununua kazi zetu halaf mwisho wa siku baadhi ya wamiliki wa mitandao wakawa hawatupi haki zetu tunayostahili, yaani wakawa wanatudhurumu na kunufaika wao huku sie wasanii wenu tukiishia kuambulia umaarufu wa majina ila maisha yetu halisi “pangu pakavu”…hii ilituumiza na kutuliza sana, karibu miaka yote…..kwenye mtandao huu wa @Wasafidotcom tumeeka njia mbalimbali rahisi za kununua nyimbo, kupitia account ya simu yani Mfano: Vodapesa na mitandao yote ya simu Afrika, na pia kununua kwa njia ya Card ya Benki mfano: Master Card, Credit card, Visa card na njia zote za kibenki…. Matumaini yetu kuwa mtatusapoti kwa kununua kazi zetu @wasafidotcom…. na panapo majaaliwa kwa mara ya kwanza ijumaa ya kesho @Harmonize ataachia wimbo wake mpya Uitwao #NAMBIE na utakuwa unapatika @Wasafidotcom tu …. nitasikitika sana sana nikiona ama kusikia shabiki yetu wa damu ama mpemda muziki, anakuwa mtu wa kwanza kuomba kutumiwa nyimbo kwa bloototh ama Watsup badala ya kuingia @wasadidotcom kudownload….. kesho hiyohiyo pia kutakuwa Rasmi na App pamoja na nyimbo za wasanii wengine zaidi uwapendao…. @Wasafidotcom #WhereTheHitsBelong !!!!!! Mie nimewaekea ngoma zooote za tangu kale na zingine ambazo hamjawai kuskia, follow account Rasmi ya @Wasafidotcom ubonyeze link kwa bio ukapakue nyimbo uzitakazo
↧
RAPA NAY WA MITEGO ASALIMU AMRI MTOTO WA SISTER FAY
MSANII wa muziki Bongo, Sister Fay ambaye siku chache zilizopita aliingia kwenye mgogoro na msanii mwenzake Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa madai ya kumtelekeza mtoto aliyezaa naye aitwaye Prince, hatimaye ameafikiana na Fay kuwa atamsomesha.
Baada ya kutokea sekeseke hilo walikubaliana kufanya kipimo cha DNA ambapo mara ya kwanza zoezi hilo halikufanikiwa na kukubaliana kufanya baada ya wiki mbili kwa maana ya wiki hii, ndipo mwanadada huyo akafunguka kuwa hawawezi kupima tena kwani Nay kakubali kumsomesha mtoto.
“Ni kweli tulikuwa kwenye mpango wa DNA lakini Nay kakataa kaona aina haja, kakubali kumsomesha mtoto, namshukuru Mungu kufikia hatua hiyo, naamini kila kitu kitaenda sawa,” alisema Sister Fay.
Kwa upande wa mtuhumiwa, Nay wa Mitego alipotafutwa kwa njia ya simu iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakujibu.
↧
↧
RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo tarehe 9/03/2017. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU.
Rais Dkt Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan mapema leo mchana mara baada ya kumaliza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma,kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawazili,kilichofanyika leo mjini Dodoma![]()

Waziri wa habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,Nape Nnauye akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo.PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.
↧
BREAKING NEWZZ:MDOGO WA MCHUNGAJI GWAJIMA AFUNGUKA MAZITO NA KUMPINGA KAKA YAKE

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, Methusema Gwajima amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika holeli ya Traveltime Kinondoni jijini Dar es salaam, Methusema amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.
“Katika hilo watanzania naomba sana tumpuuze, nasema tumpuuze kwa sababu hoja zake zimejikita katika lengo la kutafuta defance, kutafuta kinga. Umeshatuhumiwa, umeitwa polisi, kwa nini usisubiri uchunguzwe, wameitwa watu wengi wameenza kwanini yeye analifanya hilo jambo kuwa ajenda, mbaya zaidi imekuwa ni ajenda kanisani, kwahiyo kanisa limegeuzwa kuwa kijiwe cha siasa lakini watanzania wamekaa kimya hawasemi,” alisema Methusema.
Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.
Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.
Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.
Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.
↧
SAKATA LA DAWA ZA KUSISIMUA MISULI 'HALI BADO TETE URUSI
Takwimu zilizotolewa na WADA zilionesha kwamba zaidi ywa wanamichezo 1,000 walinufaika kwa namna moja au nyingine kutokana na matumizi ya dawa zilizokatazwa michezoni kti ya mwaka 2011 - 2015.
Kutokana na tatizo hilo kuonekana kuwa kubwa nchini Urusi viongozi wa michezo mbalimbali nchini humo wameahidi kupigana katika vita hiyo dhidi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
Ngili amesema jitihada zinazofanywa na Urusi ni ndogo na haziendani kabisa na kasi ya upigaji vita wa dawa za kusisimua misuli ndio sababu wanamichezo mbalimbali wa Urusi wamepigwa marufuku ya kushiriki katika michezo mbalimbali.
Miongoni mwa wanamichezo hao ni pamoja na wanariadha ambao wamepigwa marufuku na Chama cha Mchezo wa Riadha duniani IAAF
Kuhusu mchakato wa ushiriki wa Urusi kupewa nafasi ya kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya majira ya joto mwakani Katibu huyo amesema watatazama kama hilo litawezekana, lakini kubwa ni kwamba litategemea na jitihada watakazozionyesha katika upigaji vita wa dawa za kusisimua misuli.
Wakati huo huo Urusi imeandaa mpango wa kuweka mabango pembezoni mwa barabara kama sehemu ya kuonyesha hisia zake juu ya upigaji vita dawa hizo.
↧
WAZIRI MKUU KUFUNGUA MKUTANO WA LAPF,JIJINI ARUSHA

Na Pamela Mollel Arusha.
MFUKO wahifadhi ya wafanyakazi wa serikali za mitaa,LAPF,umeipongeza serikali kwakulipa malimbikizo ya madeni ambayo mfuko huo na mingine ilikuwa ikiidai kwamiaka mingi na hivyo kuathiri usitawi wa mifuko hiyo.
Meneja wa LAPFkanda ya kaskazini, Rajabu Kinande, amesema hatua ya serikali kulipa madenihayo kumeiongezea mifuko ya hifadhi ya jamii uwezo wa kuhudumia wanachama waokwa wakati. Kinande, ameyasemahayo Marchi 7 jijini Arusha,alipokuwaakizungumza na vyombo vya habari kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa, AICC,kuelezea hatua ya maandalizi ya mkutano mkuu wa siku mbili wa mwaka wa wadau waLAPF.
Amesema mkutanohuo utafunguliwa na Waziri mk
uu waJamhuri ya muungano wa Tanzania,Mh,Majaliwa KassimMajaliwa,Marchi 10 mwaka huu ambapo zaidi ya wanachama 1000 wa mfuko huo wanatarajiwa kuhudhuria.
Awali MenejaMawasiliano na Masoko wa LAPF,James Mloe, amesema kuwa kwenye mkutano huokutawasilishwa mada mbalimbali zikiwemo Uendeshaji wa shughuli za mfukohuo,Hesabu zilizokaguliwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG)za mwaka 2015/16ambapo mfuko huo umepata hati safi ya ukaguzi wa hesabu ,UKusanyaji wa michango ulipaji wa mafao kwa wanachama na uwekezaji,Utawala bora na usimamizi wa uendeshajiwa mfukohuo na Raslimali fedha .
Amesema sikuya kwanza ya mkutano huo Marchi 9 kwa kuzingatia kuwa ni siku ya Figo dunianimfuko umeandaa upimaji wa figo bure kwa wanachama wote ambao utafanywa naMadaktari bingwa
.Mloe,amesema siku ya pili yamkutano huoWaziri mkuu Kassim Majaliwa atazindua program mpya ya mikopo kwa wanachama kwa kushirikiana na benki ya CRDB,iitwayo Maisha popote ambao ni mkopo wakwanza kutolewa na mfuko huo.
Amesemakauli mbiu ya mwaka huu ni kuibua fursa endelevu za ajira kwa maendeleo endelevu kwa watanzania.Kuhusuuwekezaji kwenye viwanda,Mloe, amesema kuwa LAPF, imeweka mitaji kwenye viwanda ambako tayari wameweka hisa zao .
Amesema kuwaLAPF,haiwezi kujenga viwanda na kuvisimamia uendeshaji wake bali itaweka mitajina kusisitiza kuwa LAPF itabakia kwenye jukumu lake la msingi la kulindamichango ya wanachama wake. Mwisho .
↧
↧
PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA KWENYE MKUTANO WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM
Dodoma. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo amesema hatogombea tena nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo.
Bulembo ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi) katika kikao cha baraza hilo mjini Dodoma na kutumia fursa hiyo kuwaaga wajumbe hao na kusema kuwa hoja siyo ubunge alioteuliwa bali ni utamaduni wake aliojiwekea katika maisha yake.
"Hoja hapa siyo ubunge kwamba nitakuwa nakofia mbili huu ni utaratibu wangu niliojiwekea katika maisha siwezi kung'ang'ania madaraka. Nilifanya hivi nilipokuwa naibu Meya Musoma na nilipokuwa kiongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Nchini (TFF), " amesema.
Kutoka na uamuzi huo Bulembo amewaonya wajumbe wenye lengo la kuchukua fomu ili kumrithi kutomfuata wala kumpigia simu awasaidie badala yake amewataka wafuate utaratibu wa jumuiya hiyo.

↧
MSANII PASHA ATESEKA NA PENZI LA SNURA MAJANGA

Snura
Msanii wa Bongo Fleva, Khaji Mtepa ‘Pasha’ aliyewahi kutamba na Nyimbo za Thamani ya Penzi, Umeniweza, Hidaya, Ni Soo na nyingine kibao amefungukia mateso makubwa anayoyapata juu ya penzi la msanii mwenzake, Snura Mushi.
Pasha na Snura
Akizungumza na safu hii katika mahojiano maalum, Pasha alifunguka kuhusu maisha yake ya muziki, kawaida, uhusiano na mikakati yake mipya kimuziki.
HADI SASA UMETOA NYIMBO NGAPI?
Tangu mwaka 2006 hadi leo nimetoa nyimbo nyingi sana, mwaka 2008 nilitoa albamu moja yenye nyimbo 14, baada ya hapo, nimekuwa nikitoa single hadi sasa.
NINI KILIKUPOTEZA KWENYE GEMU?
Sijapotea, bado ninaendelea kurekodi nyimbo, nafanya shoo, pengine ukimya ni kwa sababu sijatoa ‘hit song’ kwa muda mrefu.
Snura
KUNA WAKATI ULIUNGANA NA H.BABA, MLIFIKIA WAPI?
Ni kweli, tuliungana kufanya baadhi ya nyimbo zetu ila si kwa kuunda kundi la pamoja. Tulitengana baada ya H.Baba kupata menejimenti mpya. UNA MKE AU WATOTO? Nina mtoto mmoja. Anaitwa Ipa, bado sijao ila Inshaallah muda ukifika Mungu atanipatia mke.
WAPI UNAPOHISI BIASHARA YA MUZIKI INA UPUNGUFU KWA BONGO?
Upungufu upo, lakini mimi naamini biashara ya muziki ndiyo kwanza imeanza kushika kasi miaka ya hivi karibuni. Miaka ya nyuma ubora wa kazi haukuwa mzuri kutokana na vifaa duni. Pia hatukuwa na wasambazaji nje ya Bongo. Ingawa mimi nje ya muziki ninafanya biashara tofauti.
NI MSANII GANI WA KIKE NA KIUME UNAYEMKUBALI?
Wapo wengi, kila msanii namkubali kwa kigezo chake, mwingine kwa uimbaji wake mzuri, msanii kama Dyna Nyange namsheshimu sana kwa kukomaa kwenye gemu muda mrefu tofauti na wengine. Kwa upande wa msanii wa kiume ninajikubali mwenyewe.
PENZI LA MSANII GANI WA KIKE WA FILAMU AU MUZIKI HUWEZI KULISAHAU?
Kutoka moyoni, penzi la msanii Snura Mushi, siwezi kulisahau.
SNURA WA CHURA AU MWINGINE?
Yaah. Ni huyuhuyu. NINI HASA CHA TOFAUTI KINACHOKUFANYA USIM-SAHAU? Anajua ‘kucare,’ ni mwaminifu, anajua sana mapenzi, mtoto amefundwa yule, akafundika.
IKITOKEA SNURA AKAKUBALI KUISHI NAYE YUKO TAYARI?
Hapana, imeshapita miaka mingi zaidi ya saba, ni kitambo sana. Kila mtu amesha-move on na maisha yake, mengine yamebaki stori.
MLIDUMU KWENYE UHUSIANO NA SNURA KWA MUDA GANI?
Mwaka mmoja na tuliachana bila sababu zaidi ya kila mtu kuwa bize na kazi zake.
UNAMAANISHA WAKATI UKIWA NAYE HAKUWA NA MTOTO?
Ndiyo, zamani sana, hata muziki alikuwa hajaanza, ni enzi za Jumba la Dhahabu ingawa na mimi pia niliigiza naye filamu mbili ikiwemo Kisasi cha Mzimu na Uungwana.
UMESHAWAHI KUVUTA AU KUDILI NA MADAWA YA KULEVYA?
Hapana, sijawahi kuvuta, kutumia hata pombe pia situmii. Vita ya madawa naiona ni hatua nzuri, waendelee kupigana nayo, isiwe kwa wasanii pekee, iwe kwa jamii nzima.
UNA MIKAKATI YA KURUDI KWENYE SANAA MWAKA HUU?
Nazidi kujipanga na nitarudi kwa kishindo, mashabiki waendelee kusubiri
↧
UONGOZI YANGA WAZUNGUMZIA DENI LA 'HANS VA DER PLUILM
↧
WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA ZIARA KUKAGUA USAFI WA MAZINGIRA MJINI DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akiambatana na Afisa Masoko Manispaa ya Mji wa Dodoma, Stephen Maufi katika ziara fupi ya kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene na Naibu Katibu Mkuu Afya , Dkt. Zainabu Chaula wakiangalia mfereji wa maji machafu uliopo katika Soko la Mwembeni katika ziara fupi ya kutembelea na
kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akifurahia ubunifu wa uhifadhi wa mbogamboga na matunda katika ziara fupi ya kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa
Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akizungumza na mmoja wa wafanya biashara katika soko la Mwembeni Bw. Mjahidina Hassani katika ziara fupi ya kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI) , Dkt. Zainabu Chaula akisisitiza juu ya Uhamisho wa wafanya biashara ndogo ndogo kwenda Uwanja wa Barafu katika ziara fupi ya
kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akiongea na waandishi wa habari
kuhusu tamko la utekelezaji na ufatiliaji wa ugonjwa wa Kipindupindu katika Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Ofisini kwake, Dodoma.
Picha na: TAMISEMI.
↧
↧
BILIONI 10 ZA RAIS MAGUFULI KWA UDSM ZAKAMILISHA KAZI
Ujenzi wa majengo 20 yenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya wanafunzi 3,840 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo kila jengo lina ghorofa nne umekamilika baada ya kuchukua muda wa miezi minane.
Suala kubwa nililojifunza katika siasa za Tanzania ni kuwa na kiongozi shupavu anayesimamia kile anachokiamini na kukiamua bila kujali kelele za wanasiasa wanafiki na wale wasioamini.
Ikumbukwe kuwa kuna wakandarasi walitaka kulipwa bilioni 100 katika mradi huu.
Kuna wengine walileta thread hapa na kuwaaminisha baadhi ya wana JF kuwa wataleta gharama kamili ya ujenzi lakini mpaka sasa ''wameingia mitini'' kwa sababu uwongo wao ulitumia lifti kuwafikia walengwa lakini kwa sasa ukweli unafika kwa kutumia ngazi.
Picha hizi pia zinatoa fundisho kwa wasioamini ambao pia wameainishwa kwenye vitabu vya Mwenyezi Mungu ndani ya Quran na Biblia.
Kwa wale wanaojua Quran wanaweza kuelewa maana ya maneno yangu kupitia verse 44 ya Surah Fussilat (41).
Kwa wale wanaojua Biblia wanaweza kuelewa maana ya hoja yangu kupitia Yohana 20:24.
Kuna msemo usemao, Kama hujui kusoma, hata picha huwezi kutazama?
Focus and perseverance is what separates winners from losers.
↧
STAA IRENE UWOYA AMPATANO RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE

Muigizaji Irene Uwoya amemshukuru Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kuwathamini na kuwaamini wanawake kwa kuwapa nafasi za juu katika kuongoza taifa la Tanzania.
Uwoya kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa hawezi kumsahau Rais huyo kutokana na uamuzi wake wa kutoa nafasi kubwa kwa wanawake katika serikali yake, zikiwemo nafasi za uwaziri, majaji na hata Spika wa bunge, na kwamba, Rais huyo ndiye aliyempa motisha ya kugombea ubunge.
"Namshukuru sana Rais mstaafu... Mh. JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa kutupa wanawake heshima na kututhamini... Alitupa nafasi nyingi sana katika nafasi za mawaziri, majaji na spika... Na hata mimi kama msanii nilihamasika na kuona naweza kugombea ubunge... Kiukweli amefungua njia na ameweka mwanga mkubwa kwa viongozi wengine na wao wakaendelea kuthamini na kuheshimu mchango wetu katika jamii ndiyo maana hata tukapata makamu wa Rais mwanamke kwa mara ya kwanza Tanzania". Amesema Irene
Katika hatua nyingine, Uwoya ameungana na wanawake wengine duniani kusherehekea siku ya wanawake, huku akionesha kukerwa na wanaume wanaowadharau wanawake huku akiongeza kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika jamii na kwamba mwanamke ni mlezi na pia wakati mwingine husimama kulisha familia.
"Mwanamke ndiye mama wa taifa... Ndiyo maana Marekani mwaka 1911 iliadhimishwa siku ya wanawake duniani ambapo vikundi tofauti vya wanawake viliungana kupinga ukandamizaji, uonevu na ubaguzi wa jinsia hususani sehemu za kazi... " Ujumbe wa Irene Uwoya.
↧
RC MAKONDA AKWAMISHA MIPANGO YA MANFONGO

Msanii wa singeli, Manfongo amesema yeye kushindwa kuachia wimbo wake aliomshirikisha Mr Blue ni kwa sababu ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kumtaja Blue katika orodha ya watu wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.
Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz cha EATV, Manfongo amesema kuwa wimbo huo ulikuwa katika maandalizi mazuri lakini baada ya kusikia jina la Blue katika watu walioambiwa wahudhurie kituo cha polisi akaona ni afadhali kwanza amuache msanii huyo amalize matatizo yanayomkabili kwanza.
“Blue alinipigia simu akanambia mdogo wangu nimepata ‘show’ Muscat si unajua familia lazima ile? sasa ameondoka tu Mkuu wa Mkoa naye akatangaza majina ya watu anaowataka kufika kituo cha polisi naye akawepo. Nikaona kwa vile mashabiki walikuwa wanajua ujio wa kazi yangu mpya bora niachie hii ‘Safi tuu’ halafu kichwa cha kaka yangu kikitulia tumalizie kazi lakini mashabiki wanachotakiwa kujua ni kuwa kazi hiyo ipo na lazima tuitoe".- alisema Manifongo

Katika hatua nyingine Manfongo amesema yeye kuacha kufanya kazi na meneja wake wa zamani G-Maker siyo kwamba ndiyo muziki wake utakuwa umekufa bali ndiyo atakaza kufika kimataifa kwani yeye ndiye mwenye muziki huo.
Kwa sasa Manfongo anasimamiwa katika kazi zake na Wasowiso ambaye ni meneja wake wa zamani ambapo amesema atatumia pesa zake kuji- 'brand' na siyo kuwapa watu hela waliokuwa wanamtumia bila faida.
Huyu hapa Manfongo akifunguka
↧