↧
Article 3
↧
BILIONEA ALIKO DANGOTE AANZA KUWEKEZA KWENYE MUZIKI

Tajiri Afrika nzima Aliko Dangote ameonyesha nia ya kuwekeza kwenye muziki. Kama unakumbuka mwaka jana mfanya biashara huyu alionekana na P Square na kutengeneza vichwa vya habari kuhusu colabo hio.
Aliko Dangote hivi karibuni alikuwa na staa wa muziki kutoka Mavin Records Korede Bello ikiwa ni matayarisha kuelekea kutoka kwa album ya msanii huyu #Belloved mnamo March 11
Tunasubiri kusikia kiasi gani cha pesa Aliko atawekeza kwenye muziki wa Korede Bello.
↧
↧
CHANZO CHA KIFO CHA STAA GEORGE MICHAEL KIMETAJWA

Kilichosababisha kifo cha Pop staa George Michael kimetajwa kuwa ni matatizo ya maini na moyo ila mpaka sasa haijulikani kama pombe imechangia madhara hayo.
Michael alikuwa na tatizo la mafuta kwenye maini linalosababishwa na unywaji pombe kupitiliza na uzito mkubwa. Pia daktari anasema kulikuwa na tatizo kwenye mishipa ya moyo.
Michael alifariki kwenye siku ya X Mass mwaka 2016 akiwa na miaka 53.
↧
TAZAMA PICHA ZA UJAUZITO WA STAA BEYONCE
↧
MTOTO ANAMPA UCHIZI DJ KHALED

Inasemekana boss wa We The Best Music dj Khaled ana furaha sana kuliko binadamu mwingine yoyote yule Muda huu baada ya ujio wa mwanae Asahd Khaled.
Wiki moja baada ya kuzaliwa Dj Khaleed alimfanya mwanae kuwa Exacutive Producer wa Album yake mpya ya GRATEFUL.
Kama haitoshi Khaleed alimwandikisha mwanae kama mrithi wa mali zake zote Kuwa ndiye mrithi halali unaona jinsi gani mtoto alivyompatia uchizi Dj Khaleed.
Tayari asahd ameshafanya Interview kibao na kupita kwenye Red carpet za Tuzo mbalimbali maarufu ikiwemo Grammy pamoja na I heart Radio.
Asahd amechukua headlines kutoka kwenye mikono ya Baba yake baada ya kumfungilia akaunti katika mtandao wa Instagram caption zake sasa.

Angalia convo za dj Khaleed kwenda kwa mwanae Asahd Khaled imagine mtoto mwenye miezi kadhaa tu anaweza kufanya vituko hivi?

Kinachomfanya Asahd asitulie kabisa home na Mama yake ni Dj Khaled mwenyewe Kuwa na Mapenzi kwa mwanaye kila alipo mshikaji na dogo yupo video kibao utarajie Kumuona akiuza sura Asahd.
Unaambiwa Dj Khaleed ile akaunti ya Instagram ya Asahd ipo chini yake na hivi ndivyo huwa anafanya daily tazama picha.

↧
↧
MSANII TUNDA MAN ANUSURIKA KUCHOMWA KISU HUKO ZANZIBAR

Mkali wa muziki wa Bongo FLeva Tunda Man juu ya kunusurika kuchomwa kisu huko Zanzibar.Inasemekana kuwa chanzo cha vurugu hizo ni kutoelewana kwa Tunda Man na promota ambaye alikuwa amemwita kwenye show visiwani humo.
"mimi sijashikiwa kisu wala sijashika hizo hela na mimi nilienda kule na wife kwa sababu ya spending zangu tu na jamaa walinifata kule kule kwamba sisi tuna show yetu nje kidogo ya Zanzibar na nikaenda pale nika perform na nikaondoka, Sikudai hata sh 10 wala hizo hela sikushika nasikuwaona tena”-Tunda Man
↧
STAA SHILOLE AFUNGUKA KUHUSU UJAUZITO WAKE

Msanii filamu na muziki wa bongo fleva, Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hana ujauzito wowote bali ameridhika na maisha jambo ambalo limefanya aongezeke mwili na kunenepa licha ya watu kuwa na hisia kuwa huenda ana ujauzito.
Shilole amesema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa kumi na moja jioni mpaka saa kumi na mbili kamili.
"Mimi saizi sina ujauzito wowote sema nimenenepa tu maana nimeridhika na maisha haya haya, ukimya wangu ni kwa sababu nilikuwa nazipa ngoma nafasi saizi nimeamua kuja rasmi na wimbo wangu huu 'sitoi kiki' kwani nimegundua Watanzania wanataka burudani, saizi pesa hakuna hivyo nimeona bora nije kuwaliwaza na muziki mzuri huu" alisema Shilole
Mbali na hilo Shilole amesema video ya wimbo huo ataifanya na waongozaji kutoka hapa hapa Tanzania.
↧
MTANGAZAJI DIVA WA CLOUDS FM AMTAMANI LAIVU JOKATE KIMAPENZI

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM Diva amesema kama angekuwa ni Mwanaume angem’date Jokate kwani anavutiwa sana na muonekano wake wa baby face,pia amekiri kuwa alishawahi kumchangia Charity yake.
Mbali na hilo Diva amefunguka na kusema kuwa hawezi kumuomba msamaha Jokate Mwegelo ingawaje yeye alishawahi kumuona mrembo huyo akimrushia maneno kwenye mitandao ya kijamii.
.
.
. “Siwezi kumuomba msamaha Jokate kwa sababu sijamkosea chochote kama yeye alinikosea aje yeye kuniomba msamaha“Alisema Diva
Miezi kadhaa iliyopita @Divathebawse aliwahi kumtaka Alikiba aachane na @Jokatemwegelo akidai kuwa mwanadada Huyo ndio anamtia gundu king wa bongo fleva
↧
MSANII HARMORAPPA AANZA KUMCHOKONOA MSANII AY

Msanii Ay mzee wa commercial ameamua kumuachia jina lake Rapa anayekuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva HamoRappa.
Jina la Legend alikuwa akitumia mzee wa commercial kwenye mtandao wa Twitter lakini sasa ameliachia rasmi kwa rapa huyo mwenye vituko vingi bongo anayeongoza kwa kufuatiliwa kwenye 411 news.
Baada ya HamoRappa kuitambulisha akaunti yake ya Twitter ikiwa na jina la Legend Harmo, jambo liloshtua ulimwengu vipi kwa Zee Legend aliyokuwa akitumia AY.
Mzee wa commercial ameamua kutumia jina la Masta badala ya Lile la Zee Legend ambalo Harmo amelichukua la Legend!
↧
↧
STAA WILL SMITH ATUA BONGO NA KUTEMBELEA MBUGA YA SERENGETI
Tanzania ina ugeni mzito wiki hii.Muigizaji mashuhuri wa filamu, Will Smith amekuja nchini kwaajili ya mapumziko. Staa huyo wa Suicide Squad, yupo kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti akifurahi uumbaji wa Mungu.
Hata hivyo imebainika kuwa Smith si staa pekee wa Marekani aliyepo Tanzania. Supermodel wa Marekani, Chanel Iman naye amejumuika.
Kwenye Instagram, amepost picha akiwa na Will Smith mbugani Serengeti na kuandika: Great places with great friends and Will is One of the coolest.”
↧
SUPERSTAA DIAMOND PLATNUMZ AWACHANA EFM NA CLOUDS FM
Diamond Platnumz amesema kwa sasa redio na TV si vyombo anavyovitegemea sana kwaajili ya promotion pindi anapokuwa akiachia nyimbo.
“Mimi nikiwa natoa nyimbo yangu, promotion yangu siwazi redio wala siwazi TV, ever. Promotion yangu ya kwanza mimi nawaza nyimbo iwafikiaje watu, kuna mitandao ya kijamii, kuna digital platform nyingi,” staa huyo alisema kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz.
Alidai kuwa zama za kundi Fulani la watu likiamua kumrudisha nyuma msanii, halipo tena kwa wasanii wenye nguvu kama yeye.
“Tufute zile ‘naweza nikamdhuru mtu fulani ninavyotaka mimi’ vile vitu havipo tena,” aliongeza.
↧
THE MAGAZETI YA BONGO LEO FRIDAY/IJUMAA 10/03/2017 LIVE
↧
ORODHA YA NCHI 10 ZINAZOPAKANA NA NCHI ZAIDI DUNIANI...TANZANIA IMO

Suala la mipaka ya kimataifa mara nyingi huchukuliwa kama la kisiasa zaidi ya kitamaduni ambapo watu huwa na utaratibu wa kuivuka kihalali au kwa njia za panya. Baadhi ya mipaka inayozigawa nchi duniani huwa rahisi baina ya mataifa, wakati mwingine huwa na uzio, patrols, na vitisho vya vifo au kifungo kwa wasioiheshimu.Worldatlas imetoa orodha ya nchi 10 zilizopakana na nchi nyingi zaidi huku China ikitajwa kuwa na majirani wengi zaidi kwa kuziweka Macau na Hong Kong kama nchi zinazojitegemea licha ya hini ya mamlaka ya China.
10: Turkey – imepakana na nchi nane
Turkey ina-share eneo la pekee katika ramani ya dunia, ikiwa na eneo la kilomita za mraba 756,816 Asia Magharibi (Anatolia) na ardhi ya kilomita za mraba 23,764 Kusini-mashariki ya Europe (Thrace).
Inapakana na nchi nyingi za Europe na Asia na Bahari Nyeusi upande wa kaskazini, kaskazini-mashariki inapakana na Armenia na Georgia, mashariki inapakana na Azerbaijan na Iran, magharibi na kusini-magharibi inapakana na Mediterranean Sea, kusini-mashariki inapakana na Iran na Syria, na kaskazini-magharibi inapakana na Ugiriki na Bulgaria.

9: Tanzania – inapakana na nchi 8
Nchi ya Afrika Mashariki Tanzania ina majirani wanane zikiwemo nchi za Kenya na Uganda upande wa kaskazini, Mozambique, Malawi na Zambia upande wa kusini, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi.

8: Serbia – inapakana na nchi nane
Serbia, nchi iliyopo Kusini-mashariki ya Balkan Peninsula barani Ulaya ni nchi ambayo inapakana na nchi nane pia. Inapakana na Hungary, Bulgaria, Romania, Macedonia, Montenegro, Croatia, Bosnia na Herzegovina.

7: Austria – inapakana na nchi nane
Austria ni nchi inapakana na Jamhuri ya Czech na kaskazini-mashariki inapakana na Slovakia. Mashariki inapakana na Hungary na Slovenia upande wa kusini huku Italy ikiwa upande wa kusini-magharibi. Switzerland na Liechtenstein zipo upande wa magharibi na Ujerumani upande wa kaskazini-magharibi.

6: Metropolitan France – inapakana na nchi nane
Ufaransa inapakana na Luxembourg na Ubelgiji na mashariki inapakana na Italy, Ujerumani na Switzerland, upande wa kusini inapakana na Uhispania na Andorra na kaskazini inapakana na England.

5: Ujerumani – inapakana na nchi tisa
Ujerumani inachangia mipaka yake na nchi 9 ambapo kaskazini inapakana na Denmark, magharibi inapakana na Netherlands, Luxembourg na Ubelgiji na kusini-magharibi kuna Ufaransa. Upande wa mpaka wa kusini inapakana na Austria na Switzerland. Kusiki-mashariki inapakana na Jamhuri ya Czech na mashariki zaidi kuna nchi ya Poland.

4: DR Congo – inapakana na nchi tisa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inapakana na Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Congo, na Sudan. Mashariki inachangia mpaka na Burundi, Uganda, Tanzania na Rwanda huku Zambia ikiwa kusini-mashariki na Angola upande wa kusini-magharibi.

3: Brazil – inapakana na nchi 10
Brazil inachangia mipaka na nchi 10 za Amerika ya Kusini ambazo ni Argentina, Bolivia, Colombia, Venezuela, Uruguay, French Guyana, Paraguay, Guyana, Peru, na Suriname.

Mpaka wa Brazil na Argentina
2: Russia – inapakana na nchi 14
Ikiwa na mipaka inayofikia urefu wa kilomita 20,241 Russia ni nchi ya pili kwa kuwa na majirani wengi zaidi duniani ikipakana na nchi tofauti 14.
Kusini inachangia mipaka na nchi za Korea Kaskazini, Mongolia na China, Georgia, Kazakhstan, na Azerbaijan huku kusini-magharibi na magharibi inapakana na Ukraine, Estonia, Belarus, Latvia, Lithuania, Poland, Norway, na Finland.

Mpaka unaozitenganisha nchi tatu; Russia, China na North Korea
1: China – inapakana na nchi 16
Nchi ya pili kwa ukubwa wa eneo duniani, Jamhuri ya watu wa China inachangia mipaka ya kimataifa na nchi 16 ikiwemo Korea Kaskazini na Urusi upande wa kaskazini-mashariki na Mongolia upande wa kaskazini.
Upande wa kusini inapakana na Indian subcontinent inayojumuisha nchi za India, Bhutan, na Nepal. Vietnam, Laos, na Myanmar ziko upande wa kusini-mashariki na Pakistan upande wa kusini-magharibi.
Mipaka ya magharibi Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, na Tajikistan ambapo mbali na nchi hizi 14 inachangia mpaka na Macau na Hong Kong.

Mpaka baina ya China na Mongolia
↧
↧
WANAWAKE MGODI WA BULYANHULU WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MSAADA KWA WANAFUNZI WA KIKE NA WAGONJWA VITUO VYA AFYA
Wanawake wanaofanya kazi katika Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wameadhimisha siku ya wanawake duniani Machi 8,2017 kwa kutoa zawadi ya baiskeli kwa wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na kuwatembelea na kuwapatia zawadi wagonjwa waliolazwa kwenye vituo vya afya.
Wanawake hao wametoa zawadi ya baiskeli 10 zikiwemo 8 kwa ajili ya wanafunzi waliofanya vyema katika masomo yao katika shule ya Sekondari Bulyanhulu na Bugarama na baiskeli mbili kwa ajili ya walimu wa kike walezi wa wanafunzi hao.
Mbali na kutoa zawadi kwa wanafunzi,pia wametembelea kituo cha afya cha Bugarama na Lunguya vilivyopo jirani na mgodi huo kisha kutoa zawadi ya shuka 70 kila kituo na kuwapa wauguzi na wagonjwa sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake,Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo alisema wameamua kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kuwapongeza wanafunzi wanaofanya vizuri shuleni ili kuwapa ari ya kujifunza zaidi na kuwarahisishia usafiri kufika shuleni.
“Tuwatembelea wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu na Bugarama,tumetoa msaada wa baiskeli 10 hivyo kila shule imepata tano ambapo nne kwa ajili ya wanafunzi kike na moja ni kwa ajili ya walimu wa kike kwa kila shule”,alieleza Senkondo.
“Pia tumetoa shuka 140 kwa ajili ya vituo vya afya viwili,Bugarama na Lunguya kisha kugawa sabuni,mafuta na dawa za meno kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa waliopo katika vituo hivyo”,aliongeza Senkondo.
Senkondo alisema wameamua kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kukutana na watoto wa kike na wanawake ili kuwahamisha wanawake katika jamii kushiriki katika shughuli za migodi kwani wanaweza.
Mwandishi wetu Kadama Malunde,alikuwepo wakati wa maadhimisho hayo,ametuletea picha za matukio yaliyojiri mwanzo hadi mwisho…Tazama hapa chini
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu wakiwa katika shule hiyo iliyopo katika kata ya Kakola halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri kupata zawadi kutoka kwa wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia dhahabu wa Bulyanhulu uliopo jirani na shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 920 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli nne kwa ajili ya wanafunzi wa kike waliofanya vyema katika mitihani yao ili ziwasaidie kurahisisha usafiri kufika shuleni lakini pia baiskeli moja kwa ajili ya mwalimu mlezi wa wanafunzi katika shule hiyo
Kulia ni Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi baiskeli kwa mwalimu mlezi wa wanafunzi katika shule ya sekondari Bulyanhulu ,mwalimu Bumi Mwasalujonja
Mwalimu Bumi Mwasalujonja akiwa amebeba juu baiskeli wakati akikabidhiwa na wanawake kutoka mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu Irene Gimi aliyefanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016 baada ya kupata daraja la kwanza
Mwanafunzi wa kidato cha tatu Irene Gimi akiondoka na baiskeli yake
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akishikana mkono na mwanafunzi wa kidato cha tatu Zainab Kisambale aliyepata daraja la pili katika mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016 na anaongea kwa ufasaha zaidi lugha ya Kiingereza
Wanawake kutoka mgodi wa Bulyanhulu akiwa na wanafunzi wanne waliofanya vizuri katika mtihani
Hapa ni katika shule ya Sekondari Bugarama iliyopo kata ya Bugarama ambayo imejengwa na mgodi wa Acacia Bulyanhulu.Katika shule hii pia wanafunzi wanne wa kike waliofanya vizuri katika masomo yao walipata zawadi ya baiskeli,huku mwalimu wa nidhamu naye akipata zawadi ya baiskeli
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidh baiskeli kwa mwalimu wa nidhamu/mlezi shule ya sekondari Bugarama Prisca Mwanantemi
Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakikabidhi baiskeli kwa mwalimu Prisca Mwanantemi
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akimtambulisha mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule hiyo Jesca Peter ambaye hivi karibuni alifanya vizuri katika mtihani wa majaribio. Mwanafunzi huyo amepata zawadi ya baiskeli
Wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao pamoja na mwalimu wao wakiwa wameshikilia baiskeli zao
Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiondoka katika shule ya sekondari Bugarama yenye jumla ya wanafunzi 766
Hapa ni katika Kituo cha afya Bugarama kilichopo katikakata ya Bugarama halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama.Kituo hiki cha afya kimepewa shuka 70 kwa ajili ya wagonjwa.Kulia ni Muuguzi katika kituo hicho Mwalushani Mabula akizungumza wakati wa kupokea shuka 70,sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno kwa ajili ya wagonjwa waliokutwa katika kituo hicho siku ya siku ya wanawake duniani Machi 8,2017
Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza wakati wa kukabidhi shuka 70 kwa ajili ya wagonjwa lakini pia sabuni,dawa za meno na mafuta ya kujipaka kwa ajili ya wauguzi na wagonjwa katika kituo hicho cha afya
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa Muuguzi kituo cha afya Bugarama Mwalushani Mabula
Wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakikabidhi shuka kwa wauguzi wa kituo cha afya Bugarama
Zoezi la kugawa shuka likiendelea. Kituo cha afya Bugarama kimejengwa na mgodi wa Acacia Bulyanhulu
Wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakielekea katika wodi za wagonjwa kwa ajili ya kuwapatia zawadi ya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akiwa katika wodi ya wazazi akiwaeleza akina mama waliojifungua kuwa wameamua kuwatembelea ili washerehekee kwa pamoja katika siku ya wanawake duniani kwa kuwapatia msaada
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akitoa zawadi ya sabuni kwa Tedy Paul
Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa wamebeba mtoto aliyezaliwa na Salome Raphael baada ya kumpatia zawadi ya vipande 10 vya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa ya meno
Zoezi la kugawa zawadi wodini likiendelea,ambapo kila mgonjwa alipewa vipande 10 vya sabuni,mafuta ya kupaka na dawa ya meno
Ndani ya wodi ya wazazi baada ya kumaliza kutoa sabuni,dawa za meno na mafuta ya kujipaka
Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakifurahia baada ya kutembelea kituo cha afya Bugarama
Wanaendelea kufurahia
Picha eneo la kituo cha afya Bugarama baada ya kutoa zawadi kwa wagonjwa
Hapa ni katika kituo cha afya Lunguya ambapo pia wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu walitoa zawadi ya shuka 70,sabuni,mafuta na dawa za meno kwa ajili ya wagonjwa katika kituo hicho cha afya. Kulia ni Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza katika kituo hicho
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza kabla ya kutoa zawadi hizo.Kulia ni wauguzi katika kituo hicho
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa Afisa tabibu wa kituo cha afya Lunguya,Dkt. John Malongo kwa ajili ya wagonjwa katika kituo hicho
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa wauguzi wa kituo cha afya Lunguya
Akina mama kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakigawa sabuni,mafuta na dawa za meno kwa akina mama ndani wodi ya watoto
Ugawaji wa zawadi unaendelea
Mama akifurahia baada ya kupata zawadi ya sabuni,dawa ya meno na mafuta ya kujipaka
Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakielekea katika wodi nyingine ya wagonjwa
Wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakimpatia zawadi mama aliyelazwa katika wodi ya akina mama
Zoezi la kugawa zawadi likiendelea
Mwanamme anayeuguza mama yake mzazi wodini naye akapewa zawadi ya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa ya meno
Kulia ni Afisa tabibu wa kituo cha afya Lunguya,Dkt. John Malongo akiwaaga wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu
Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiondoka katika kituo cha afya Lunguya
Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiondoka katika kituo cha afya Lunguya baada ya kumaliza kutoa zawadi kwa akina mama na akina baba waliokuwa katika kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
↧
TCCIA INVESTMENT PLC YATOA DARASA KWA WAKAZI WA LINDI NA MTWARA KUHUSU SOKO LA HISA.
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya TCCIA Investment PLC bi Magdalena Mkocha akizungumza na wafanyabiashara mkoani Lindi katika ukumbi wa Double M humo.Bi Mkocha alisema TCCIA Investment ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na mtaji wa shilingi Bilion 1.97 imeweza kukuza mtaji hadi zaidi ya Bilion 28.6 na imekuwa ikilipa gawiwo kwa wanahisa wakeMkochi ameongeza kuwa TCCIA Investment PLC ni kampuni ya uwekezaji wa pamoja, imara na imekuwa ikifanya vizuri sana hivyo amewahimiza wajasiriamali hao kuitumia fursa hii muhimu na adhimu kabla ya March 14 mwaka 2017, ambapo milango ya uuzaji wa hisa hizo itafungwa
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Chemba ya Biashara,viwanda na kilimo, Magdalena Mkocha, amewataka wananchi na wafanyabiashara wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa ya soko la hisa za TCCIA Investment PLC kwa awamu ya awali ambayo inakaribia kuisha.
Hayo ameyasema wakati akizungumza wafanyabiashara kwenye ziara yake ya mikoa ya kusini, Lindi na Mtwara alipokuwa kwenye mikutano ya kuhamasisha ununuzi wa Hisa hizo ambazo zinamilikiwa na kampuni hiyo.
Bi Magdalene Mkocha akifafanua jambo kwa wafanyabiashara waliohudhulia mkutano huo mkoani Lindi
“Nipende kuwahimiza ndugu zangu tuchangamkie fursa hii kwasababu TCCIA Investment PLC nikampuni imara ambayo imeweza kusimama na kujiendesha yenyewe kwa kipindi kirefu bila kutegemea mikopo, sasa imeona ni wakati sasa kuwapa na wananchi nafasi ya kushiriki katika kuchangia mitaji yao ili mwisho wa siku wavune matunda kupitia hisa zao” alisema Bi Mkocha
Mmoja wa wajasiriali waliohudhulia mkutano huo Bwana Condrad Makwiya akiuliza swali kwa bi Mkocha kuhusiana na upatikanaji wa hisa hizo
Hisa za TCCIA Investment PLC zinapatikana kwa shilingi 400 tu, huku kima cha chini cha kununua hisa hizo kikiwa ni hisa 100, pia unaweza kupata hisa hizo kupitia kwa mawakala wa walioidhinishwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) au tembelea kwenye matawi yoyte ya Benki ya CRDB.
Pia unaweza kutumia simu ya mkononi kwa kupiga *150*36# kisha kufuata maelekezo.
Bi Madgalena Mkocha akigawa vipeperushi kwa wafanyabiasha mkoani Mtwara baada ya kumalizka kwa mkutano huo kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Mtwara.
Moja ya mshiriki mkoni Lindi akitoa shukrani zake kwa uongozi wa TCCIA Investment PLC kuhusu fursa hiyo uuzaji wa hisa
↧
KIKAO MAALUM CHA BARAZA KUU LA UVCCM CHA RIDHIA NA KUPITISHA MAPENDEKEZO YA MAREKEBISHO YA KANUNI YA UVCCM
Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika kikao cha kamati ya Utekelezaji kilichoketi mapema ya leo kabla ya kikao cha Baraza kuu Maalum la Uvccm Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma.
Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Sadifa Juma Khamis wa pili kulia akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alipowasili katika kikao cha Baraza kuu Maalum la Uvccm Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma.
Mwenyekiti Wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg:Sadifa Juma Khamis akifungua Kikao cha Baraza Kuu Maalum la UVCCM Taifa kilichofanyika Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Mohammed Seif Khatibu Akizungumza katika kikao cha Baraza kuu Maalum la Uvccm Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma leo.
Ndg:Nyundo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kupitia UVCCM akichangia hoja katika kikao cha Baraza kuu Maalum Kilichofanyika leo Mjin Dodoma.
Mhe: Deo Ndenjembe Mkuu wa Wilaya ya Kongwa akichangia hoja katika kikao cha Baraza kuu Maalum Kilichofanyika leo Mjin Dodoma.
Wajumbe Wa Baraza kuu la UVCCM Taifa
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mariam Ditopile akisikiliza kwa Makini
Wajumbe Wa Baraza kuu wakiwa kikaon
SOMA
MAAZIMIO YA BARAZA KUU MAALUM LA UMOJA WA VIJANA WA CCM TAIFA LILILOKUTANA ALHAMIS TAREHE 9/03/2017 ROYAL VILLAGE HOTEL MJINI DODOMA
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo Alhamis tarehe 9/03/2017 umefanya kikao cha Baraza Kuu la UVCCM Taifa Maalum chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Sadifa Juma Khamis (MCC)(MB) katika Hotel ya Royal Village Hotel Mjini Dodoma.
Kikao kwa kauli moja kimepitisha na kuridhia mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni ya Umoja wa Vijana wa CCM kufuatia maboresho ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi Toleo la 1977 marekebisho ya 2017 na kupeleka katika Vikao vya Chama Cha Mapinduzi Taifa kwa hatua zinazoendelea.
“Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itakuwa na uwezo kwa kushauri, kutoa maagizo ya jumla na maelekezo maalum kwa Jumuiya zinazoongozwa na CCM”.
“Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itathibitisha Kanuni/Katiba ya kila Jumuiya inayoongozwa na CCM marekebisho yake kabla ya kutumika”. Katiba ya CCM ya 1997 Toleo la 2012 uk. 191 kifungu (4) na sura ya (5).
Kufuatia kikao Maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM na kuzingatia mambo yafuatayo:-
Mabadiliko ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake yana lengo la kukiimarisha Chama chetu ili kuzidi kuziteka hisia, mioyo na fikra za Watanzania walio wengi kwa nia ya kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika lengo lake la kushika dola na kuleta maendeleo endelevu.
Kupunguza idadiya wajumbe ili kuwa na michango makini kwenye vikao vyetu ili kuweza kuwajengea na kuwatetea Vijana wakulima na wafanyakazi na wale walio katika sekta binafsi ili wanufaike na masuala ya Kiuchumi, kijamaii na Kisiasa kulingana na fursa zilizopo kama zilivyoainishwa na kuelekezwa na sera za CCM katika misingi ya kujitegemea.
Mabadiliko haya yatasaidia sana kupunguza migogoro isiyo na msingi katika Jumuiya inayotokana na Vikao vya Kikanuni.
Aidha Umoja wa Vijana wa CCM unaahidi kwa CCM kufanyia kazi maagizo na maelekezo yote yatakayotolewa kwa lengo la kufikia kwa vitendo dhana ya CCM mpya, Tanzania mpya wakati Jumuiya hiyo ikielekea kutimiza miaka 40 toka kuzaliwa na kumepiga hatua kubwa za mafanikio Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.
Mwisho UVCCM imempongeza kwa dhati Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa umakini, uhodari, ushupavu na kusimamia vyema Ilani ya Uchaguzi wa CCM sambamba na azma yake ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
PICHA NA FAHADI SIRAJI
↧
ANGALIA VIDEO DIAMOND PLATINUMS AKUFUNGUKA TENA KUHUSU KAZI ZA WASANII WA BONGO,AFICHUA MAZITO
↧
↧
SUPERSTAA DIAMOND PLATNUMZ AZINDUA TOVUTI MPYA YA KUUZA MZIKI,"WASAFI.COM"
Tovuti namba moja ya kuuzia muziki nchini, Mkito.com, imepata mpinzani mpya, Wasafi.com. Diamond Platnumz ameizindua rasmi website yake ya kuuzia muziki, si tu wa wasanii wa WCB, bali wasanii wengine pia.
Wiki hii, hitmaker huyo wa Marry You, amekuwa akifanya mikutano ofisini kwake na wasanii mbalimbali, kuzungumza namna ya kufanya nao kazi kwenye mradi huo. Tayari amekutana na wasanii kama Ben Pol, Barnaba, Cassim pamoja na Chege na Temba.
Kwa mwelekeo huo, Wasafi.com inakuja kuwa mpinzani mkubwa wa Mkito.com, ambayo hadi sasa ndio website inayotegemewa na wasanii wengi kuuzia nyimbo zao.
Msanii wa WCB, Harmonize anaachia wimbo wake mpya exclusively kupitia website hiyo inayokuja na app yake pia.
↧
HARMORAPA NA AMBER LULU WAKINUKISHA VIBAYA, WAFANYA MAMBO YA AJABU LIVE
Harmorapa and Ambalulu on Heard line Today.
Many of us live a full life. A life filled with so many
experiences, creating so many wonderful memories and lessons and wisdom.
BOFYA HAPA KUONA PICHA WALICHOFANYA LIVE
Many of us live a full life. A life filled with so many
experiences, creating so many wonderful memories and lessons and wisdom.
BOFYA HAPA KUONA PICHA WALICHOFANYA LIVE
↧
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA ENEO LENYE MGOGORO LA PORI TENGEFU LA LOLIONDO.
Msafara wa Magari ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Malisili na Utaalii,yakpita katika maeneo mbalimbali ya Pori Tengefu la Loliono kwa ajili ya kujionea hai halisi ya mgogoro ulioo katika eneo hilo.
Mwenyekii wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi ,Maliasii na Utalii,Atashasta Ndetiye (katikati) akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo kutizama vyanzo vya maji vilivyoko katika Pori Tengefu la Loliondo.
Waziri wa Malisili na Utalii ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo,Prof Jumanne Maghembe akiongozana na wataalamu katika ziara ya kamati hiyo.
Mtafiti Mkuu wa Idara ya Ikolojia (TAWIRI) Dkt Edward Khoi akitoa maelezo ya kitaalamu kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Ardhi,Malisili na Utalii wakati wakitembela Pori tengefu la Loliondo.
Baadhi ya wajumbe wa kamato hiyo wakifuatilia maelezo kutoka kwa wataalamu wa Ikolojia na Uhifadhi.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema akiwaeleza wajumbe w kamati hiyo madhara yatakayojitokea endapo eneo la Pori Tengefu la Loliondo halita hifadhiwa.
Wajumbe wa Kamati ya Maliasili na Utalii,wakitizama eneo linalotajwa kutengenezwa na wafugaji kwa ajili ya kunyweshea maji mifugo yao ndani ya Pori Tengefu la Loliondo.
Eneo linalouiwa na wafugaji unyweshea mifgo yao.
Sehemu ya Mabirik yanayotajwa kutengenezwa na jamii ya wafugaji kwa ajili ya kunywesha mifgo yao.
Mwenyekiti a Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii,Atashsta Ndetiye (kulia) pamoja na Waziri wa Malisili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe wakitizama eneo ambalo i mapiio ya maji katik Pori Tengefu la Loliondo.
Moja ya Makundi ya Ng'ombe yaliyokutwa na Kamati hiyo katika Pori Tengefu la Loliondo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakizungumza na mmoja wa wafugaji waliokutwa wakichunga Ngombe ndani ya Pori Tengefu la Loliondo.
Kamati ilikutana pia na Changamoto ya uboovu wa Miundombinu ya barabara hali iliyolazimu magari kupita kwa tahadhari .
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakitizama moja kati ya vyanzo vy maji vinavyotiririsha maji yake katika mto Gurumeti uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mbunge wa Jimbo la Sumve ambaye pia ni mjube wa kamati hiyo,Richard Ndasa akizungumza jambo mara baada ya kutizama moja ya vyanzo vya maji vilivyoko katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.
Sehemu ya Makundi ya Mifugo pamoja na Mashamba yaliyopo katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazinia
↧