↧
SIRI ZAANZA KUFICHUKA KUMBE JACKY CLIFF ALICHOMWA NA WATU WAKE WA KARIBU SANA SOMA HAPA HABARI YAKE LIVE!!
↧
Kocha Ahly agoma kujiuzulu, aisubiri Yanga
KOCHA Mkuu wa Al Ahly ya Misri, Mohammed Youssef, ameziba masikio na kutupilia mbali kelele za mashabiki wanaomshinikiza ajiuzulu kutokana na matokeo mabaya na kesho Jumatano anaiingiza timu kambini.
Ahly inajiandaa na msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa ambapo itaanza na Yanga mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam, lakini kesho kutwa Alhamisi itacheza mechi ya ‘Super Cup’ dhidi ya Safaxien ya Tunisia nchini Misri kwenye Uwanja wa Cairo.
Mechi hiyo ni kuashiria mwanzo wa msimu mpya wa mashindano ya kimataifa na hukutanisha bingwa wa Kombe la Shirikisho na wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.
Mashabiki wa Al Ahly wanahofia kwamba mwenendo wa timu hiyo katika ligi yao ya ndani usije ukaiathiri na kukumbana na kipigo cha aibu kutoka kwa Yanga na wakaondoshwa mapema na kuwa timu ya pili ya Misri kuondoshwa mashindanoni na timu ya Tanzania ikiwa bingwa mtetezi. Simba iliitoa Zamalek mwaka 2003 wakati Wamisri hao wakiwa mabingwa watetezi.
Kocha huyo alisema kwamba kujiuzulu siyo hoja ya msingi kwa sasa kwa vile timu hiyo inayumba kutokana na majeruhi waliomo, ingawa kocha wa Yanga, Hans Pluijm, amedai hiyo ni danganya toto tu ili wajisahau.
Akizungumza baada ya mchezo wao wa mwisho uliopigwa wikiendi iliyopita dhidi ya vibonde katika kundi lao El Gounah ambapo Al Ahly ilipokea kipigo cha bao 1-0, Youssef alisema licha ya kikosi chake kupokea kipigo cha tatu tangu kuanza kwa ligi hiyo, matokeo ambayo yaliwashusha mpaka nafasi ya tatu, hana mpango wa kuachia ngazi.
Youssef alisema kwa sasa kikosi chake kinapita katika wakati mgumu na wanasumbuliwa na tatizo la majeruhi ambao ni kiungo mshambuliaji, Walid Soliman na mabeki wao wa pembeni; Ahmed Fathi na Sayed Moawad.
Alisema bado timu yake ina nafasi ya kurudisha makali yao ambapo amewataka wachezaji wake kusahau matokeo ya mchezo huo haraka na kujikita katika kuangalia michezo ya Ligi ya Mabingwa.
“Sina mpango wa kujiuzulu kwa sasa, nitabaki kuondoa changamoto tunazokutana nazo kwa sasa, nataka wachezaji wangu kusahau kila kitu kuhusu kufungwa kwetu katika mchezo uliopita, nawaamini wachezaji wangu wanao uwezo mkubwa wa kuirudisha timu katika mwendo mzuri,” alisema Youssef.
“Najua kwamba kuna presha kubwa kwa wachezaji wangu hasa katika hiki kipindi kigumu ambacho tunachopitia, tuhahitaji kupewa muda kuwa sawa, huu ni mchezo wa soka lolote linaweza kutokea wakati wowote.”
Yanga itamtuma kocha msaidizi wake, Boniface Mkwasa, kwenda Cairo kuiangalia mechi hiyo ya Super Cup.
-mwanaspoti
-mwanaspoti
↧
↧
MAJANGAZII....Denti wa Darasa la 5 Afungwa Minyororo na Shangazi yake ili Atumike Kishirikina..!!
KATIKA hali ya kushangaza, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Dorah Joseph (34) anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kutuhumiwa kumfunga mnyororo mtoto wa kaka yake aitwaye Happy Joseph (13) na kumtelekeza bila kumpatia huduma muhimu, ikiwemo chakula.
Kwa mujibu wa majirani na mashuhuda, kisa cha mwanamke huyo kufanya kitendo hicho cha kikatili, ni katika harakati zake za kutaka kumtumia mtoto huyo kishirikina ili aweze kujipatia mali.
Akizungumza muda mfupi baada ya kufika kituoni hapo, mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Eleray alisema shangazi yake huyo amekuwa akimfanyia ukatili wa kutisha akishirikiana na jirani yake ambaye jina lake linahifadhiwa.
Happy alisema wazazi wake wote walishafariki, hivyo kumfanya yeye na dada yake kuishi kwa shangazi yake huyo, aliyemwelezea kama amekuwa akimtesa kwa kumnyima chakula, kumpiga, kumfunga mnyororo na kumfungia ndani kama mbwa.
Akizungumzia tukio hilo, Askari wa Dawati la Jinsia, Deborah alisema ukatili uliofanywa na dada huyo kwa mwanafunzi huyo hauelezeki na kwamba wanakamilisha mashtaka ili kumfikisha mahakamani ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo walifika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo ambaye hadi anafikishwa polisi, alikuwa bado na mnyororo mguuni kutokana na kukosekekana kwa ufunguo wa kufungua kufuli kubwa mguuni kwake.
Kwa upande wake, mtuhumiwa huyo alisema alilazimika kumfunga mnyororo binti huyo baada ya kuchoshwa na tabia yake ya kuzurura ovyo, kwani muda mwingi anatoroka nyumbani na kwenda kusikojulikana.
Kwa mujibu wa majirani na mashuhuda, kisa cha mwanamke huyo kufanya kitendo hicho cha kikatili, ni katika harakati zake za kutaka kumtumia mtoto huyo kishirikina ili aweze kujipatia mali.
Akizungumza muda mfupi baada ya kufika kituoni hapo, mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Eleray alisema shangazi yake huyo amekuwa akimfanyia ukatili wa kutisha akishirikiana na jirani yake ambaye jina lake linahifadhiwa.
Happy alisema wazazi wake wote walishafariki, hivyo kumfanya yeye na dada yake kuishi kwa shangazi yake huyo, aliyemwelezea kama amekuwa akimtesa kwa kumnyima chakula, kumpiga, kumfunga mnyororo na kumfungia ndani kama mbwa.
Mtoto Happy Joseph (13).
‘’Shangazi ananitesa sana, ananifunga mnyororo kama mbwa na kunifungia chumbani, hanipi chakula wala kunipeleka shule, nina zaidi ya mwaka sasa sijaenda,” alidai Happy.
Aliongeza kuwa tofauti na dada yake, yeye ndiye amekuwa akiteswa huku ndugu zake wakizuiwa kumuona.
Akizungumzia tukio hilo, Askari wa Dawati la Jinsia, Deborah alisema ukatili uliofanywa na dada huyo kwa mwanafunzi huyo hauelezeki na kwamba wanakamilisha mashtaka ili kumfikisha mahakamani ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo walifika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo ambaye hadi anafikishwa polisi, alikuwa bado na mnyororo mguuni kutokana na kukosekekana kwa ufunguo wa kufungua kufuli kubwa mguuni kwake.
Kwa upande wake, mtuhumiwa huyo alisema alilazimika kumfunga mnyororo binti huyo baada ya kuchoshwa na tabia yake ya kuzurura ovyo, kwani muda mwingi anatoroka nyumbani na kwenda kusikojulikana.
↧
KWELI MAJANGAZI...KUMBE ASILIMIA 90 YA WA TZ..WANA LALA STOO..CHEKI HAPA LIVE...
↧
MCHEKI HUYU MBULULAZ AKIWA KWENYE JAKUZI..LIVEEE
↧
↧
ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KWENYE MABANDA YA KUHIFADHIA CHUI
Mwanamume mmoja nchini China amenusurika kifo katika hifadhi ya wanyama pori nchini humo, baada ya kujirusha ndani ya hifadhi hiyo akisema alitaka 'kuwalisha' wanyama hao hatari.
Mwanamume huyo alitaka kujitoa uhai kwa kujirusha ndani ya chumba cha kuhifadhia Chui wakubwa wenye Milia au Tiger katika hifadhi ya wanyamapori nchini China.
Wageni waliopigwa na mshangao, walitizama mwanamume huyo aliyejulikana tu kama Yang Jinhai, mwenye umri wa miaka 27 akiumwa, kugwaruswa na kubururwa na wanyama hao kabla ya walinzi kumuokoa.
Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la China, Chengdu, watalii waliokuwa katika hifadhi hiyo walidhani kuwa bwana Yang alikuwa mmoja wa wafanyakazi wa hifadhi hiyo kwani walioshuhudia wanasema walimuona akibeba begi mabegani na kupanda mti kama aliyetaka kuwalisha wanyama hao wakubwa.
Lakini baada ya watalii kuanza kumpigia mayowe wakimtaka arejee, bwana Yang alijirusha kutoka mtini na kuanguka ndani ya sehemu walimokuwa wamefungiwa Chui hao.
Watalii hao walisema kuwa Yang alijirusha akitaraji kuwa Chui hao wangemshambulia na kumuua , lakini wanyama hoa waliokuwa Chui Milia Dume na Jike walionekana kushtuka zaidi kwa kumuona Yang huku Chui jike akitoroka kuliko kutaka kumla Yang.
"bwana Yang alionekana akijaribu kuwafanyia vitendo vya kuwakasirisha ili wanyama hao waweze kumshambulia lakini hakufanikiwa. Hatimaye Chui Dume alimshambulia Yang baada ya kushikwa na hasira na kuanza kumuuma na kumgwara lakini aliokolewa na walinzi wa hifadhi hiyo.
Yang alipata matibabu lakini baada ya kutibiwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa nia yake ilikuwa 'kuwalisha wanyama hao.'Familia ya Yang ilisema kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili na kuwa walikuwa wamepanga kumpeleka hospitalini kwa ushauri nasaha,.
Walinzi wa hifadhi hiyo walisema kuwa Yang alikuwa na bahati mno kuweza kunusurika kifo.chanzo bbc swahili
↧
NI KUFA AMA KUPONA LEO MAN CITY V/S BARCELONA
↧
KWELI HUYU MZUNGU KIBOKO ...AAMUA KUWA BODABODA...SERIKALI YA CHACHAMAA NAKUMRUDISHA KWAO POLAND
↧
KWA MARA YA KWANZA MSHINDI WA MISS TANZANIA BEAUTY CONTEST USA KWENDA BONGO KUSHIRIKI REDD'S MISS TANZANIA 2014
KWA MARA YA KWANZA MSHINDI KWENDA KUIWAKILISHA USA KWENYE MASHINDANO YA REDD'S MISS TANZANIA 2014 - JIJINI DAR-ES-SALAAM
MSHINDI WA 1,2,3 KILA KANDA KUJA DC KWENYE FINALS AMBAPO
MKURUGENZI NA MWAKILISHI WA MISS TANZANIA KUTOKA TANZANIA WATAKUWEPO KUTOA TAJI HILO.
MSHIRIKI LAZIMA AWE NA MAKARATASI YA KUSAFIRIA
VENUES & REGISTRATION -DROPPING NEXT
MAELEZO-TUANDIKIE ## MISSTANZANIA2014@GMAIL.COM
↧
↧
LE MUTUZ BACK IN ACCRA POSING WITH MY BOSS HERE IN GHANA MR. KENPONG NA GARI LAKE LA USD $ 500,000 MAYBACH 2014 I LOVE IT U KNOW!!
↧
HABARI ZA KWANZA ZA MWANAFUNZI KUJINYONGA LIVE SOMA SABABU!!
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Ualimu cha Winneba, nchini Ghana, amejiua kwa kujinyonga mara baada ya jina lake kubandikwa kwenye ubao wa matangazo (notice board) kuwa amefeli masomo matatu.
Jina la mwanafunzi huyo limehifadhiwa kwa sasa, ila inasemwa kuwa sababu ya kujinyoga kwake ni kutokana na kufeli masomo hayo matatu ambapo kungepelekea kufutwa kwake shule hapo.
Sababu hasa ya kifo chake haijajulikana moja kwa moja ila inaaminika ilitokana na hofu ya kutimuliwa chuoni hapo kutokana na kufeli mitihani mitatu.
Wilson Dabuo, ambaye ni muwakilishi wa wanafunzi kwenye baraza la chuo hicho, alieleza kupitia Joy News kwamba chuo hicho kina sheria ya kutimua wanafunzi wanaofeli masomo matatu kwenye mitihani yao
Jina la mwanafunzi huyo limehifadhiwa kwa sasa, ila inasemwa kuwa sababu ya kujinyoga kwake ni kutokana na kufeli masomo hayo matatu ambapo kungepelekea kufutwa kwake shule hapo.
Sababu hasa ya kifo chake haijajulikana moja kwa moja ila inaaminika ilitokana na hofu ya kutimuliwa chuoni hapo kutokana na kufeli mitihani mitatu.
Wilson Dabuo, ambaye ni muwakilishi wa wanafunzi kwenye baraza la chuo hicho, alieleza kupitia Joy News kwamba chuo hicho kina sheria ya kutimua wanafunzi wanaofeli masomo matatu kwenye mitihani yao
↧
LE BIG SHOW WITH WASHIKAJI MACHINGAZ AT ACCRA MARKET GHANA IYO LIVE!!
↧
NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AIOMBA MAHAKAMA KUU IITUPILIE MBALI KESI YA KIKATIBA INAYOMKABILI WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA
NAIBU Mwanasheria Mkuu, Mhe George Masaju (pichani) amedai mahakamani katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) dhidi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba kwa mujibu wa katiba mamlaka ya mahakama kuingilia mwenendo wa bunge yameondolewa.
Pia, Mhe Masaju amedai kuwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi bunge halina mamlaka ya kuingilia mwenendo wa mahakama na kwamba kesi iliyopo mahakamani haina mashiko ya kisheria hivyo mahakama iitupilie mbali.
Kesi hiyo ya Kikatiba inasikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu, likiongozwa na Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, akisaidiana na Jaji Augustine Mwarija na Dk. Fauz Twaib.
Mhe. Masaju alitoa madai hayo jana wakati akijibu hoja za upande wa walalamikaji kwamba kesi iliyopo mahakamani ina mashiko ya kisheria.
“Watukufu majaji, kwa mujibu wa kifungu cha 4 kidogo cha 4 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinaeleza kwamba kila chombo kitaundwa na kutekeleza majukumu yake… mahakama haina mamlaka ya kuingilia mwenendo unaotokea bungeni na kwa utaratibu huo, wabunge wanazuiliwa kujadili masuala yaliyoko mahakamani” alidai Mhe Masaju.
Mbali na Mhe Masaju upande wa walalamikiwa, mawakili wengine ni, Mawakili wa Serikali Wakuu, Gabriel Marata, Sara Mlipano na Alesia Mbuya.
Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa leo ambapo upande wa walalamikiwa watato hoja zao. Katika madai ya msingi LHRC na TLS waliwasilisha madai mahakamani wakidai wanapinga kauli iliyotolewa na Mhe. Pinda bungeni, Juni 20, mwaka huu, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo.
Mhe.Pinda anadaiwa kutoa kauli inayolalamikiwa alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyetaka kujua msimamo wa serikali na mambo mengine, malalamiko dhidi ya vyombo vya dola katika baadhi ya maeneo kama Mtwara, kuwapiga wananchi.
↧
↧
PANDU KIFICHO ACHAGULIWA MWENYEKITI WA MUDA WA BUNGE LA KATIBA
↧
BARCELONA YAICHAKAZA MAN CITY BAO 2-0
↧
HAWA NDO MATAJIRI WAKUBWA TANZANIA NA VYANZO VYAO VYA MAPATO VIKO HAPA....
R. Mengi |
WAFANYABIASHARA watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz, Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo matajiri zaidi nchini.
Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni). Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni).
Matajiri hao wamepatikana baada ya kuangalia nafasi zao kifedha, ufanisi wa kampuni zao katika soko la hisa, mfumo wa wanahisa katika soko la hisa na mtiririko mzima wa fedha katika akaunti zao kwenye benki mbalimbali.
Jarida hilo linalotoka mara moja kwa mwezi kutoka Afrika Magharibi, limesema matajiri hao wa Tanzania ni kati ya Waafrika wenye utajiri ambao ni mabilionea 4,800 kutoka mataifa 17.
Asilimia kubwa ya watu 1,523 ni mamilionea na wamo katika ripoti ya watu matajiri Afrika.
Jarida hilo linataja jinsi matajiri hao walivyokuwa wajasiriamali wadogo kabla ya kuibuka na kuwa mabilionea.
Said Salim Bakhresa
Jarida hilo limesema chanzo cha utajiri wa Bakhressa ni mapato yanayotokanana uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye viwanda vyake.
Mfanyabiashara huyo aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanzisha biashara zake. Alianza kuuza urojo Zanzibar na baadaye alifungua mgahawa miaka ya 1970.
Mgahawa huo ulipanuka na alitumia faida yake kufungua mashine ya kusaga pamoja kiwanda za usindikaji vyakula, huku akiunda Kundi la Makampuni ya Bakhressa.
Aliendelea kusindika vyakula mbalimbali na kutengeneza unga wa mahindi na baadaye kuanzisha kiwanda cha kuoka mikate na baadaye kutengeneza chocolate, ice cream, vinywaji na makasha ya kufungashia bidhaa. Kutokana na shughuli hizo, kwa mwaka huingiza Sh800 milioni.
Kampuni zake kwa sasa zinafanya biashara mbalimbail katika nchi za Tanzania, Uganda, Malawi, Rwanda na Msumbiji na ameajiri zaidi ya wafanyakazi 2,000.
Gulam Dewji
Mfanyabiashara huyo ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 560 milioni kutokana na kuzalisha bidhaa na kutoa huduma mbalimbali.
Ni mmoja wa mataikuni wa Tanzania tangu miaka ya 1970 na kazi yake kubwa ilikuwa kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka nje.
Alianza na kampuni ndogo aliyoiita Mohammed Enterprises Tanzania, ambayo kwa sasa ni kati ya kampuni kubwa Afrika Mashariki na Kati.
Miongoni mwa mali zake ni Kiwanda cha 21st Century Textiles, moja ya viwanda vikubwa vya nguo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kampuni yake ina viwanda vinne, Tanzania na Msumbiji huku ikizalisha Dola 100 milioni kwa mwaka. Pia kampuni hiyo husindika juisi kwa matunda ya Tanzania, mafuta ya kula, sabuni na tishu.
Kampuni hiyo pia inamiliki kampuni ya bima, makontena, kampuni za kuuza mafuta ya petroli na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali zaidi ya 100 Tanzania nzima.
Hata hivyo, Gulam alisema jana kwamba takwimu zilizotolewa zimekosewa. Alisema kwa sasa yuko nje ya Dar es Salaam na atatoa taarifa sahihi atakaporejea.
“Kuna baadhi ya tarakimu zimekosewa niko Morogoro kuangalia biashara zangu nikirudi Dar es Salaam nitazungumza,” alisema Dewji.
Rostam Aziz
Ameelezwa kuwa utajiri wake umetokana na kuendesha shughuli zake mbalimbali ikiwamo kampuni za mawasiliano ya simu, madini na biashara za usafiri wa meli.
Mwanasiasa huyo mwenye asili ya Asia, alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa Igunga mwaka 1993 na alishinda kwa vipindi viwili.
Aliachana na ulingo wa siasa mwaka 2011. Anamiliki asilimia 19 ya Hisa za Kampuni ya Vodacom ambayo ina wateja zaidi ya milioni nane.
Ameelezwa pia kuwa anamiliki Kampuni ya Ujenzi ya Caspian na sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Hutchison Whampoa ya Hong Kong.
Akizungumzia utafiti huo, alisema: “Umefanyika kwa umakini isipokuwa tu kwa upande wangu wanasemas ninamiliki asilimia 19 ya Kampuni ya Vodacom kitu ambacho si sawa kwani ninamiliki asilimia 35.”
Reginald Mengi
Mengi anakimiliki kampuni mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, viwanda vinavyozalisha vinywaji baridi vya Coca-Cola na ana mgodi wa dhahabu.
Mfanyabiashara huyo baada ya kufanya kazi ya uhasibu ambayo ndiyo taaluma yake, alifanya biashara ya kutengeneza kalamu za wino zilizopata soko kubwa Afrika Mashariki.
Leo hii, IPP Group ambayo Mengi ni mwenyekiti wake, inamiliki magazeti mbalimbali ikiwemo Financial Times, ThisDay na The Guardian, televisheni mbili kubwa Afrika Mashariki na Kati EATV na ITV na vituo vya redio. Anamiliki Kampuni za IPP Gold na Handeni Gold.
Ali Mufuruki
Utajiri wake unatokana na biashara mbalimbali za rejareja na za ushirika.
Ni mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Infotech Investment Group.
Kampuni hiyo inajumuisha Watanzania na Waganda kwa ajili ya kuuza bidhaa za Afrika Kusini za Woolworth.
Ni mmoja wa waanzilishi wa taasisi mbalimbali ikiwemo East Africa Capital Partners, vyombo vya habari, sekta ya mawasiliano ikiwamo Venture Capital Fund Manager na nyingine katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Afrika Mashariki.
Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mwananchi Communications Limited, Benki ya Stanbic, Mwenyekiti wa Africa Leadership Initiative East Africa Foundation.
Akizungumzia taarifa hiyo, Mufuruki aliwapongeza waliotajwa kuwa ni matajiri.
“Ningefurahi sana kama ningekuwa na utajiri huo lakini kwa upande wangu naona kwangu kuna tatizo la taarifa kwani walizotoa si sawa,”alisema Mufuruki na kuongeza;
“Sizungumzii watu wote waliotajwa, bali nazungumzia mimi mwenyewe ‘data’ walizotoa si sawa kwa upande wangu.”
Hata hivyo, alisema anafurahi kuona watu wanaanza kuzungumzia utajiri wa watu wengine ‘in a positive way’ (kwa mrengo chanya) na si vinginevyo.
↧
TAZAMA PICHA ZA JENGO AMBALO LIPO CHINI YA MAJI KWA KINA CHA FUTI 130 NA LENYE MIAKA 50 NCHINI CHINA
A maze of white temples, memorial arches, paved roads, and houses... hidden 130 feet underwater: this is China's real-life Atlantis.The so-called Lion City, tucked in a lake between the Five Lion Mountain, was once Shi Cheng - the centre of politics and economics in the eastern province of Zhejiang.But in 1959, the Chinese government decided a new hydroelectric power station was required - so built a man-made lake.
Classical: The structures in Shi Cheng were built 1,300 years ago featuring traditional Chinese statues. Away from the wind and sun, it has remained intactWatch video
Hidden: The city was once a political and economic hub for eastern China but after authorities built the man-made Qiandao Lake in 1959, it is nowhere to be seen
Divers have rediscovered the opulent city and plan to bring tourists round
Carvings: Visitors will be able to see the traditional engravings first-hand when guided by Qiu Feng and her team
Before: This is a sketch of the city dating back hundreds of years, showing people pacing the streets and goods being carted in on horseback
↧
↧
AMINI USIAMINI HII NDIO THE BEST WEDING DANCE, HAIJAWAHI KUTOKEA DUNIANI KOTE:
↧
PICHA WAGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA WALIPORUDISHA FOMU ZAO LEO
Mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo la Kalenga kupitia CCM; Bw. Godfrey Mgimwa alipokuwa anatoka baada ya kukamilisha zoezi lake la kurudisha fomu hiyo.
Mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo la Kalenga kupitia CHADEMA; Bi Grace Tendega alipokuwa anatoka baada ya kukamilisha zoezi lake la kurudisha fomu hiyo ya ugombea.
Na Riziki Mashaka.
WAGOMBEA WA NAFASI YA UBUNGE KATIKA JIMBO LA KALENGA KUTOKEA VYAMA VYA CCM NA CHADEMA WALIPOKUWA WANARUDISHA FOMU HIZO LEO KATIKA UKUMBI WA SIASA NI KILIMO KATIKA ENEO HILO LA MANISPAA YA IRINGA, MWAKILISHI WA CCM NI GODFREY WILLIUM MGIMWA NA KUPITIA CHADEMA NI GRACE TENDEGA AMBAO WOTE WATAANZA KAMPENI ZAO SIKU YA KESHO YA TAREHE 19/02/2014↧
THE BONGO & MAJANGAZ:- MCHAWI AANGUKA USIKU AKIWANGA NA KUGEUKA KUKU KAMA KITOKOLOLO ONA HAPA LIVE!!
HALI ya taharuki iliyoambatana na imani za kishirikina iligubika Jiji la Arusha kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina kudondoka na ungo wa kishirikina asubuhi ya Ijumaa iliyopita kisha ghafla kubadilika kuwa kuku mweupe mwenye mayai ndani ya ungo, Uwazi limeona mengi
Mamia ya wananchi katika eneo la Kimandolu kando ya Barabara ya Arusha- Moshi walimiminika kushuhudia tukio hilo lililojiri saa tatu asubuhi.
Akizungumza na Uwazi, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye ni dereva wa bodaboda, Martin Mbise alisema:
“Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila siku, ghafla niliona kitu kipana kikidondokea kwenye huu mtaro, ndani yake nikamwona mtu amekaa akiwa uchi wa mnyama.
“Wengi tuliamua kusogelea eneo la tukio, lakini kabla hatujakifika, mtu huyo alitoweka, badala yake mle mwenye ungo mkawa na kuku mweupe na mayai zaidi ya kumi, tulishangaa sana:
Mbise alisema hali hiyo ilidumi kwa saa mbili na nusu, ndipo wananchi hao wakaamua kumchoma moto kuku huyo baada ya kumuua na kuyavunja mayai.
Hata hivyo, alisema haikuwa rahisi kuku huyo kuungua licha ya kumwagiwa mafuta ya taa na petroli na wakachukua uamuzi wa kumkatakata na kugawana nyama yake huku baadhi
yao wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema tukio hilo ni laana na anapaswa kuitwa mtumishi wa Mungu kwa ajili ya kukemea pepo mchafu kwa maombi ya kiroho wakiamini mchawi huyo alikuwa ana lengo la kuwadhuru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Lebaratus Sabas hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini baadhi ya maafande waliofika katika eneo hilo walithibitisha.
Chanzo:.globalpublishers
Mamia ya wananchi katika eneo la Kimandolu kando ya Barabara ya Arusha- Moshi walimiminika kushuhudia tukio hilo lililojiri saa tatu asubuhi.
Akizungumza na Uwazi, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye ni dereva wa bodaboda, Martin Mbise alisema:
“Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila siku, ghafla niliona kitu kipana kikidondokea kwenye huu mtaro, ndani yake nikamwona mtu amekaa akiwa uchi wa mnyama.
“Wengi tuliamua kusogelea eneo la tukio, lakini kabla hatujakifika, mtu huyo alitoweka, badala yake mle mwenye ungo mkawa na kuku mweupe na mayai zaidi ya kumi, tulishangaa sana:
Mbise alisema hali hiyo ilidumi kwa saa mbili na nusu, ndipo wananchi hao wakaamua kumchoma moto kuku huyo baada ya kumuua na kuyavunja mayai.
Hata hivyo, alisema haikuwa rahisi kuku huyo kuungua licha ya kumwagiwa mafuta ya taa na petroli na wakachukua uamuzi wa kumkatakata na kugawana nyama yake huku baadhi
yao wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema tukio hilo ni laana na anapaswa kuitwa mtumishi wa Mungu kwa ajili ya kukemea pepo mchafu kwa maombi ya kiroho wakiamini mchawi huyo alikuwa ana lengo la kuwadhuru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Lebaratus Sabas hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini baadhi ya maafande waliofika katika eneo hilo walithibitisha.
Chanzo:.globalpublishers
↧