Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live

LIVEEEE!! ABAMBWA AKIIBA KANISANI,WAUMINI WAGEUZA BUCHA MWILI WAKE

$
0
0
Kijana anayejulikana kwa jina moja la Emmanuel (30), amejikuta akipokea kipigo ‘hevi’ baada ya kukamatwa akiiba katika Chuo cha Theofilo Kisanji ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dar.
Emmanuel baada ya kupokea kichapo cha nguvu kutoka kwa wanachuo.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kanisani hapo, mchana kweupe ambapo jamaa huyo ambaye amekuwa akifika mahali hapo mara kwa mara, alijikuta arobaini yake ikitimia na hivyo kutiwa mikononi mwa wanachuo ambao kabla ya kuhoji zaidi, walimshushia kipigo cha mbwa mwizi.
Wanachuo wakikagua baadhi ya
vitu alivyokutwa navyo Emmanuel.
“Huyu ndiye huwa anatuibia humu chuoni na kanisani, kila siku watu wanalalamika kuibiwa vitu vyao. Juzi tu, kuna watu waliibiwa simu, wengine fedha lakini hatukujua ni nani aliyekuwa akitufanyia hivyo, sasa huyu tutamkomesha,” alisema dada mmoja huku akiwa na furaha ya kukamatwa kwa jamaa huyo.
Emmanuel akiwa mikononi mwa wanachuo wenye hasira.
Wanachuo hao, wakionekana kupania kumfundisha adabu na kumwachisha Emmanuel udokozi, walikuwa wakimhoji maswali huku wakimwangushia kipigo mfululizo, hali iliyosababisha mwili kutoka damu nyingi iliyotapaa sakafuni kama buchani.
Emmanuel akiwa na vitu vya wizi alivyokutwa navyo.
Kama kawaida, mapaparazi wetu hawakutaka kuishia kuangalia kipigo tu, waliwaita baadhi ya wanachuo walioibiwa mali zao na mashuhuda waliomuona jamaa huyo akiiba na kueleza mchezo mzima ulivyokuwa.“Nilikuja hapa chuoni saa tisa (alasiri) nikaelekea mapokezi na baadaye darasani.
Nilipofika hapo, nikamuona mtu akisimama  ghafla, nikashtuka lakini sikutaka kuwa na wasiwasi sana, nilidhani ni mwanachuo wa hapa,” alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Adolphina na kuendelea:
“Nikaondoka hapo na kupanda juu (ghorofani). Moyo wangu ukawa mzito, ghafla nikajikuta nikishuka ngazi na kurudi kule mapokezi. Nilipofika mapokezi, yule mtu niliyemuona pale hakuwepo, nilipoanza kumtafuta, nikaona akielekea getini kwa mwendo wa harakaharaka, hapo ndipo nilipoanza kupiga kelele za mwizi, naye akaanza kukimbia mpaka alipokamatwa,” alisema Adolphina.
Jamaa huyo alipopekuliwa begi alilokuwa nalo alikutwa na vyeti mbalimbali vya shule ya sekondari ya mkoani Mbeya, cheti cha kuzaliwa, cheti cha TRA na vyeti vingine vingi, vyote vikiwa si vyake.Mbali na vyeti hivyo, pia alikuwa na kadi za mashine za ATM zikiwepo za CRDB, NMB na NBC, hali iliyoonesha kwamba huwa anazitumia kwa ajili ya kuchukulia ‘mkwanja’ kutoka katika akaunti za watu.
Alipopekuliwa zaidi mifukoni mwake alikutwa na simu aina ya Huawei yenye thamani ya shilingi 360,000 na Nokia Asha yenye thamani ya shilingi 150,000, ambazo zote ziliibwa ndani ya chuo hicho siku chache zilizopita.
Askari wa Kituo cha Polisi Kijitonyama – Mabatini ndiyo walimuokoa jamaa huyo mikononi mwa wanachuo hao ambapo walifika eneo la tukio baada ya kujulishwa na mmoja wa watu walioshuhudia jamaa huyo akisulubiwa kwa hasira
 NA GPL

LIVEE!!SIMANZI WAKATI MWILI WA MKUU WA CHUO CHA DSM ULIPOWASILI JKNA

$
0
0


 Waombolezaji wakisukuma jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), marehemu Balozi Fulgence Kazaura ulipowasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jioni hii , kutoka India. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick akiwafariji ndugu wa marehemu
 Ndugu jamaa na wafanyakazi na aliye kushoto ni Dereva wa gari la kubeba mwili huo  wakifunua jeneza kwa utambuzi  wa  mwili wa marehemu Kazaura mara ulipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jioni hii , kutoka India.
Wakiutoa nje tayari kwa kuondoka uwanjani hapo kupelekwa kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Kairuki, Mikocheni
 Mwili ukipakiwa kwenye gari tayari kupelekwa kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Kairuki, Mikocheni,kulia ni dereva wa gari litakalo beba mwili

BUNDI AENDELEA KUWAKALI MAN UNITED,MATOKEO HAYA HAPA

BAD NEWZ,UTEKAJI WA WATOTO NA KUUA JIJINI DSM,WAZAZI SOMENI HAPA

$
0
0

UHALIFU WA KUTEKWA WATOTO NA KUUAWA JIJINI DSM, WAZAZI, WALEZI KUWENI MAKINI

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuhusu ujumbe unaozunguka kwenye mitandao pamoja na ile ya kijamii, ikiwa ni pamoja na simu za mikononi kuhusu utekaji watoto jijini Dar es Salaam.












Ujumbe huo unaosomeka hivi

"Jmn kuna mchezo wakuiba watoto wa

shule umeanza, kuanzia majuzi watoto 12 wa boko wameibiwa, juzi yake watoto20 wa ununio na wengine wa idadi isiyo eleweka wa kunduchi wameibiwa na wote wameibiwa mashuleni…..jana wawili wamepatikana wakiwa wamefariki!! Na inasemekana wanapelekwa mabwepande na mbweni kuna mashimo wanagukiwa na kunyonwa damu…..tupendane, mtaarifu na mwezio!!!"


Taarifa hii sio ya kupuuzia, wazazi na walezi mnaombwa sana kuwa waangalifu na watoto wetu kwani hali hiyo inatisha.
Gazeti moja la kila siku nchini liliwahi kuripoti kuhusu watoto wawili waliotoroka katika handaki moja huko maeneo ya Mabwepande na kwamba polisi walifuatilia lakini hawakuliona handaki hilo.

Immamatukio itaitafuta taarifa hiyo ili kuiweka hadharani kwa faida yako msomaji stay tuned.

PICHA YAKWANZA YA SUPER MKAREEZ ROSE NDAUKA AKIWA NA MTOTO WAKE

$
0
0

Msanii maarufu nchini wa filamu, Rose Ndauka akimbusu mtoto wake aliyepewa jina la Naveen alipokuwa na umri wa siku 9 baada ya kuzaliwa. Hivi karibuni Familia ya Malik ambaye ni baba wa Naveen walisherehekea siku ya kumtoa mtoto huyo, ambapo sherehe hizo zilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu.

CHEKI HUYU POLISI MBULURAAAZ ALICHOKIFANYA HUKO MEXICO

$
0
0

POLISI HUYU ALIONEKANA HUKO MEXICO CITY METRO.



HUYU MBULURAAA AAMBULIA KIPIGO BAADA YA KUIBA KANISANI

$
0
0

http://theclicktz.com/
Emmanuel baada ya kupokea kichapo cha nguvu kutoka kwa wanachuo.
Stori: Nyemo Chilongani na Deogratius Mongela
KIOJA! Kijana anayejulikana kwa jina moja la Emmanuel (30), amejikuta akipokea kipigo ‘hevi’ baada ya kukamatwa akiiba katika Chuo cha Theofilo Kisanji ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dar.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kanisani hapo, mchana kweupe ambapo jamaa huyo ambaye amekuwa akifika mahali hapo mara kwa mara, alijikuta arobaini yake ikitimia na hivyo kutiwa mikononi mwa wanachuo ambao kabla ya kuhoji zaidi, walimshushia kipigo cha mbwa mwizi.

http://theclicktz.com/Wanachuo wakikagua baadhi ya vitu alivyokutwa navyo Emmanuel.
“Huyu ndiye huwa anatuibia humu chuoni na kanisani, kila siku watu wanalalamika kuibiwa vitu vyao. Juzi tu, kuna watu waliibiwa simu, wengine fedha lakini hatukujua ni nani aliyekuwa akitufanyia hivyo, sasa huyu tutamkomesha,” alisema dada mmoja huku akiwa na furaha ya kukamatwa kwa jamaa huyo.
http://theclicktz.com/Emmanuel akiwa mikononi mwa wanachuo wenye hasira.
Wanachuo hao, wakionekana kupania kumfundisha adabu na kumwachisha Emmanuel udokozi, walikuwa wakimhoji maswali huku wakimwangushia kipigo mfululizo, hali iliyosababisha mwili kutoka damu nyingi iliyotapaa sakafuni kama buchani.
Kama kawaida, mapaparazi wetu hawakutaka kuishia kuangalia kipigo tu, waliwaita baadhi ya wanachuo walioibiwa mali zao na mashuhuda waliomuona jamaa huyo akiiba na kueleza mchezo mzima ulivyokuwa.
“Nilikuja hapa chuoni saa tisa (alasiri) nikaelekea mapokezi na baadaye darasani.
Nilipofika hapo, nikamuona mtu akisimama  ghafla, nikashtuka lakini sikutaka kuwa na wasiwasi sana, nilidhani ni mwanachuo wa hapa,” alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Adolphina na kuendelea:
“Nikaondoka hapo na kupanda juu (ghorofani). Moyo wangu ukawa mzito, ghafla nikajikuta nikishuka ngazi na kurudi kule mapokezi. Nilipofika mapokezi, yule mtu niliyemuona pale hakuwepo, nilipoanza kumtafuta, nikaona akielekea getini kwa mwendo wa harakaharaka, hapo ndipo nilipoanza kupiga kelele za mwizi, naye akaanza kukimbia mpaka alipokamatwa,” alisema Adolphina.
Jamaa huyo alipopekuliwa begi alilokuwa nalo alikutwa na vyeti mbalimbali vya shule ya sekondari ya mkoani Mbeya, cheti cha kuzaliwa, cheti cha TRA na vyeti vingine vingi, vyote vikiwa si vyake.
Mbali na vyeti hivyo, pia alikuwa na kadi za mashine za ATM zikiwepo za CRDB, NMB na NBC, hali iliyoonesha kwamba huwa anazitumia kwa ajili ya kuchukulia ‘mkwanja’ kutoka katika akaunti za watu.
Alipopekuliwa zaidi mifukoni mwake alikutwa na simu aina ya Huawei yenye thamani ya shilingi 360,000 na Nokia Asha yenye thamani ya shilingi 150,000, ambazo zote ziliibwa ndani ya chuo hicho siku chache zilizopita.
Askari wa Kituo cha Polisi Kijitonyama – Mabatini ndiyo walimuokoa jamaa huyo mikononi mwa wanachuo hao ambapo walifika eneo la tukio baada ya kujulishwa na mmoja wa watu walioshuhudia jamaa huyo akisulubiwa kwa hasira.

KAMA KAWAIDA bONGO MOVIE: Skendo ya Msanii JB kufamaniwa na Mke wa mtu yachukua sura Mpya baada ya mke kugundulika ana Mimba…

$
0
0
LILE sakata la madai kwamba, staa mkubwa wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’ amenaswa akiwa na mke wa mtu mjini Dodoma limeingia katika sura tofauti baada ya habari yenyewe kujaa utata.

Staa mkubwa wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’. 
Habari za awali zilidai kuwa, tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita katika hoteli moja (jina lipo) iliyopo mjini Dodoma ambapo JB alikutwa na mke huyo wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Sarah.

 
Kwa mujibu wa mwanaume aliyedai kuwa ni mume wa Sarah aitwaye Rama (jina moja), alifuatilia nyendo za mkewe huyo kwa saa kumi na mbili siku ya tukio na mawasiliano yake ambapo kwa muda mrefu alikuwa akiwasiliana na JB ambapo walipanga kukutana katika hoteli hiyo usiku.

 
Saa tatu usiku, Rama alifika ndani ya hoteli hiyo na kuingia kwenye chumba alichokuwa amelala JB na mwanamke huyo ambapo aligonga mlango kwa muda mrefu baadaye sana ndipo ukafunguliwa.

 
Baada ya mlango kufunguliwa, kwa mujibu wa mume wa Sarah,  JB alipokea  kipigo cha haja kutoka kwa mwanaume huyo ambapo wahudumu wa hoteli na polisi waliokuwa wanafanya doria katika shoo ya Jahazi iliyokuwa ikiendelea kwenye ukumbi wa hoteli hiyo  waliingilia kati kumuokoa JB na walipelekwa Kituo cha Polisi cha Area D ambapo maelezo yalichukuliwa na kutakiwa warudi kesho yake.

 
Mwanaume huyo alisema kuwa kesho yake waliporudi polisi walimshinikiza akubali yaishe ambapo walilazimishwa kuelewana.

 
Mume huyo akasema hakurudi nyumbani tangu siku hiyo mpaka juzi hata hivyo akasema:
 “Mimi simuhitaji tena japokuwa ana mimba ya miezi minne na sina uhakika kama ni ya kwangu kwani tabia zake sizielewi bora niachane  naye maana tulikuwa wachumba hatujafunga ndoa.”

HUYO ALIKUWA MUME, JB SASA

Mapaparazi wetu walifanikiwa kumuweka mtu kati JB ambapo baada ya kumuuliza kilichotokea, alisema:
“Mimi nifumaniwe! Hivi inawezekana kweli? Mna uthibitisho au ushahidi wowote? Yule msichana alikuwa klabu, akachukua namba yangu. Si yeye tu, mashabiki wengi waliniomba namba siku hiyo.

 
“Ulikuwa usiku akarudi klabu, mimi nilikuwa hotelini, akanipigia na kusema anataka kuniona ana shida ya kisanii.
“Hata alipokuja sikuwa nimefunga mlango, akaingia na bado mlango ulikuwa wazi. Muda mfupi baadaye akaingia huyo bwana akiwa peke yake na kusema amenifumania.

 
“Hivi jamani, kweli unakwenda kumfumania mkeo upo peke yako? Kwanza hatari! Nilipoona anachachamaa kwa madai hayo, nilitoka nje, huyo anayesema mkewe naye akaondoka lakini alikuwa akisema mbele yake kwamba hajaolewa.
“Kule nje niliwaambia wenye hoteli, wakaamua kuita polisi maana alikuja kunifanyia fujo. Sijui nini kiliendelea, lakini ukweli ni kwamba sikufumaniwa.”

 
Sarah alipopatikana hewani juzi  alisema hajafumaniwa na huyo anayedai ni mumewe ni mpenzi wake tu. Alidai kama kufumaniwa angekutwa akiwa hana nguo.

HIVI NDIVYO LULU ANAVYO ENDELEA KUWATESA MAPEDESHEE VICHECHEZI HAPA BONGO....

MUONEKANO MPYA WA SUPER MKALEEZ SINTAH THE UNSTOPABLE

RIHANNA NA DRAKE WAANZA KUJIACHIA LIVE ..

AYA UGANDA WAANZA KUKOSA RAHA SASA: FACEBOOK NA INSTAGRAM YAFUNGIWA BAADA YA MUSEVENI KUSAINI SHERIA MPYA YA KUPINGA USHOGA

$
0
0

Kufuatia Rais wa Uganda kusaini sheria mpya ya kupinga Ushoga na aina zote za namna hiyo, wamiliki wa Facebook, Instagram, na Twitter wamefunga huduma zote katika nchi ya Uganda ikiwa ni ishara ya kuonyesha kutoridhishwa kwao na hatua ya Museven kusaini sheria hiyo. Kwa sasa wananchi wa Uganda hawatapata huduma hizi labda Rais wao aamue vinginevyo katika sheria hiyo. 

LIVE SOME MBULURAAAZ WAANZA KUIBA WATOTO BONGO SOMA HII LIVE JAMANI TAKE CARE

AYA SASA HUKO FACEBOOK SASA KIMENUKA.. KALA JEREMIAH AMSHHUKIA DIAMOND PLATNUMZ KUHUSU ALIKIBA ....

$
0
0
kalaa
Kwa kitu ambacho kinaonekana si 
cha kawaida kwa Kala Jeremiah kuandika status kali ikiwa kama inamchafua Diamond na kumsifia Ally Kiba kwa kile kilichosemekana kuwa Ally Kiba kakopa pesa ili kumalizia ujenzi wa nyumba aliyokuwa anajenga. 

Screenshot_2014-02-26-13-09-30

AYA SASA CHECK THIS OUT YULE MBABEEEZ MKALEEEZ KULE MAMBELEZ MAREKANI NZIMA WA KWETU FASHION NA MUONEKANO WAKE MPYA...YANI DESIGNED NA YEYE MWENYE NOMA SANA


AYA SASA MAJIRANI ZETU KIMENUKA... DR. SLAA ADAI KUWA KIONGOZI ANAYETAKA KUONDOKA CHADEMA MILANGO IKO WAZI .....ASEMA HATA WAKIBAKI WATATU, CHAMA CHAO HAKITAKUFA - See more at: http://onelovetz.blogspot.com/2014/02/dr-slaa-adai-kuwa-kiongozi-anayetaka.html#more

$
0
0


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa mbunge au diwani anayetaka kuondoka CHADEMA milango iko wazi, kwa sababu hawawezi kumvumilia kiongozi msaliti wa chama.

Dk. Slaa alitoa msimamo huo jana wakati akimnadi mgombea ubunge wa CHADEMA jimboni Kalenga, Grace Tendega, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mnadani, Kijiji cha Kidamali, Kata ya Nzihi huku akisisitiza kuwa hata wakibaki watatu tu ndani ya chama, Chadema haitakufa na kwamba wameridhia kujiuzulu kwa madiwani wao wawili mkoani Shinyanga.

Alisema kujiuzulu kwao ni mpango maalumu uliotengenezwa na wapinzani wao kisiasa kwa lengo la kuwadhoofisha na kuwavuruga -

POLISI WAFAFANUA JINSI MILIPUKO MINNE YA MABOMU ILIVYOTEKEA HUKO ZANZIBAR NA KUUA MTU MMOJA -

$
0
0

JESHI la Polisi Zanzibar, jana limetoa ufafanuzi wa matukio ya milipuko iliyotokea katika maeneo manne tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Hamdani Omari Makame, alisema tukio la kwanza lilitokea Februari 23 mwaka huu, saa saba mchana eneo la Pangawe.


Alisema mlipuko huo ulitokea baada ya waumini wa dhehebu la Evengilistic kumaliza ibada na haukuleta madhara yoyote.

Aliongeza kuwa, wakati polisi wakishughulikia tukio hilo, saa 6:36 mchana ikatokea milipuko mingine mitatu katika maeneo mawili tofauti.

"Mlipuko wa kwanza ulitokea eneo la Malindi mjini Zanzibar kwenye Mkahawa wa Mercury unaomilikiwa na Bw. Simai Mohammed Saidi (45) lakini haukuwa na madhara.


"Ilipofika saa 8:35 na 8:40 kwenye mtaro mmoja uliopo karibu na Mkunazini, eneo la Mji Mkongwe, Mjini Zanzibar ilitokea milipuko miwili iliyopishana kwa muda wa dakika chache," alisema.


Alisema milipuko hiyo pia haikuleta madhara kwa binadamu isipokuwa gari moja lenye namba Z.355 ET Harrier mali ya Bw. Mohammed Ibrahim Ali, lililoegeshwa karibu ya mtaro lilipata madhara kidogo kwa kutoboka bati upande wa nyuma kulia.

Kamishna Makame alisema milipuko yote ilitengenezwa kienyeji na Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wamechukua mabaki ya milipuko hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitaalamu.

Aliongeza kuwa, polisi wameimarisha doria katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Zanzibar ili kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei tena na kuweza kuwakamata wahalifu hao.

"Tayari timu ya Makachero wakiwemo Wataalamu wa Uchunguzi wa Kisayansi kutoka Makao Makuu ya Upelelezi, Dar es Salaam, wamewasili mjini Zanzibar kuungana na Makachero wenzao wa Zanzibar kuendelea na uchunguzi huu," alisema.


Alisema katika hali isiyo ya kawaida, Mkoa wa Kusini Unguja, juzi saa nane mchana katika Kijiji cha Unguja Ukuu, eneo la Kae Pwani, kulikuwa na wavuvi wakivua vyuma ili kwenda kutengeneza nanga ya boti lao, lakini wakati wakiendelea na kazi hiyo chuma walichokuwa wakikitengeneza kililipuka na kujeruhi watu wanne.

Waliojeruhiwa na kukimbizwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ni Juma Abdallah Juma (32), Shabani Khamisi Ibarahim (32) Haji Khamisi(35) na Sumai Hussein Hassan (38).


Wakati majeruhi hao wakiendelea na matibabu, majeruhi mmoja Juma Abdallah Juma (32) alifariki dunia saa 11 jioni na mmoja kati yao Sumai Hussein Hassani (38) alitibiwa na kuruhusiwa ambapo wengine wawili wanaendelea na matibabu.

HAYA SASA MKALEEEZ MTANGAZAJI DIDA WA TIMES FM ANUNUA GARI JIPYA ... TAZAMA HAPA

PREVIEW: GALATASARY VS CHELSEA - MOURINHO DHIDI YA VINYAGO ALIVYOVICHONGA MWENYWE

$
0
0

Galatasaray AŞ walifungwa 5-0 wakati Chelsea FC walipokwenda Uturuki kwa mara ya mwisho, ingawa hivi sasa wana mtu anayeijua vizuri Chelsea Didier Drogba, mshindi wa UCL na Chelsea mwaka 2012. Gala chini ya kocha mpya Roberto Mancini watakuwa wakitumaini kulipiza kisasi.


Mechi zilizowakutanisha nyuma. • Tore André Flo aliipa Chelsea uongozi wa mabao mawili katika mchezo wa makundi baina ya timu hizi miaka 15 iliyopita akifunga kwenye kila lango ndani ya vipindi viwili. Mabao mengine kipindi cha pili yalifungwa na Gianfranco Zola na Dennis Wise pam naoja Gabriele Ambrosetti.
• Vikosi vilivyocheza kwenye mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Ali Sami Yen Spor Kompleksi mnamo 20 October 1999 vilikuwa:
Galatasaray: Mehmet Bölükbasi, Popescu, Emre Belözoğlu, Arif Erdem, Okan Buruk, Fatih Akyel (Ümit Davala 46), Hagi (Hasan Şaş 46), Tugay Kerimoğlu, Hakan Ünsal, Hakan Şükür (Saffet Akyüz 65), Capone.
Chelsea: De Goey, Ferrer, Leboeuf, Desailly, Le Saux, Deschamps (Wise 66), Morris, Poyet (Petrescu 66), Babayaro, Flo, Zola (Ambrosetti 75).
• Mchezo uliochezwa London mnamo 28 September 1999 uliisha kwa ushindi wa 1-0 kwa Chelsea bao la Dan Petrescu dakika 52. 
• Kipigo cha mabao 5-0 cha nyumbani kwa Galatasary kilikuwa cha pili katika michezo nane dhidi ya timu za EPL. Wakiwa wameshinda dhidi ya Liverpool katika michezo miwili katika hatua ya makundi msimu wa 2006/07 (3-2) na Manchester United FC (1-0) msimu uliopita - rekodi yao ya nyumbani W3 D3 L2. Yote dhidi ya timu za EPL W3 D7 L7. 
• Mnamo msimu wa 1999/2000 Galatasaray iliifunga Arsenal FC 4-1 kwenye hatua ya penati kwenye fainali ya UEFA Cup jijini Copenhagen ambayo iliisha bila kufungana kwenye muda zaida, ikiwa timu ya kwanza ya Uturuki kushinda mashindano hayo ya UEFA.
• Katika mchezo wao wa mwisho na klabu ya kutoka Uturuki, Chelsea walifungwa 2-1 na Fenerbahçe SK msimu wa katika robo fainali, lakini wakashinda 2-0 nyumbani na kusonga mbele. Pia walikutana na Beşiktaş JK katika hatua ya makundi msimu wa 2003/04, walifungwa 2-0 Stamford Bridge lakini wakashinda 2-0 ugenini.


Habari za timu
David Luiz ana majeruhi ya paja na John Obi Mikel ana majeruhi lakini hajulikani na alikosa mchezo wa wikiendi iliyopita, Oscar ana tatizo la enka.


Aydın Yılmaz ana tatizo la enka na Gökhan Zan ana majeruhi ya misuli wote wamepona na watacheza leo. - See more at: 

HUKO INSTAGRAM KIMENUKA ..DIAMOND AWASHUKIA WASANII WOTE MBULURAAZ WABONGO WANAOMSEMA....NI BAADA YA KALA JEREMIAH KUMPONDA DIAMOND KUHUSU ALIKIBA

$
0
0


Hivi ndivyo alivyopost kwenye page yake jioni ya leo, "kiukweli, nasikitishwa sana jins baadhi ya wasanii kutwa wanavyolazimisha kunitengenezea ugomvi wa kilazima pasipo kuwa na sababu, mara wengine wakizusha eti Nimewatusi kwenye Media,
Mara sjui Nimepost kuwakashif, yaani ilimradi tu....kwanini Wanamuziki wa Tanzania Tunashindwa kubadilika... mbona mi nahangaika na muziki wangu kimpango wangu... Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba mie sijui "sinatatizo"... Mnasema nyie ndio wenye sauti nzuri yangu mbaya "Sina tatizo"... sasa mbona tena bado mnanifatilia na kutokujua kwangu... Nafkiri ni vyema mkaanza kutumia ujuzi wenu kukuza sanaa ya nchi yetu na kuleta heshima na maendeleo nchini, kuliko kupika majungu..... Watu wanataka kazi" 


SOMA HAPO ALICHOKUA AMEANDIKA KALA JEREMIAH KUHUSU DIAMOND PLATNUMZ

http://williammalecela.blogspot.com/2014/02/aya-sasa-huko-facebook-sasa-kimenuka.html
Viewing all 32622 articles
Browse latest View live