Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

THE BONGO & MAJANGAZ:- HUYU ANATUHUMIWA KUUA BOSS WAKE BAADA YA KUMUUULIZA KWA NINI AMECHELEWA KAZINI!!

$
0
0

Kijana Daniel Kossam (21) anatuhumiwa wa  kumuua bosi wake Bi,Pelesi Chaula (32)ambaye alikuwa akiishinaye nyumba moja huko mtaa wa Ilembo kata ya Iyela mkoani mbeya akiwa chini ya polizi kwenda kuonyesha pesa na simu alivyotumbukiza chooni
Marehemu Bi,Pelesi Chaula (32) enzi za uhai wake
Harakati za kutafuata fedha na simu tatu zilizotupwa chooni na anaetuhumiwa kwa mauaji
Afisa upelelezi wa wilaya Mbeya mtatiro akishukuru wakazi wa mtaa wa iyela kwa ushirikiano utulivu waliouonyesha wakati wa zoezi la kutafuta vidhibiti.



Kijana Daniel Kossam (21) anatuhumiwa wa  kumuua bosi wake Bi,Pelesi Chaula (32)ambaye alikuwa akiishinaye nyumba moja huko mtaa wa Ilembo kata ya Iyela mkoani mbeya
Daniel alikuwa akiuza duka la vifaa vya pikipiki la bi, Pelesi  lijulikanalo kwa jina la 'Twiyanze' lililopo kijiji cha Mbalizi nje kidogo ya jiji la Mbeya.
Chanzo cha ugonvi inadaiwa kuwa ni kuchelewa kurudi nyumbani kijana huyo ndipo Pelesi alipochukua jukumu la kumuuliza jambo lililozua ugonvi katiyao na kusababisha kifo cha bi.Pelesi Chaula.
 Kifo cha marehemu Pelesi kimetokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali mwilini mwake.
Wakati mauaji hayo yanafanyika mume wa bi Pelesi Chaula alikuwa safarini wilayani Makete mkoani Iringa.
Baada ya mauaji hayo Kijana Daniel alichukua simu mbili za marehemu na simu yake pamoja na fedha kiasi cha 114000/= na kuzitumbukiza chooni  kisha alienda kwa jirani kuwajulisha kuwa walikuwa wamevamiwa na majambazi na kwamba wamemuua bosi wake huyo.
 Majirani walipofika eneo la tukio walishangaa kuona kuwa hakuana sehemu ya nyumba iliyokuwa imevunjwa, walipo muuliza Daniel alijibu kuwa alisahau kufunga milango, baaada ya majibu hayo waliingiwa na mashaka na kuamua kutoa taarifa polisi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mjumbe wa serikali ya mtaa Bi,Neema Mwasampeta alisema,'  Dan alichelewa kurudi na alifokewa sana,nadhani hicho ndiyo chanzo cha ugonvi wao'. aliongeza kuwa alimjua kijana huyo kwa muda wa mwaka mmoja.

Na Uswege Luhanga
Mbeya yetu

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>