CCM kidedea jimbo la Kiembe samaki, yashinda kwa 78%
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Zanzibar ambapo alitangaza uteuzi wa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Ndugu Mahmoud Thabiti Kombo. Ndugu Mahmoud Thabiti Kombo
Katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi katika jimbo la kiembe samaki lililopo Mkoa wa Mjini Zanzibar, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Chama Dume, Chama chenye viongozi wanaotumia vichwa kufikiri na kufanya maamuzi kimeibuka mshindi wa jimbo hilo ambapo mgombea wake Ndugu Mahmoud Thabit Kombo ameibuka mshindi kwa kushinda kwa zaidi ya asilimia 78 ya kura zote.
ushindi huo ni salamu kwa chaguzi zingine zinazoendelea kote nchini kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiko imara na tuko seriuos on this business. Hakuna majungu, hakuna u-mungu mtu, huku kazi tu maneno huko huko kwenu.
Wananchi Jimbo la Kiembesamaki, Zanzibar wakiangalia majina yao kujua vituo vyao walivyopangiwa kupiga kura leo asubuhi.