Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MTANGAZAJI M,AARUFU DUNIANI MUAFRIKA ALIYEFARIKI AKIWA USINGIZINI!!

$
0
0


  • Kwa asilimia kubwa alisaidia sana kulitangaza Bara la Afrika hasa alipobuni kipindi maalumu cha kutangaza habari za Afrika pekee.Wengi wa viongozi wa Afrika wamekuwa wakimuona kama ni mwandishi ambaye anafaa kuigwa kwa namna ambavyo alikuwa akifanya kazi zake vizuri.

Wengi wanapendwa na namna alivyokuwa akitangaza, kwani alionekana kuiletea sifa Afrika.
Afrika inasikitika kwa kifo cha Komla Dumor. Rais wa Ghana John Dramani Mahama amemtaja marehemu mtu huyu kama zawadi ya Ghana iliyoletwa kwenye ulimwenguni na kukaa kwa muda mfupi.
Komla Dumor ndiye aliyepamba na kuyatikisa mawimbi ya Shirika la Utangazaji BBC kupitia kipindi chake kipya kilicholenga kuangazia masuala ya Afrika.
Wakati alipojiunga kwa mara ya kwanza na shirika hilo mwaka 2006, Komla alipewa jukumu la kuendesha vipindi vya redio kabla ya kuingia kwenye luninga. Ndiye aliyeasisi kipindi cha luninga cha Sura ya Afrika “Focus on Africa” ambacho kinatoa nafasi kwa mambo yanayojiri barani Afrika kujulikana ulimwenguni kote.
Alikuwa mwandishi aliyebuni mfumo wa aina yake. Kuna wakati alitajwa na jarida moja la kimataifa kuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri barani Afrika. Katika toleo lake la mwezi Novemba mwaka jana Jarida la New African lilimtaja Komla kuwa miongoni mwa watu 100 Afrika kuwa na mvuto mkubwa.
Jarida hilo lilisema lilifikia hatua ya kumweka kwenye orodha ya watu mashuhuri barani Afrika kutokana na mfumo wake wa uendeshaji wa vipindi vya luninga na namna alivyoweza kukabiliana na wanasiasa waliojitokeza kwenye vipindi vyake.
“Komla amefanikiwa kujitambulisha kwa sura ya pekee barani Afrika. Amekuwa  tokezo jipya la utangazaji katika ulimwengu wa watangazaji barani Afrika. Hakika amefaulu kuonyesha namna bara la Afrika linavyopaswa kuripotiwa,” ilisema sehemu ya Jarida la New African likifafanua kwa nini liliamua kumweka katika orodha ya watu mashuhuri na makini barani Afrika.
Komla Dumor alifariki akiwa usingizini Januari 10, 2014 kutokana na tatizo la mshtuko wa moyo nyumbani kwake London akiwa na umri wa miaka 41. Alihitimu shahada yake ya kwanza ya Sosholojia na Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Ghana na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Harvard ambako alitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Utawala.
Dumor ameelezewa kuwa miongoni mwa waandishi shupavu barani Afrika. Rais wa Ghana John Dramani Mahama anasema Ghana imempoteza mmoja wa wajumbe wake.
Mhariri wa habari za ulimwengu katika Shirika la BBC, Andrew Whitehead amemtaja kuwa mwadishi shupavu aliyekuwa na uhusiano mzuri na wasikilizaji.
Tangu kutokea kwa kifo chake, salamu mbalimbali zimeendelea kumiminika ikiwemo kutoka kwa wanasiasa, viongozi waandamizi na wakuu wa taasisi za kimataifa wakielezea namna walivyoshtushwa na taarifa za kifo hicho.
Katibu Mkuu Kiongozi katika Serikali ya Tanzania, Balozi Ombeni Sefue, ambaye kabla ya kutangaza baraza la mawaziri hivi karibuni, alituma salaam za pole kwa Shirika la Utangazaji la BBC kutokana na kifo cha ghafla cha mtangazaji huyo (Komla Dumor).
Balozi Sefue  alimwelezea Komla kuwa ni mtangazaji ambaye alifanya kazi yake kwa weredi mkubwa na hivyo kulijengea heshima bara la Afrika.
“Nianze kutoa pole kwenu na kwa taaluma yenu kwa msiba wa Komla Dumor. Kama mnavyomfahamu alikuwa mtangazaji maarufu wa BBC na kwetu sisi Waafrika ni jambo la faraja inapokuwa kwamba habari za Afrika zinatangazwa na Mwafrika.
“Komla Dumor amefanya kazi nzuri sana, ni wazi kabisa hakupewa nafasi ile kwa sababu tu ni Mwafrika lakini na uwezo wake ulikuwa mkubwa sana, kwa hiyo aliipa Afrika heshima kubwa sana.
 “Na katika kipindi hiki cha majonzi kwa kweli naungana nanyi katika kupeleka salamu zetu za rambirambi kwa familia yake, kwa BBC na kwa Waafrika wote na Ghana kule alikotoka, kwamba msiba huu ni wetu sote Afrika.” anasema Balozi Sefue.
Komla mara ya mwisho alikuwa nchini mwaka jana wakati wa ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama ambako anatajwa kuwa alifanikisha kuandaa matangazo yaliyoangazia ziara hiyo kwa kiwango cha juu.
Pia katika kipindi hicho cha mwaka jana alikwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya mahojiano maalumu na Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton aliyekuwa nchini kuangalia utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na wakfu wake.
Watu wengi wakiwemo waandishi wa habari wanamwangalia mtangazaji huyo kama mtu ambaye kwa kiasi kikubwa aliifanya kazi yake vizuri kiasi cha kuiletea sifa kubwa siyo tu Ghana bali Afrika kwa ujumla

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>