Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

THE MAJANGAZ & BONGO:- SUPER STAR WEMA SEPETU AMCHANA LIVE FUNDI WAKE!!

$
0
0
BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu ametengeneza habari mpya kama kawaida yake. Safari hii amemuanzishia timbwili zito fundi wake aliyefahamika kwa jina moja la James.

Wema Isaac Sepetu.
Akizungumza kupitia kipindi chake cha In My Shoes mapema wiki hii, Wema ambaye hachukii ukimuita Madam,
aliweka bayana kuwa tukio hilo ambalo lilitokea siku za nyuma lilimkera kwa sababu fundi huyo alimuamini kuwa atamfanyia ukarabati mzuri wa nyumba yake, badala yake akamharibia.
 

Siku ya tukio, Wema aliyekuwa amehama kwa muda kupisha ukarabati wa nyumba hiyo, baada ya fundi kujiridhisha kuwa amekamilisha ujenzi, alimuita Wema akakague ndipo mtiti ulipoanza. Alimtukana fundi huyo, akamfokea vya kutosha akidai hajaridhishwa na ukarabati alioufanya.
 

“This is my house, kwa nini umefanya vibaya? Sijapenda, sasa hivi ndiyo nini? Rangi gani hii umepaka? Yaani umeniharibia kila kitu, sipendi kuharibiwa kabisa nyumba yangu…” alifoka Wema.
Licha ya Meneja wa Wema, Martin Kadinda kuwepo nyumbani hapo na kumsihi wampe siku mbili fundi huyo ili arudie ukarabati, Madam aliendelea kuvurumisha ‘mitusi’ kama aliyechanganyikiwa.
Sini hiyo ya varangati ilioneshwa ‘live’ kupitia kipindi chake hicho kinachorushwa na Runinga ya East Africa ambapo fundi huyo alionekana akimwaga machozi kisha kuondoka nyumbani hapo kwa unyonge baada ya kukosa muafaka.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>