Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

THE MAJANGAZ & BONGO:- RED HANDED MWANAUME ANASWA NA MKE WA RAFIKI YAKE GESTI HOUSE LIVE!!

$
0
0

Na Mwandishi WetuMAANDIKO yanasema ‘usitamani mali ya mtu mwigine’! Ni kweli kabisa, onyo hilo lilichukua fursa yake kufuatia njemba mmoja aliyejulikana kwa jina la Anton John Mwaweje kunaswa laivu gesti na mke wa rafiki yake aliyefahamika kwa jina moja la Chalz.
ANGALIA KAMANDA WA OFM AKIELEZA ALIVYOMNASA NJEMBA AKIWA NA MKE WA RAFIKI YAKE GESTI!
Mke wa mtu sumu: Anton John Mwaweje baada ya kunaswa akiwa na mke wa rafiki yake gesti.
Tukio hilo lilijiri mwanzoni mwa wiki hii kwenye gesti moja maarufu (jina tunalo) iliyopo Buguruni- Malapa jijini Dar es Salaam.
Katika sakata hilo ilidaiwa kuwa, Mwaweje alikuwa akiifahamu vyema familia ya Chalz sambamba na mke wake (jina lipo) lakini hilo hakulijali na kumtokia mke wa Chalz ambaye kwa utamaduni wa Kiafrika ni shemejiye.
Mshangao: Anton John akishangaa baada ya kuba
Habari zikazidi kudai kwamba, ilifika mahali katika kumtaka shemejiye huyo ambaye alikuwa akimkatalia katakata, Mwaweje alitumia gia nyingine ikiwemo ya kumuahidi mambo manono kama angekubali kuivunja amri ya 6 ya Muumba na yeye.
Chanzo cha habari kiliendelea kudai kuwa,  ‘Mungu si Athuman wa Lucas’ siku isiyo na jina jamaa alimtumia ujumbe (SMS) mke wa mwenzake kwa kutumia maneno ya kumtoa nyoka pangoni kumbe muda huo bwana simu alikuwa nayo mwenye mke.
Misosi na mitungi: Baadhi ya misosi na vinywaji vilivyokutwa chumbani humo.
Chalz alimwita mkewe na kumuuliza ni nani aliyemtumia ujumbe huo? Ndipo mke akaanika ukweli akisema:
“Mume wangu, wala usikonde. Aliyetuma ujumbe huo si mwingine, ni Anton…”
Mume:  “(akihamaki) Anton huyuhuyu?”
Mke: “Huyuhuyu mume wangu. Amekuwa akinitaka kimapenzi kwa muda mrefu sana, namkatalia lakini hasikii.”

 
Za mwizi 40: Bwana Anton John akiwa na pingu mkononi baada ya kunaswa na kamanda wa OFM pamoja na wanausalama.
Pia, mwanamke huyo alimwonesha mumewe meseji kibao ambazo jamaa huyo amekuwa akimtumia na zile ambazo yeye amekuwa akimkatalia.
“Sasa sikia, mkubalie,” mwanaume huyo alimwambia mke wake huku midomo ikimcheza kwa hasira.
Chini ya usimamizi wa mumewe, mwanamke huyo aliwasiliana na Anton na kumwambia alikuwa na nafasi wanaweza kukutana kwa ajili ya kumsaliti Chalz.

Baada ya kupanga mipango ya kukutana, mume huyo alipiga simu Global Publishers kwenye kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kuomba msaada wa fumanizi ambapo alibahatika kukuta kuna kamera mpya zimewasi tayari kwa kazi kama hizo.
Baada ya kupata maelezo ya Chalz, OFM ilishirikiana na Jeshi la Polisi Buguruni –Kwamnyamani jijini Dar na kuandaa mtego ambapo Jumatatu iliyopita, saa nane na ushee mchana, Anton ambaye naye inasemekana ana mke aliuingia mtego na kunasa kwenye chumba namba 5 akiwa na mke mwema huyo.
Ndani ya chumba hicho, Anton alikutwa na boksa  tayari kwa mlo wa wizi ambao alibakia kuendelea kusikia njaa. Mezani, kulikuwa na chipsi kuku na pombe ambazo zingewapa stimu kabla ya mchezo.
Kitendo cha Chalz kumnasa jamaa huyo na mkewe kitandani kilimpandisha munkari ambapo nusura afanye ndivyo sivyo lakini alitulizwa na polisi waliokuwa eneo hilo kwa ajili kulinda usalama.
Kilichofuata baada ya hapo, mgoni huyo akiwa na pingu mkononi alipelekwa kwenye kituo hicho cha polisi ambapo awali, Chalz alitoa ripoti ya malalamiko baada ya kugundua  jamaa huyo anataka kumtumbukiza mkewe kwenye mstari wa usaliti.
Mpaka OFM wanaondoka kituoni hapo, taratibu za kisheria kuhusiana na kesi hiyo zilikuwa zikiendelea huku mgoni huyo akiwa chini ya ulinzi mkali.
Kujua jinsi jamaa huyo alivyonaswa, tembelea Global TV Online kupitia: www.globalpublishers.info

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>