Bw.Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng. George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi (kulia) wakisaini MOU.
Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
KAMPUNI tanzu ya Tume ya sayansi na teknolojia ya DTBi-COSTECH na Silicon Valley Black Chamber of Commerce’s Center for Entrepreneurial Development (SVCED) wametiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano (MoU) ambapo pande zote mbili zitashirikiana kwa njia mbalimbali kwa ajili ya ukuaji wa wajasiriamali.
Mkataba huo, kati ya DTBi na SVCED utawezesha pande hizo mbili kukuza ujasiriamali na kujenga uwezo katika Habari, Teknolojia na Mawasiliano kwenye sekta zote za kiuchumi.
Mkataba huo wa MoU utawafanya wadau kufanya shughuli za biashara kwa kuanza na mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano kwa kupitia njia ya mtandao na kusaidia wale walio na ubunifu katika nyanja mbalimbali za biashara.
Bw. Carl Davis Jr, Rais wa Silicon Valley Black Chamber of Commerce na Eng. George Mulamula, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi kupeana mikono baada ya kusaini MOU.
Mkataba huo pia utasaidia wajasiriamali kuweza kukua na kufanya biashara kwa kutumia mifumo habari, teknolojia na mawasiliano katika kukuza ujasiriamali na kuanzisha mfumo wa kubadilishana uzoefu katika kuendeleza biashara na ukuaji wa ujasiriamali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi, Injinia. George Mulamula amesema mkataba MOU utatoa ushirikishiano ambao utaruhusu wajasiriamali wa Tanzania kufaidika na ujuzi, maarifa ya Silicon Valley ya ujasiriamali.
Amesema hii itasaidia nchi ya Tanzania kuruhusu uanzishwaji wa biashara kupitia njia ya mtandao na mifumo ya Habari, teknolojia na mawasiliano katika kukuza ajira na kuchangia pato la taifa.
Eng.George Mulamula akielezea ushirikiano kwa vyombo vya habari.
Baada ya kutiliana saini ya MOU, Bw Carl Davis Jr, alikuwa na semina kwa wajasiriamali yenye jina la “The Mindset of the Silicon Valley Entrepreneur: Lessons for the Tanzania Entrepreneur/Innovator”.
Mr Davis Jr amesema anaweza kuwasaidia “wajasiriamali kuelewa jukumu la uzinduzi na ujasiriamali na jinsi Wajasiriamali hapa nchini jinsi wanavyoweza kujiinua katika kufikiri chanya kwenye maeneo ya biashara.
Bw. Carl Davis Jr, akitoa majadiliano DTBi kwa wajasiriamali wa Tanzania juu ya jinsi ya kuwa mwekezaji mwenye mafanikio.
Mshiriki akichangia mjadala.