Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

DR. KITILA MKUMBO KIONGOZI ALIYEFUKUZWA CHADEMA AFUNGUKIA KATIBA MPYA NA KURA ZA SIRI MSOME HAPA LIVE!!

$
0
0

 
Hili suala la kura ya siri na wazi sio gumu lakini pia sio rahisi sana. Cha kuzingatia ni kwamba wote waliomo katika Bunge la Katiba wanawakilisha kundi fulani. Makundi haya kwa pamoja ndiyo yanaunda hili Bunge na ndio yanayojenga uwakilishi wa wananchi. Ndio kusema wabunge hawa hawapo kivyao. Wanatuwakilishi sisi na kila mbunge katumwa na kundi fulani. Sisi tuliopo katika taasisi za elimu tuna wawakilishi 20. Hapa UDSM tunao watatu. Hivyo hivyo kwa makundi mengine. Ningependa nijue hawa wawakilishi wangu wameunga mkono kitu gani na kitu gani wamepinga, hasa katika mambo magumu katika Katiba kama vile adhabu ya kifo, uraia pacha, ushoga na muundo wa muungano. Sasa wakipiga kura ya siri mimi nitajuaje? Na atakuwa anamwakilisha nani kwa kura hiyo ya siri?

Dhana ya kura ya siri inafanya kazi sana katika uchaguzi kwa sababu kwa kiasi kikubwa kuchagua mgombea ni jambo la utashi binafsi. Kwenye katiba hii hakuna utashi binafsi. Unawakilishi kundi fulani na makundi yaliyokutuma yana haki ya kujua umeunga mkono nini na umepinga nini.

Kama wewe ni mwakilishi wa chama kwa kiasi fulani una wajibika kufuata msimamo wa chama chako. Kama wewe umetumwa na wafugaji una wajibu wa kufuata msimamo wa wafugaji. Kama wewe unawakilisha NGO unawajibika kubeba msimamo wa NGO yako. Vivyo hivyo kwa wakulima, n.k.

Wabunge wa JMT na wawakilishi wa Baraza la wawakilishi wanawajbika kuzingatia maoni ya wapiga kura wao, vyama vyao na nafsi zao. Ni wajibu wao kutii maoni ya wapiga kura wao, vyama vyao au nafsi zao au vyote kwa pamoja. Wananchi wangependa kujua wabunge hawa wameunga mkono nini na wamepinga kitu gani kama ilivyo katika mijadala mingine ya kibunge.

Makundi haya kwa pamoja ndio yanaunda nchi na kwa pamoja tunawapata wananchi. Sasa hii dhana kwamba hatupo hapa kuwakilisha makundi yetu sijui inatoka wapi wakati mnajua kabisa mmetumwa huko mlipo na makundi yenu! Bila makundi dhana nzima ya nchi na wananchi ni nadharia kabisa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>