Ikiwa yamebaki masaa machache kuelekea mechi ya marudiano kati ya klabu ya Chelsea na Galatasaray,kocha mwenye mbwembwe na
maneno mengi Jose Mourinho amesema anaamini mchezaji wake wa zamani katika klabu hiyo ya London Didier Drogba atarejea katika klabu hiyo kwa siku za usoni.Mourinho alisema kuwa japo Drogba bado ni mchezaji halali wa klabu hiyo ya Galatasaray lakini anafahamu mkataba wa mshambuliaji huyo toka Ivory Coast utafika kikomo mwishoni mwa msimu huu,huku akisisitiza kuwa si wakati sahihi kuzungumza juu ya hilo.
“Nafikiri ipo siku hiki ninachokiamini kitatokea,na ukiniuliza ni lini kwa kweli sitakuwa na jibu,lakini naamini atarudi katika klabu hii ama kama mchezaji,kocha au pengine balozi wa klabu,naamini atarudi ndio nab ado nasisitiza sijui ni kama mwakani au hata baada ya miaka mine au kumi.”
Mreno huyo alimalizia kwa kusema Drogba ni mmoja kati ya wachezaji bora wa kihistoria kwenye klabu hiyo inayotumia uwanja wa starmford bridge.