Familia ya afisa mmoja wa Elimu nchini Kenya imepigwa na butwaa baada ya kupata jeneza dogo likiwa limewekwa kwenye mlango wao mjini Kisumu Magharibi mwa Kenya. Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Taifa Leo, familia ya Afisa huyo Elias Oganda, mwenye umri wa miaka 56, ilipata jeneza hilo dogo likiwa na mzoga wa Paka nje ya mlango wao na sasa anaishi kwa hofu kubwa. Afisa huyo anayefanya kazi katika wizara ya elimu, alisema kuwa hii ni mara ya nne katika miezi sita kupata jeneza kama hilo nyumbani kwake. Polisi walifungua jeneza hilo na kupata mzoga wa Paka ndani yake. Walishuku kuwa Paka huyo alinyongwa na kuwekwa ndani ya jeneza hilo kwani hapakuwa na dalili yoyote ya damu. .
↧