Kila kukicha msanii Christopher Mourice a.k.a Chris Brown amezidi kukumbwa na mikiki ya hapa na pale baada ya kukaa sana rehab.Tangu ijumaa ya wiki iliyopita alitimuliwa na sasa mahakama imeamua Chris aende jela mwezi mmoja kuanzia sasa hadi mwezi April 23, kutokana na kukiuka masharti aliyopewa na mahakama.
Sababu moja wapo iliyompelekea Chris kutimuliwa rehab ni kukataa kipima kipimo kinachoonesha kama anatumia dawa za kulevya, pia sharti lingine ambalo amelikiuka alionekana akimshika mwanamke wa rehab hiyo sehemu ya mkono.
Katika rehab iyo inayoitwa Malibu, sharti moja wapo ni kukaa mbali na mwanamke yeyote zaidi ya umbali wa hatua mbili, lakini Chris alionekana kukiuka hivyo ikampasa atimuliwe