Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtwisha ndoo ya maji Bi. Amina Rajab, mkazi wa Wilayani Mpwapwa, baada ya kuzindua rasmi Kisima cha Bomba la maji, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi Kisima cha Bomba la maji sikiliza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014. Kushoto kwa Makamu ni Waziri wa Maji , Profesa Jumanne Maghembe,(kushoto) ni Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa Maji wa Wilaya ya Mpwapwa, Shadrack Matemba (wa pili kulia) wakati alipotembelea moja ya chanzo cha maji wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014. Kulia kwa Makamu ni Mama Asha Bilal na Waziri wa Maji , Profesa Jumanne Maghembe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wagogo wakati alipokuwa akiwasili katika sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014.
Baadhi ya wananchi wa Wilayani Mpwapwa wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akiwahutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014.Picha na OMR