Sumaye:Rushwa nchini tatizo linaloathiri maisha ya wengi
Rushwa ni tatizo linaloongezeka kwa kasi na kuumiza uchumi, wananchi na linavunja heshima na hadhi ya taifa letu kwa jumla
Mauaji ya kutisha yanayotokea kila mara kama vile watu kujitoa mhanga na kuua watu wengi wasio na hatia, ni miongoni mwa vielelezo vya ukosefu wa maadili mema.
Hili ni tatizo katika jamii, taifa na katika ulimwengu mzima, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kukemea, kuelimisha na kuzungumzia ubaya wa mmomonyoko wa maadili. Viongozi wa kisiasa na wale wa madhehebu mbalimbali ya dini, wamekuwa wakijitokea kila mara kukemea matukio haya na kutoa angalizo kwa jamii hususan, vijana kugeuka na kuwa waadilifu ili taifa liwe na amani.
Wiki iliyopita, Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye alialikwa na taasisi ya vijana wa Vyuo Vikuu wa Kipentecoste (UPSF), mkoani Morogoro katika uzinduzi wa albamu yao ambapo alipata fursa ya kuzungumzia ubaya wa mmomonyoko wa maadili.
Sumaye anasema ukosefu wa maadili husababisha matatizo mengi yakiwemo ya rushwa, ufisadi, ujambazi, biashara na matumizi ya madawa ya kulevya na mengine mengi yanayoisibu jamii yetu.
Anasema kwa tathmini yake rushwa ndiyo tatizo kubwa linaloumiza Watanzania wengi kuliko matatizo mengine na kwamba Watanzania wengi wanashindwa kupata haki zao mpaka watoe chochote.
“Rushwa ni tatizo linaloongoza Tanzania katika kuathiri maisha ya watu wengi...madereva barabarani hupata shida kupita bila kutoa kitu kidogo kwa baadhi ya askari wa barabarani na kadhalika.
Anaongeza kuwa, rushwa ni tatizo linaloongezeka kwa kasi na kuumiza uchumi, wananchi na linavunja heshima na hadhi ya nchi yetu na taifa letu kwa jumla. “Leo kuna watu wanataka kuhalalisha ulaji wao wa rushwa kwa kusingizia neno kama takrima kuweko katika sheria ya uchaguzi...hivi ni kweli neno takrima ndiyo inayohalalisha wewe kujengewa nyumba, kununuliwa gari au kupewa mamilioni ya fedha kwenda kuwanunua wapigakura” anahoji.
Wito kwa vijana
Sumaye akatoa aliouita ushauri wa bure kwa vijana akisema kutokana na nguvu na wingi walionao, wana uwezo wa kutengeneza Tanzania ya kesho ambayo wangependa kuishi.
Anaongeza kuwa takwimu za sensa ya 2012, zinaonyesha kuwa idadi ya vijana inakaribia asilimia 60. “kwa wingi na kwa nguvu mlizo nazo, mna uwezo pia wa kuiharibu au kutengeneza Tanzania iliyo mbovu.” Akaendelea, “Lakini kwa vile kila mmoja wenu anataka kuishi katika nchi yenye neema, basi wote lengo letu ni kuwa na nchi nzuri yenye amani, neema, upendo, mshikamano, yenye maendeleo na yenye kuheshimika” anasema. Anaongeza kuwa kihalisia wazee wanapenda siku zao chache zilizobakia waishi kwa raha, lakini vijana wana masilahi zaidi ya kutazama miaka 50 ijayo ifananaje.
“Ukishaamua unataka miaka 50 ijayo Tanzania yako ifananaje, kazi iliyoko mbele yako ni kuitengeneza hiyo Tanzania. Kwa bahati nzuri pia una uwezo wa ama kuitengeneza hivyo utakavyo au una uwezo wa kuchonga vitendea kazi vya kukutengenezea hiyo Tanzania uitakayo” anasema. Anasema vijana ni tegemeo kubwa la taifa kwa hali zote kwa kuwa ni nguvu kazi ya taifa, ni nguzo ya uchumi, ni wajenzi wa kesho na vilevile ni jeshi la kulinda taifa.
“Unaitwa kijana kwa sababu ya umri wako mdogo kuliko wa mtu mzima au mzee, hakuna kigezo kingine...kama una umri wa miaka 25 leo na Mungu akakujalia kuishi hadi umri wa miaka 75, maana yake una miaka mingine 50 ya kuishi, hivyo kama kijana una sababu na masilahi zaidi ya kutaka miaka 50 ijayo iwe ya neema katika nchi hii kuliko mzee aliyebakiza labda miaka 5 au 10 ya kuishi,” anaongeza. Madhara ya uvivu Sumaye vilevile akazungumzia madhara ya uvivu akieleza kuwa lipo tatizo la Watanzania walio wengi kutowajibika na kusema endapo kila mtu atafanya kazi kwa nguvu zake zote na kwa juhudi na maarifa hali ya nchi yetu itabadilika.
“Viashiria na vigezo vya uchumi mzuri vipo...hivi ni pamoja na amani na utulivu, rasilimali watu, rasilimali za asili na rasilimali ardhi, endapo kila mtu atafanya kazi kwa nguvu zake zote na kwa juhudi na maarifa hali ya nchi yetu itabadilika sana” anasema.
Anasema ipo haja kwa Watanzania kubadilika na kupunguza alichokiita majungu na badala yake wafanye kazi kwa bidii sana.
“Siku hizi utakuta katika kila kijiji kuna sehemu inaitwa kijiweni na hapo hukosi vijana ambao wamejikalia tu iwe asubuhi, mchana au jioni...kama Watanzania wote wakiongozwa na vijana tukiamua kufanya kazi kwa bidii umaskini huu utapungua sana na tatizo la ajira litapungua kwa kiasi kikubwa” anaongeza.
Utawala bora
Sumaye vilevile akazungumzia kuhusu umuhimu kwa kila kiongozi katika eneo lake kuheshimu utawala bora unaofuata misingi ya katiba, sheria, kanuni na taratibu. Anasema kutokuwepo kwa utawala bora kunasababisha matatizo makubwa katika nchi kama uonevu, unyanyasaji, upendeleo, ukabila, uwizi na ujambazi na mengine mabaya zaidi kama rushwa, ufisadi na biashara za dawa za kulevya.
Anasema ni wakati wa kila Mtanzania kwa imani yake kuwa na hofu ya Mungu kwa maelezo kuwa mtu anayemjua Mungu na mwenye hofu ya Mungu hawezi kufanya mambo maovu ambayo yanamchukiza Mungu na yanaichukiza jamii. “Mcha Mungu wa kweli atatenda haki; hawezi kumdhulumu binadamu mwenzake, hawezi kudai rushwa ili atoe huduma kwa mtu, hawezi kuiba fedha za umma wala hatafanya ufedhuli au ufisadi wa aina yoyote au uonevu wa aina yoyote kwa maana anajua hayo yote ni dhambi” anasema . Anaongeza kuwa maneno ya Mungu yanajenga kiimani, kimaadili na kusaidia kuwa na hekima na busara.
Wito kwa wasomi
Sumaye pia akatumia wasaa huo kutoa wito kwa wasomi nchini kwa kuwaeleza kuwa wanayo nafasi kurekebisha mambo yasiyofaa na yanayotendeka nchini. “Wasomi lazima mchukue nafasi yenu katika mambo ya nchi na katika jamii, musiwaachie tu wanasiasa kila kitu na ninyi mkabaki watazamaji na baadaye walalamikaji. Timiza wajibu wako sasa” anasema.
Anaongeza kuwa wanasiasa wana tabia ya kuangalia zaidi kipindi cha uchaguzi ambacho ni kila baada ya miaka mitano lakini akasema wasomi wakiwa kichocheo cha kuelimisha jamii umuhimu wa kuwa na viongozi wanaotimiza wajibu wao watasaidia taifa kupata viongozi walio bora. “Ni kweli sisi wanasiasa huwa hatupendi kupingwa pingwa.. hayo musiyaogope kwa sababu kukwaruzana kwa lengo la kujenga ndiyo afya ya jambo lenyewe...Kunyamaza wakati mnajua tunavyokwenda sivyo ni kutokutenda wajibu na hilo ni dhambi” anasema.
Anaongeza kuwa kwa jinsi wasomi wanavyozidi kuwaachia uwanja wa ukiritimba kwa sababu yoyote iwe ya uwoga au kutokujali hali anayosema itawaweka mbali na masuala yanayohusu taifa na ndivyo umuhimu wa usomi na taaluma utakavyopungua.