Mara baada ya kuchukua na kukabidhiwa fomu ya kugombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa alisema "nipeni urais ning'oe ufisadi".
Katika hafla hiyo iliyojaa shangwe, vigelegele na kelele zilizomtaja Dk Slaa kuwa ni Rais, mgombea huyo ambaye amekuwa mbunge wa Karatu kwa takriban miaka kumi sasa, aliwaambia Wananchi kuwa, “Nilikuwa sina mpango wa kugombea nafasi ya Urais ndiyo maana nikaamua kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge...,” “Sababu ya kutochukua fomu ya kugombea nafasi ya urais ni kwamba najua kuwa Ikulu si sehemu ya kukimbilia....” lakini aliamua kuchukua fomu hiyo kufuatia maombi ya kamati kuu ya CHADEMA ya kumtaka agombee nafasi hiyo. Mara baada ya kusema hayo, aliwaomba wananchi wa Karatu waseme kama wamekubali, ndipo walipomjibu kuwa wamekubali naye akairejesha fomu.
"Nawaomba Watanzania mniunge mkono ili niendeleze vita dhidi ya ufisadi pamoja na kuwatetea masikini hapa nchini," Dk. Slaa.

Naye Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliwaeleza Wananchi sababu za kamati kuu kumuomba Dk. Slaa agombee na aliwaahidi Wananchi kuwa watapambana kwa kila hali ili jimbo la Karatu libaki mikononi mwa CHADEMA, "tutaweka mgombea makini atakaye endeleza yale yote aliyoyafanya Dk. Slaa”.
Baada ya hotuba ya viongozi hao, mamia ya wananchi walipanga foleni na kujaza majina kwa ajili ya kumdhamini Dk. Slaa.
Dk. Slaa aliingia mjini Arusha majira ya saa 7:00 na ndege ya Precision akiwa na baadhi ya wajumbe wa chama hicho. Baada ya kupokelewa ulianza msafara wa mnagari 15 kuelekea Karatu. Msafara huo ulihusisha wabunge Halima Mdee, Grace Kiwelu na Lucy Owenya na wafuasi wa CHADEMA Arusha na Kilimanjaro.
Ratiba ya chama hicho inaonyesha kuwa mara baada ya mkutano huo, itaanza ziara ya kutembelea tarafa zote za Karatu kwa helikopta kukusanya wadhamini na baadaye atakwenda Arusha mjini, Musoma, Mwanza, Singida, Bukoba, Dodoma ikiwa ni safari ya kusaka wadhamini. Ziara hiyo imepangwa kuhitimishwa Agosti 6.
credits: Picha - Yahya Charahani/Mzee Wa Mshitu Habari - Mussa Juma/Mwananchi