Kikosi cha Simba SC kilichoanza mtanange wa leo.
Mshambuliaji wa Simba Sc, Ramadhani Singano 'Messi' akikwaana na beki wa Coastal Union wakati wa mechi ya leo.
Simba SC imeendelea kusuasua katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Coastal Union leo.
Bao la Coastal limewekwa kimiani na Hamad Juma dakika ya 45 kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.Chanzo GPL