Ajali mbaya ya pikipiki ambapo mwendesha Bodaboda amemgonga mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Heri Idd mkazi wa kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora, Idd aligongwa na Bodaboda hiyo wakati akiwa barabarani akiendesha usafiri wake wa baiskeli na mara baada ya kugongwa na kuvunjika mguu,Mwendesha Bodaboda ambaye hakufahamika mara moja aliamua kukimbia na kuicha pikipiki yake imezunguukwa na umati wa watu huku majeruhi akipatiwa msaada wa kupelekwa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya matibabu.
↧