Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

POMBE SI CHAI,ANGALIA JAMAA LAVYOFAKAMIA POMBE

$
0
0
Wakazi wa Dar es Salaam pamoja na wahudumu wa bar ya Bulls park wakimuangalia kijana ambaye jina halikufahamika akiwa amelala chini baada ya kuzidiwa na pombe.Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja alijikuta akianguka na kutokwa na povu mdomoni kwa kile kinachosemekana kwamba alizidiwa na pombe.

Nkurlu Exclusive ilifika mda mchache eneo la tukio na kushuhudia kijana huyo akiwa amelala chini pasipo kujiweza. Wasamaria walionekana kujaribu kumwagia maji ili aweze kurudi katika fahamu zake pasipo mafanikio.

Kama baada ya dakika 10 alitokea kijana mmoja na kukiri kuwa ndiye aliyekuwa akistarehe nae, alieleza hali halisi na kusema kabla ya kuanza kunywa pombe kijana mwenzake alipata mlo wa nguvu tuu kisha ndo wakaanza kushusha mbili tatu. Alisema wakati wakuondoka alimkabidhi kwa dereva bajaji mmoja ila hakufanikiwa kupanda ile Bajaj na kukuta amedondoka.
Kijana huyo pia alisema kuwa kijana mwenzake alikuwa ni mwenyeji wa Mwanza na alikuja Dar es Salaam maalumkwa ajili ya kujirusha na nayeye na ndipo akakutwa na huo mkasa.
 
ANGALIA PICHA ZAIDI

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>