Consolata Edward ni mke wa mtu, mkazi wa Igoma jijini hapa ambaye amebaki na kipisi cha sikio baada ya kunyofolewa kiungo hicho kisa kikidaiwa kuwa ni hawara yake.Tukio hilo lilitokea Desemba 16, mwaka jana ambapo mwanamke huyo alidai kuwa alikuwa akizungumza kwa simu na mfanyakazi mwenzake ambaye anauza naye chakula maeneo ya Mlango Mmoja jijini hapa kabla ya mumewe kumvamia na kumpiga.
Consolata akiwa na mumewe.
Kwa huzuni, Consolatha aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa baada ya mumewe kumpiga yeye aliamua kupigana naye kisha kumchania ‘boksa’ na kusababisha viungo vyake vya uzazi kubaki wazi.
Alisema wakati timbwili likiendelea, ghafla alitokea mama mwenye nyumba akifuatana na mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Hawa na kumg’ata sikio lake hadi akalinyofoa na kulitema.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mume wa Consolathaaliyejitambulisha kwa jina moja la Athuman alidai kuwa siku ya tukio alimuona mkewe akiongea na simu usiku jambo ambalo halikuwa kawaida yake na alipomuuliza alikata simu na kwenda kuongelea nje ya nyumba.SOMA ZAIDI