Imeshawahi kuandikwa baada ya stori kusambaa kwamba mwimbaji mtanzania Diamond Platnumz ana uhusiano wa kimapenzi na mwimbaji Mkenya Victoria Kimani ambae ni dada wa rapper Bamboo, rapper huyu alisema
Diamond hana hadhi ya kutembea na mdogo wake.
Inawezekana hii kauli ya staa huyu wa ‘compe’ labda iliwafanya baadhi ya watu waone kama hampendi Diamond ila kiukweli, staa huyu ambae ni msanii anaependa kujihusisha na muziki unaoinua watu kimaisha pia, amekua mkweli kuhusu jitihada zinazofanywa na Diamond kwenye muziki.
Kwenye Exclusive interview Bamboo amesema ‘kitu kizuri au kikubwa ninachokiona kwenye muziki wa bongofleva sasa hivi ni kile kinachoonekana kwenye Channel O, MTV au East Africa TV na ninachokiona ni kwamba Diamond anang’aa sana sehemu hizo’