Marekani imetangaza kutuma ndege za kijeshi na vikosi maalumu vya kijeshi kumtafuta kiongozi wa uasi wa Uganda, Joseph Kony.
Ndege zipatazo nne aina ya CV-22 Ospreys zenye kusambaza mafuta, pamoja na vikosi 150 vya jeshi la anga vitawasili nchini Uganda wiki hii.
Bwana Kony anahitajika na Mahakama ya Makosa ya Jinai (ICC) kwa makosa ya uhalifu wa kivita.
Mara ya kwanza Marekani ilipeleka vikosi maalum 100 vya kijeshi mwaka 2011 kuzisaidia nchi za Afrika kumkamata.
Kundi lake la waasi wa Lord Resistance Army linasifika kwa vitendo vya kuteka watoto na kuwalazimisha kuwa wanajeshi na kuwafanya mabinti kama watumwa wa ngono.
Watoto wa kiume wanalazimishwa kuua wazazi wao wenyewe, na hivyo kuwafanya washindwe kurejea nyumbani.
Kundi hilo lilianzishwa nchini Uganda miaka ya 1980 ambalo kwa sasa wapiganaji wake huranda randa kati kati ya nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Marekani wametoa ofa ya fedha ya dola milioni 5 kwa yeyote atakayewesha kukamatwa kwake.