Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MENGI YAENDELEA KUIBUKA KESI YA PISTORUS...

$
0
0

Aliyekuwa mpenzi wa Oscar
Pistorus, marehemu Reeva
Steenkamp, alimtumia ujumbe wa
simu kumwambia kuwa wakati
mwingine alikuwa anamuogopa
sana.

Haya yamejitokeza katika kesi
inayoendelea dhidi ya Oscar Pistorius
nchini Afrika Kusini.
Ujumbe huo aliutuma Reeva baada ya
wawili hao kugombana
alipomtuhumu kwa kutongozana na
mwanamume mwingine...wiki chache
kabla ya kumuua.
Afisa mmoja wa polisi ndiye amekuwa
akitoa ushahidi dhidi ya Pistorius hii
leo.

Pistorius amekanusha madai ya
kumuua kwa maksudi mpenzi wake
akisema kuwa alifyatua risasi akidhani
alikuwa anampiga mwizi aliyekuwa
amevamia nyumba yake.
Reeva alikuwa amemlalamikia Pistorius
kwa kumwambia kuwa anahitaji ulinzi
zaidi kutoka kwake kwani hawezi
kushambuliwa na watu wa nje kwa
sababu ya kuwa na uhusiano nae
wakati yeye mwenyewe pia
anamshambulia''

Kesi hiyo, imeingia sasa wiki yake ya
nne huku upande wa mashitaka
ukitarajia kumaliza kuwailisha kesi
yake siku ya Ijumaa.
Afisaa huyo wa polisi alisema kuwa
alipata ujumbe wenye kurasa 35,000
katika simu ya Steenkamp.
Bwana Pistorius aliambia mahakama
kuwa alisahahu nambari ya siri ya
simu yake punde mauaji yalipofanyika
hali iliyolazimisha polisi kuenda
Marekani kuitaka kampuni ya Apple
kuwawezesha kufungua simu ya Oscar
ambayo ni ya Apple.

Chanzo:-bbc


Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>